Katika maisha ya kawaida ya binadamu, kila mtu huwa anavaa akiwa na lengo flani kutokana na haiba yake.
Japo malengo kwa wakati mwingine hutofautina, ila wote huwa na lengo kuu ambalo ni la kupendeza, kuvutia na kuonekana nadhifu mbele ya watu na jamii kwa ujumla.
Mitindo
tofauti tofauti inayo endana na wakati huwa inabuniwa na kukivutia
kizazi cha wakati huo na pia hukumbana na misuko suko mingi toka kwa
jamii za wakati huo, wengine wakipinga mitindo husika na wengine
wakikubaliana nayo.
Kelele
na malalamiko mengi huwa yanakuwa juu ya uvunjaji wa maadili ya jamii
husika. Jamii nyingine zikisema inavuunja maadili na nyingine zikisema
hakuna tatizo juu ya mitindo husika
.
Kitu cha muhimu ambacho jamii huwa inasahau ni madhara ya mitindo iyo katika mwili wa mvaaji.
Hakuna ubishi na ni ukweli usiopingika kuwa kwa
wakati wa sasa na kizazi cha sasa, mtindo wa uvaaji wa nguo zinazobana
na kuonyesha maumbile ya mvaaji ndio ambao unakubalikwa na kila jinsia
ya sasa.
Kwenye mitaa mingi kwa sasa,ni kawaida kukutana na kina mama na mabinti wenye maumbile makubwa (kibantu) ambapo mara nyingi utakuta wakiwa wamevaa suruali za kubana.
Kwa
aina ya watu hawa, utagundua kuwa suruali zao zimebana kwakuwa wengi
wao huwa hazifungi kwa juu kutokana na maumbile yao na hata kupata tabu pale
wanapo kuwa wanatumia usafiri wa wote mfano daladala, hujikuta kila
baada ya dakika wanavuta nguo zao za juu ili ziwasitiri maana nguo zao
za ndani huwa zinaonekana.
Pia wale kina mama na mabinti wembamba ambao miili yao na maumbile sio makubwa, lakini nao utawakuta wamebanwa kuendana na ngozi za miili yao.
Kwa
vijana wa kiume, wanaamini ya kuwa uvaaji wa suruali na mashati yanayo
endana na miili yao ndio mtindo wa kisasa na unafanya waonekane nadhifu
na kupendeza mbele za watu.
Pia uvaaji wa nguo
za ndani zinazo bana, huifadhi vizuri maumbile yake na humfanya mvaaji
awe huru na kutokuwa na wasi wasi haswa pale inapo tokea kwa bahati
mbaya, akasisimka maumbile yake akiwa kwenye umati wa watu, hii humfanya
asigundulike na yeyote yule na humwepusha pia na aibu na tafsiri mbaya
toka kwa wanao mzunguka maana atakuwa kashikiriwa sawa sawia na nguo
yake.
Hii
ni tofauti na aina za nguo za ndani ambazo huacha sehemu zake za siri
kuwa huru zaidi na hata kumfanya mvaaji asiwe huru pale inapotokea
maumbile yake yakasisimka akiwa katikati ya umati wa watu ambapo
kunaweza pelekea akagundulika na mara nyingine kumwachia aibu kubwa.
Kwa
upande wa kina mama na wadada pia, uvaaji nguo zinazobana sana
(skintight) ambapo mara nyingi huwa zinavaliwa pamoja na nguo za ndani
na huendana na aina ya maumbile ya mvaaji. Kwa mfano wale wenye maumbile
makubwa kama mapaja, inawalazimu kuvaa ili kuepuka kuchubuka mapajani.
Pia mtindo wa
uvaaji wa suruali iliyo bana kwao lazima uendane na kuvalia ndani nguo
inayo bana (skintight) ili kuepuka kuonekana kwa nguo ya ndani au
tofauti na hapo na kutokana na mtindo mvaaji atalazimika kuvaa nguo ya
ndani inayo unganishwa na mikanda midogo midogo tu (bikini) ili tu
asichoreke. Japo sio lazima na huwa inategemea na ustaarabu au mapenzi
ya mtu husika juu ya mtindo wa uvaaji wa suruali inayo bana.
Tofauti
na wengi tufikiliavyo kuwa uvaaji wa nguo za namna iyo inakufanya uwe
huru, kupendeza na hata kuendana na wakati, bila ya kutambua kuwa upande
wa pili wa shilingi kuna madhara makubwa sana ambayo yanasababishwa na
uvaaji wa nguo zinazobana mwili sana.
Tafiti
mbali mbali zilizofanyika na madaktari bingwa sehemu tofauti duniani,
zimekuja na majibu ambayo yanalenga juu ya madhara ya uvaaji wa nguo za
aina iyo.
Yafuatayo ni madhara yanayo sababishwa na uvaaji wa nguo za kubana upande wa wanaume na wanawake pia.
1: Kuharibika kwa mishipa ya fahamu
Hii inatokana na ukweli ambao haupingiki kuwa damu
katika mwili wa binadamu inasfiri kwa kasi, na kwa kubana sana misuli
ya damu kunako sababishwa na uvaaji wa mtindo huo, hupelekea kuharibu na
kuua neva za fahamu.
2: Ugumba
Kwa
kiasi pia huchangia ugumba kwa wanaume na wanawake. Ubanaji mkubwa
sehemu za siri, huvuruga mishipa na mirija midogo midogo ambayo huusika
katika utengenezaji wa mbegu ambazo hutumika katika kutunga mtoto, ivyo
kusababisha kutokuwa na ubora unao takiwa kwa hali ya kawaida ili
kuwezesha utungwaji wa mtoto. Utengenezwaji katika ubora wa chini na pia
Usafirishaji wake duni, hupelekea mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika
mimba na hata mwanaume kutokuwa na uwezo wa kuwezesha mimba kutungwa
3: Kupungua kwa nguvu za kiume
Hili
ni tatizo ambalo linawapata haswa wanaume. Korodani za mwanaume zina
hifadhiwa na ngozi ambayo hutengeneza joto hitajika kwa ajiri ya
utengenezaji wa manii. Kunapokuwa na baridi kali, ngozi husinyaa na
kurudisha korodani ndani ili kupata joto na kunapokuwa na joto sana,
korodani hurudishwa nje ili kupata joto la kawida. Ivyo kulibana sana
kunafanya uvurugaji wa kuingia na kutoka nje kwa korodani na pia kuharibu mishipa midogo midogo ambayo husambaza na kusafirisha mbegu ivyo kuathiri uzalishaji na usambazaji wa mbegu.
4: Kupata fangasi sehemu za siri.
Hii
inatokana na joto kubwa ambalo husababishwa na uvaaji wa nguo inayo
bana ivyo kutoa nafasi kwa bacteria ambao husababisha fangasi katikati
na pembeni mwa sehemu za siri
5: Kuharibu kibofu cha mkojo.
Msukumo
usio wa kawaida unao ongezeka kwenye kibofu cha mkojo unao sababishwa
na uvaaji wa nguo zinazo bana, hupelekea bacteria kuzaliana kwa wingi na
kuingia kwenye njia ya mkojo na ivyo kuharibu kibofu na njia pia ya
mkojo.
6: Mapaja kufa ganzi (Meralgia Paresthetica)
Pia
hii inatokana na kukazwa sana kwa mishipa inayo safirisha damu, na
misuli pia hushindwa fanya kazi yake kwa ufasaha, ivyo kufanya mapaja
kufa ganzi.
Makala kwa msaada wa kampuni ya TENA inayo husika na kampeni ya usalama wa watumiaji wa bidhaa mbali mbali pamoja.