Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 10, 2014

Kassim Mganga ajipanga kwa soko la kimataifa

Msanii hodari kwa kuimba nyimbo za mahaba kama anavyojulikana Tajiri wa Mahaba, Kassim Mganga ameeleza mpango wake wa kupeleka video zake kwenye vituo vya runinga vya kimataifa kama wanavyofanya wasanii wengine kama Diamond, AY, Shetta na wengine.

Akiongea na Times Fm, Kassim ambaye jana ameachia wimbo wake mpya ‘Motomoto’ amesema tayari yeye na menejimenti yake wameshajipanga kufanya kuzipeleka video zake kwenye vituo kama Trace, MTV na Channel O na kwamba wanaenda hatua kwa hatua. 

Safari lazima iwe na ngazi, huwezi kutoka namba moja ukaenda namba kumi direct, lazima upite namba mbili, tatu, nne, tano hadi ufike kumi.  
Huenda hapa tulipo tuko kwenye namba saba kwa hiyo InshaAllah watu watarajie kutuona huko pia,” alisema Kassim. 

Akizungumzia kitu kilichokuwa kikwazo kwake kufika level hizo, amesema vipo vitu vingi vilivyokuwa vinakwamisha lakini kwa sasa wako imara na kampuni yake ya Manzabay na wako tayari kufika mbali. 

Sasa niko imara tumejijenga na kampuni yangu ya Manzabay na timu yangu kwa ujumla. Menejimenti yangu iko strong na tunafocus. Na mfano utaonekana hivi punde kwa sababu tumefanya jambo tayari na inshallah litakuwa jambo”, alieleza Kassim Mganga.