Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Sunday, August 3, 2014

Jose Chameleone afunika Dar

Onesho kali kabisa la msanii Jose Chameleone jijini Dar es Salaam, Tubonge Concert limefanyika kwa mafanikio makubwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Maisha Club, na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wapenda burudani.
Chameleone Jukwaani Maisha Club Dar Usiku wa kuamkia leo

Kivutio kikubwa katika usiku wa onesho hilo, ni namna wasanii walivyoshambulia Jukwaa, mashambulizi yakianzishwa na mwanadada Vanessa Mdee, vilevile msanii Mirror, huku Chameleone mwenyewe akipata sapoti ya nguvu kama surprise kutoka kwa msanii Ferouz na Proffesa Jay, na TID. 

Chameleone aliwapatia ladha mashabiki kwa kuimba moja kwa moja nyimbo zake kali za kuanzia zamani ikiwepo Bomboclat mpaka nyimbo mpya ya Wale Wale. 

Wasanii wakali pia kama vile Barnaba Classic na Chidi Benz kati ya wengine walikuwepo eneo la tukio kufuatilia show hii kali. 

Onesho hilo kali limefanyika kwa udhamini mkubwa wa East Africa Radio na East Africa TV.