Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Wednesday, July 16, 2014

Picha: Atumia zaidi ya Milioni 49 kufanya upasuaji afanane na Kim Kardashian

Kupenda ama kutamani kuwa kama star fulani unaemkubali hakuna sheria ya mipaka zaidi ya mwenyewe kuthibiti hisia zako zisipitilize, lakini wapo wengine ambao wamechoka kutamani kuwa kama fulani na wameamua kutumia nguvu kuwa kama yeye. 

Claire Leeson, msichana mwenye umri wa miaka 24, mkaazi wa Landani ametumia zaidi ya $30,000 (Tsh 49,755000)kufanya upasuaji ili afanane na Kim Kardashian. 

Claire ameiambia This Morning kuwa aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa shuleni wenzake walikuwa wanamcheka na kuuita ‘mbaya’ kuliko kitu chochote kilicho hai. 

Nilikuwa naambiwa kila siku mimi ndiye mbaya kuliko kitu chochote kilicho hai na kwamba inabidi nijiue. Nilipoacha shule marafiki zangu waliniambia kuwa ninavitu ambavyo vinafanana na Kim Kardashian.” Amesema Claire. 

Ameeleza kuwa baada ya kuambiwa hivyo na marafiki zake aliamua kuanza kuangalia kwa makini Keeping Up With The Kardashians na akagundua kuwa kweli kuna vitu ambavyo wanafanana na Kim Kardashian. 
Tunafanana katika mabishano na vitu vingine. Nikafikiri ni mzuri sana na kwa kweli nilitaka kufanana nae.”

Boob Job- $8500  
Teeth Whitening-$4300 
Hair Extensions-$7700 
Make-up-$1700 
Spray Tans-$1700 
Nails-$850 
Bum Padding-$600 
Shoes and Clothes-$5400
Hata hivyo, msichana huyo ambaye kwa kiasi fulani zoezi hilo limemuweka katika madeni amesema anaona alichokifanya kinathamani ya fedha aliyotoa.