Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 10, 2014

Justin Bieber ahukumiwa kufanya kazi za jamii na faini kwa kosa la kurusha mayai kwa jirani

Nyota wa muziki wa Pop, raia wa Canada Justin Beiber amejitetea kupinga tabia yake mbaya ya uharibifu inayohusisha urushaji mayai kwenye nyumba ya jirani yake, amehukumiwa miaka miwili ya kua chini ya uangalizi. 

Mahakama ya mjini California imemtaka kulipa faini dola 80, 900 (mil. 135) ya uharibifu, kutumikia jamii kwa siku tano na kumaliza mpango wa kumudu hasira zake.  Beiber, 20, hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu. 
Mwanamuziki huyo pia anakabiliwa na kesi mbili nyingine za jinai huko Florida na Toronto. 

Justin ana furaha kuona masuala yake yanatatuliwa”, alisema mwakilishi wake. 
Ataendelea kuzingatia kipaji chake na maisha yake ya muziki”, aliongeza.