Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Wednesday, July 2, 2014

Safari ya mchujo kwa washiriki wa TMT yaanza rasmi

Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza.
Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza.  Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane. 

Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane. 

Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678 

Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno "TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki" kwenda namba 15678