Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Friday, July 4, 2014

Baada ya utata wa BET Awards: Iggy Azalea ajibu alivyochukulia maneno ya Nicki Minaj

Baada ya tuzo za BET 2014, kuliibuka maswali mengi kuhusu kama Nicki Minaj kweli alimdiss rapper mwenzake wa kike Iggy Azalea. Minaj aliamua kuelezea na kuweka mambo sawa kwa kile alichokiongea baada ya kushinda tuzo ya ‘Best Female Hip Hop Artist’. 
Nicki aliamua kuzungumzia suala hilo kupitia Twitter na kusema vyombo vya habari vinamuwekea maneno kinywani, ila alichomaanisha ni kuwahamasisha wanawake kuandika wenyewe mawazo na mitazamo yao.

Pia aliongeza kuwa amewahi kumpongeza Iggy kwa mafanikio ya wimbo wake ‘Fancy’ hadharani. 
Naye Iggy aliamua kutumia Instagram kueleza jinsi alivyojisikia na kudai kuwa suala hilo halikumshtua hata kidogo na ameshangaa jinsi watu wanavyotaka kuongea kwa niaba yake wakati hana uhakika wa asilimia 100 kama ni kweli.