Kipi sijasikia ni wimbo mkubwa wa msanii mwenye heshima kubwa katika game la bongo flava na asiyechuja, Profesa Jay ambaye amemshirikisha msanii anae-kick zaidi katika kizazi cha bongo flava kinachoanza miaka ya 2000, Diamond Platinumz.
Lakini pia moja kati ya nyimbo zilizokuwa na utata na kuvuta usikivu wa watu wengi ni wimbo wa KKK(Karibu Kwenye Karamu) wa Roma Mkatoliki ambaye siku zote akitoa wimbo huzua mada nyingi kwenye media na mitandaoni huku akizungumzia mambo mengi katika dakika chache za wimbo wake.
Profesa Jay na Roma Mkatoliki wote katika nyakati tofauti wameongea na tovuti ya Times Fm na kuzungumzia video zao zinazofanyika hivi karibuni ambapo wote wamemtaja muongozaji mkongwe wa video za muziki Tanzania, Adam Juma kuwa ndiye atakayeongoza video hizo.
“Video ataisimamia director anaitwa Adamu Juma wa Visual Lab. Watu wanamjua ndiye director bora zaidi wa video aliyewahi kutokea Tanzania na ameboresha sana mashine zake, ameboresha sana vitu vingi.” Amesema Profesa Jay.
Katika video hiyo itakayofanyika Jumamosi, July 12 Profesa Jay amewaalika mashabiki wote kuvaa smart kwa jinsi wanavyoweza na kushiriki kwenye video hiyo.
Kwa upande wa Roma ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa atafanya video yake na Adam Juma na kwamba wataifanya katika mazingira tofauti ambapo vipande vingine vitashutiwa mikoani.
Katika hatua nyingine, Adam Juma ameandika kwenye Instagram ujumbe unaoleza kuwa anaipenda sana kazi yake ya kuongoza video za muziki na kwamba anaipenda kwa sababu imemkutanisha na watu wengi.
Usikikosea kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm na Jabir Saleh na DJ D Ommy kuanzia saa mbili kamili usiku hadi saa nne kamili utawasikia Roma na Profesa Jay wakieleza kiundani.
Unaweza kusikiliza kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.
Thursday, July 10, 2014
Adam Juma kuongoza video mbili nzito, Profesa Jay 'Kipi sijasikia' na Roma 'KKK'
Labels:
Entertainment