![]() |
Neymar Jr. atakosa mechi ya leo ya kuwania mshindi wa tatu kati ya Brazil na Uholanzi baada ya kupata majeruhi ya kuvunjika mshipa wa mgongo kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia. |
Neymar aliweza kutembea bila msaada kwenda kuwasalimia wachezaji wenzake, ambao walikuwa wakifanya mazoezi wakati anawasili. Na atakuwa na timu hiyo wakati wa mechi ya kugombea mshindi wa tatu watakapominyana na Uholanzi siku ya Jumamosi.
Brazil bila mfungaji wao, tumaini la kunyakua taji hilo la dunia kwa mara ya sita lilizimika baada ya kuchapika magoli 7-1 na Ujerumani siku ya Jumanne.
Nyota huyo, 22, amekuwa akipona taratibu nyumbani kwake baada ya kupata majeraha kwenye mechi ambayo Brazil ilishinda 2-1 dhidi ya Colombia.
Klabu ya Barcelona ilithibitisha kutuma madaktari wake kumtembelea mchezaji huyo na wanaamini atakuwa fiti wakati ligi yao itakayoanza Agosti 23.
“Mchezaji wetu anaendelea vizuri, na ataendelea na matibabu mjini Barcelona yatakayoanza Agosti 5”, ilieleza taarifa ya klabu.