Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Wednesday, July 2, 2014

Kamanda wa Polisi Kinondoni azungumzia tukio la basi la Magereza kushambuliwa kwa risasi

Basi la Magereza lililokuwa limebeba wafungwa/maabusu limeshambuliwa kwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi leo (July 2) katika eneo la Mikocheni, Dar es Salaam. 

Akizungumza na 100.5 Times Fm, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camellius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi. 

Kamanda Wambura amesema ni mapema kutaja nia ya watu hao wenye silaha waliovamia gari hilo kwa kuwa wanaweza kuwa na nia tofauti kabisa na fikra za haraka. 

Tunafanya uchunguzi ambao utatufikisha mahali tuweze kubaini ni nini. Inawezekana pengine kuna wahalifu walikuwa katika harakati za uhalifu ghafla wakaona basi lile ambalo lina askari wazuri wenye silaha wakaanza kulishambulia…inawezekana. Au inawezekana vingine vyovyote ambavyo hatuwezi kufikiri wala kubaini.” Kamanda Wambura ameiambia 100.5 Times Fm. 

Ameeleza kuwa hakuna maabusu yoyote aliyeweza kutoroka katika tukio hilo na kwamba madhara yaliyotokea kwenye gari hilo sio makubwa. Amesema bado hajapata taarifa yoyote ya uharibifu wa mali au upotevu wa mali uliotokea katika eneo hilo kufuatia tukio hilo.

Akizungumzia watu waliojeruhiwa katika tukio hilo, Kamanda Wambura amewataja watatu waliopata majeraha kuwa ni dereva wa basi hilo, mahabusu mmoja na askari mmoja wa kike. 

Kuna baadhi wana michubuko, wale wawili ambao ni dereva na mahabusu mmoja. Lakini kuna askari wa kike ambaye yeye ana majeraha kwenye kifua upande wa kulia. Lakini ni nini kimesababishia michubuko ile hatuwezi kujua kama ni vioo ama ni purukushanai wamejichubua mle ndani au vitu gani.” Amefafanua.

Credit TIMES FM.