Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Tuesday, July 8, 2014

Hizi ndizo sababu za Brazil kufungwa

Huu msemo “siku ya kifo cha nyani miti yote huteleza” umekuwa na maana kubwa kutokana na dhalili waliyopata Brazil.  Goli 1-7 katika mechi ya nusu fainali ni rekodi ya kipekee – wapo wanaosema tatizo ni kocha Felipe Scolari kupanga timu mbona na mfumo mbovu. 

Wengine wanasema hayo ni matokeo ya kumtegemea Neymar kuibeba Brazil, na majeraha aliyopata lilikuwa ni pengo lisilozibika kwa muda mfupi. 

Lakini wapo wanaosema wachezaji wa Brazil walichanganyikiwa kuwakosa Thiago Silva na Neymar. 
Kubwa kuliko yote ni kwamba wajerumani walikuwa vyema sana, wamejiandaa vizuri na hawategemei mchezaji mmoja. 

Na kadri wanavyocheza mechi nyingi ndivyo wanavyozidi kuwa imara. 
Brazil walikuwa wanaishiwa nguvu kila mechi waliyocheza, walikuwa wakirudi kinyumenyume. 

Kimsingi, Brazil walijua tangu mwanzo kuwa hawana timu ya kutwaa taji labda wakute wapinzani dhaifu.
Swali la msingi sasa ni, je Argentina watawamudu waholanzi? Kinyume na hilo, itakuwa fainali ya mataifa ya Ulaya matupu.

Credit Taarifa.