Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Monday, July 14, 2014

Baada ya kuvamiwa na kupigwa, Ray C asema itakuwa Chid Benz amechanganyikiwa kwa madawa

Msanii wa muziki na mmiliki wa Ray foundation, Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kusema kuwa alhamisi (july 10) alivamiwa na kupigwa na msanii Chid Benz.

Ray C amesema kuwa Chid Benz anatafutwa na polisi baada ya kufanya tukio hilo.
“kweli alinivamia alhamisi usiku, amenipiga mimi na amefanya uharibifu wa mali, mimi nashangaa usiku navamiwa ata sikujua nani amemuonyesha nyumbani kwangu, mimi nilikuwa namtafuta kwa sababu ya show ya kuelimisha vijana na maswala ya madawa ya kulevya, yeye akalichukulia kivingine kabisa, nahisi amechanganyikiwa na madawa ya kulevya, kweli itakuwa amechanyikiwa na madawa, hayuko sawa kabisa.

Sasa hivi nina RB yake , kwaiyo anatafutwa na polisi, kokote atakapo kamatwa anawekwa ndani, najua atajifisha lakini ipo siku atakamatwa na polisi tu. 
Watanzania wanatakiwa kushirikia na polisi ili akamatwe kwa sasabu Chid hayuko sawa kabisa” Alisema Ray C.