David Luiz |
Mabingwa hao mara tano walinyukwa na Ujerumani 5-0 ndani ya dakika 29 za kipindi cha kwanza.
“Walikuwa vizuri zaidi yetu”, alisema Luiz ambaye alikuwa nahodha badala ya Thiago Silva.
“Ni siku ya huzuni ila pia ni siku ya kuanza kujifunza”.
“Naomba radhi kwa watu wote wa Brazil. Nataka kuona watu wangu wakitabasamu.”
Naye mlinda mlango wa Brazil Julio Cesar alidai kuwa timu yao ilikuwa kwenye “maruerue”.
Julio Cesar, 34, alisema: “Palikuwa pamendeza”.
“Nawashukuru watu wa Brazil, mashabiki wanapaswa kupongezwa kwa msaada waliotupa.
“Wachezaji wataomba radhi, Ujerumani walikuwa na nguvu, lazima tulikubali hilo”, alisema.