Wikendi iliyopita tasnia ya sanaa za filamu na muziki ilipata ugeni uliowezeshwa na mheshimiwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kwa lengo la kuongeza weledi na uzoefu wa masuala ya sanaa kwa mtazamo wa dunia kwa ujumla.
Ugeni huo uliwahusisha wasanii na wafanyabishara wakubwa katika kiwanda cha sanaa za aina hiyo, Terrence J (Muigizaji,
Mwandishi wa vitabu na mtangazaji), David Banner (Mtayarishaji wa muziki aliyewahi kushinda tuzo ya Grammy, rapper), Chaka Zulu (Meneja wa wasanii wakubwa na mmiliki wa label inayomhusisha Ludacris ‘DTP’), Ravi (Mfanyabiashara mkubwa katika kiwanda cha sanaa).
Mtangazaji wa kipindi cha The Switch cha 100.5 Times Fm, Cnda King alifanya mahojiano na wasanii hao Jumamosi (July 12). Isikilize hapa interiview yote na usikose kusikiliza The Switch ya 100.5 Times Fm kila Jumamosi saa sita kamili mchana hadi saa kumi kamili jioni.
Tuesday, July 15, 2014
Audio: Sikiliza Interview ya The Switch ya Times FM na Terrence J, David Banner, Chaka Zulu na Ravi
Labels:
Entertainment