Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 31, 2014

Video: Mapokezi ya Diamond Platnumz July 30 Dar es salaam

Ni mamia ya wakazi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioamua kwenda kumpokea Diamond Platnumz baada ya safari yake ya kutoka Marekani ambayo imekua njema kwa Tanzania baada ya kurudi na tuzo.

Mapokezi yalianzia  uwanja wa Julius Nyerere International Airpot kisha msafara ukaelekea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ukipitia Buguruni,Kariakoo na baadae kumalizia nyumbani kwake Sinza.

Wakati akiwa kwenye gari ya wazi Diamond Platnumz muda wote alikua kaishikilia tuzo yake aliyoipata Marekani kwenye tuzo za AFRIMMA ambapo kwa upande wake ameibuka na ushindi wa tuzo ya Msanii bora wa Afrika Mashariki.

Ratiba ya Diamond kuingia Tanzania ilikua July 29 lakini kutokana na sababu walizosema zilizokuwa nje ya uwezo wao safari yao ikasogezwa mpaka July 30 na alifanikiwa kuingia saa 1 asubuhi.

Ingawa hali ya hewa ilikua imetawaliwa na manyunyu pamoja mvua ndogo ndogo,Hizi ni baadhi ya picha za mashabiki waliojitokeza kumpokea Diamond.

Pia Diamond Amesema haya
Japokuwa nina show Canada tareh 2 lakini ilinibidi kwanza nilete Mzigo nlioagizwa na Wananchi Nyumbani kisha ndio nirudi kuendelea na shughuri zangu!... Kama wasemavyo "There is no place like Home... Ever!"