Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Monday, July 14, 2014

Audio: Terrence J asema atachuma 'madini' ya wasanii wa Tanzania na kuwapa aliyonayo

Mtangazaji, muigizaji na mwandishi wa vitabu kutoka Marekani Terrence Jenkins ambaye ameletwa nchini na mheshimiwa rais Jakaya Kikwete, anathamini kile ambacho wasanii wa Tanzania wanacho na anakihitaji sana pamoja na kwamba amekuja kwa lengo la kuwapa/ kufundisha na kushare uzoefu alionao katika kiwanda cha sanaa ya kimataifa.

Terrence J ambaye ameongozana na Chaka Zulu (Meneja wa wasanii na mmoja wa waanzilishi wa lebel ya DTP  ya Ludacris), David Banner (rapper na Producer na Muigizaji)  na Riva Shalton (Mfanyabiashara Mkubwa katika sanaa) ameeleza uhitaji wao wa kubadilishana maarifa na wasanii wa Tanzania alipokuwa anafanya mahojiano na kipindi cha The Switch cha 100.5 Times Fm, Jumamosi (July 12).

Nahisi kama nina mengi ya kujifunza nitakaporudi. Nimekuwa nyumbani, ni uzoefu mzuri na nataka kujifunza. Watu wengi wanasema wanataka kujifunza kutoka kwetu lakini tumekuja kujifunza kutoka kwenu pia.” Alisema Terrence J.

Nadhani nchi yenu ina ‘turning point’ nzuri na ya kuvutia (kuifahamu) na wasanii wa hapa ni wazuri wa kushangaza sana na wana mzuka sana. Na sisi tunadhani ni vitu ambavyo tunaweza kuvifyonza na tukarudi nyumbani tukiwa bora zaidi.” Amesema Star huyo wa Think Like A Man Too na mtangazaji wa E! Entertainment.

Ameielezea njaa na mzuka anaomini watanzania wanayo kujifunza kutoka kwao ni sawa sawa na njaa waliyonayo kujifunza kutoka kwa wasanii wa Tanzania.

Sikiliaza hapa.


Credit Times FM.