PRODYUZA anayefanya vizuri kwa sasa hapa nchini katika utayarishaji wa muziki wa kizazi kipya, Mensen Selecta kutoka Studio ya D Fatality, amekanusha uvumi unaozidi kutanda kuhusiana na kuwabeba wasanii kutoka Arusha ili ‘kuwaboost’ na kuwaweka juu kwenye ‘game’.
Akizungumza kupitia Global TV Online, Selecta amesema kufanya kazi na wasanii kutoka mkoani humo haimaanishi kuwa yupo kwa ajili ya wasanii kutoka mkoa huo, bali anafanya nao kazi kwa kigezo cha kuangalia kipaji.
“Arusha mimi ni nyumbani kwangu lakini haimaanishi kuwa nipo kwa ajili ya wasanii kutoka huko, kwa kifupi mimi naangalia kipaji cha msanii na siyo kumbeba mtu,” alisema Mensen.
Monday, July 14, 2014
Video: Producer Mensen Selecta aeleza kuwa hayupo kwaajili ya wasanii wa Arusha tu
Labels:
Entertainment,
Video