Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Monday, July 21, 2014

Tudd Thomas azungumzia mpango wa kutengeneza headphones zake kama Dr Dre , msikilize hapa

Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya, Tudd Thomas anautamani u-millionaire wa Dr Dre alioupata kupitia biashaara ya headphone, na yeye ameamua kutengeneza headphone zake kwa ajili ya muziki wa Bongo Flava na Afrika alizozipa jina la TTP (Tudd Thomas Production).

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Tudd amesema tayari ameshafanyia kazi tangu mwaka jana na hadi sasa ameshapata kiwanda ambacho kimeanza kuifanyia kazi idea yake.

Amesema aliangalia headphones zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi, kama headphones za Dr Dre na ndipo alipopata idea ya kufanya kitu kwa mtindo wa Tanzania.

Wakati mimi naanza kufanya production rasmi, alikuwepo mtu ambaye anatusimamia mimi na Marlaw anaitwa Ben Konzo, ana kampuni ya kutengeneza subwoofer na TV na simu zake. Kwa hiyo nilimfuata yule nikamuomba aweze kunielekeza.” Amesema Tudd Thomas.

Kwa hiyo akanielekeza nini cha kufanya, ukiwa na mtaji hivi na hivi unaweza kufika hapa. Kwa hiyo nikatafuta income na mpaka sasa hivi nimeshazicreate zile headphones na wameshatutumia sample kwamba ‘je mnataka iwe hivi?’. Nikasikiliza sound haikwenda sawa na unavyotaka. Kwa sababu nataka headphone nayoitengeneza iwe na sound ambayo mimi naitaka, akisikiliza bongo fleva awe anaenjoy.” Ameeleza.

Amesema soko analolilenga zaidi ni la ndani na anataka headhone zake ziwe maalum kwa kusikiliza muziki aina ya Bongo Flava.

Tudd amesema headphone yoyote ambayo inatengenezwa kuna mtu ameitengeneza kwa wazo la jinsi anavyotaka isikike kitaalam hivyo yeye pia anataka mtumiaji anapotumia kusikiliza Bongo Flava apate kile alichokitarajia.

Asilimia kubwa ya wanaotengeneza headphone ni watu kutoka nje, kwa hiyo huwa wanaifikiria sound yao wenyewe. Kwa hiyo nachokifikiria mimi naifikiria sound yetu sisi Africans, fusion…kwa sababu fanya vyovyote unavyofanya, muziki wetu sisi unasound tofauti na muziki wa Ulaya. Kwa hiyo naweka kile kitu ambacho kitakuwa best kwetu, tuenjoy sisi wenyewe.”

Sikiliza hapa chini

Credit Times FM.