Mascara inatumika kuongeza urembo na mvuto wa kope zako, kazi ya mascara ni kuongeza mvuto wa kope zako kwa kuongeza ujazo na urefu wake. Mascara zinakuja katika aina mbalimbali tofauti na zenye matumizi mbalimbali, zipo za kuongeza urefu wa kope, za kuongeza ujazo wa kope,za kunyoosha na kukunja kope katika rangi mbalimbali nyeusi, kahawia(brown), blue, colourless na kijani.
Angalizo wakati wa kuchagua mascara:
- Kama una kope fupi tafuta mascara inayoongeza urefu (lengthening mascara) ili kuongezea urefu wa nyusi zako na kuzifanya ziwe na mvuto zaidi.
- Kama una kope nyembamba/hazijajaa kiasi cha kutosha tumia mascara inayoongeza ujazo(voluptuous mascara)
- Kama una kope ndefu tumia mascara inayokunja nyusi (curling mascara) itakayozifanya kope zako ndefu zijikunje kwa madaha zaidi na mvuto zaidi.
- Kama una macho yaliyo sensitive tumia gentle mascara ambazo ni maalumu kwa macho sensitive ni nzuri kwa wanaovaa contact lens pia sababu hazileti muwasho na kuvimba kwa macho.
- Mascara ya rangi nyeusi huwa inatumiwa zaidi sababu inaweza kutumika katika mazingira mbalimbali na kwa macho ya rangi yoyote (blue, black and brown eyes)
- Izungushe brush ya mascara kwenye chombo chake ili kupata kiasi cha kutosha cha mascara katika brush.Usiipump brush kwenye tube yake hii itasababisha hewa kuingia na kusababisha mascara ikauke.
- Futa kiasi kilichozidi kwa tissue au pembezoni ya tube yake ili upate kiwango unachohitaji ile iliyozidi huwa haileti muonekano mzuri machoni.
- Shikilia brush kwenye mwisho wa kope zako na izungushe kiasi na ipake kuelekea mwisho wa kope zako.
- Anza na kope za chini na malizia na zile za juu kope za chini zipakwe kiasi kidogo cha mascara.
- Ongezea ujazo kwa kuongeza layer za mascara kiasi unachokihitaji huku ukisubiri ikauke kabisa kabla ya kurudia kupaka tena.
- Kama kuna fundo(clump) kwenye kope ichane kwa kutumia brush yake.
- Zingatia yafuatayo:
- Muda wa kuisha mascara ili kuepusha madhara kwa macho yako inashauriwa kubadilisha mascara kila baada ya miezi mitatu.
- Toa mascara kwenye macho kwa kutumia make up remover na nawa vizuri kabla ya kulala.
- Usishee mascara na wengine hii itakuepusha kutokupata maambukizi ya macho kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
- Kabla ya kugusa macho na uso wako hakikisha mikono yako ni misafi kwa kuiosha kwa maji na sabuni.
- Macho ni kiungo pekee (delicate) tuyatunze na kuyajali kila siku.