Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Wednesday, July 30, 2014

Lady Jaydee awashukuru mashabiki baada ya kushinda tuzo ya AFRIMMA

Lady Jaydee na Diamond July 27 walitangazwa kuwa washindi katika tuzo za AFRIMMA 2014 nchini Marekani.

Diamond alishinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume Afrika mashariki, huku Lady Jaydee alishinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kike Afrika mashariki. Tuzo hizo ziliwashindanisha wanamuziki mbalimbali wakubwa wa Afrika wakiwemo Davido, Mafikizolo, Tiwa Savage, Fally Ipupa, Flavour na wengine. 
Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Facebook aliwashukuru mashabiki wake, aliandika: 
Nashukuru wote mnaokubali kazi zangu, wote mnaosimama na kutetea JayDee bila kusita, nashukuru kwa Tuzo nyingine tena toka AFRIMMA . Wahenga walinena kuwa utavuna ulichopanda, mapenzi tele kwa kila mtu

Katika post nyingine Jide amepost picha ya tuzo yake na kuandika: 
Tuzo yangu ya 30. Asanteni kwa ushirikiano, nimeipokea na ninarudi nayo nyumbani. Shhhhhh! !!! Kimya Kimya”.