Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Sunday, July 20, 2014

Picha: Diamond kamvalisha Wema pete ya ndoa!

SAPRAIZ! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana akirandaranda na pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa siri kubwa.

Baada ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao wamefunga ndoa ya siri.

Kuna maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka 2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.

Wiki iliyopita jitihada za kumnasa Wema akiwa na pete ya uchumba zilizaa matunda ambapo mwanahabari wetu alimuweka ‘mtukati.
Wema alipotakiwa kuanika ukweli juu ya pete hiyo, alikubali na kueleza kuwa ameamua kufunguka kwa mwanahabari wetu baada ya kuwa kimya tangu alipovishwa pete hiyo.

Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) akionyesha pete aliyovishwa na Diamond.
 
Wema alisema si kweli kwamba amefunga ndoa ya siri ila Diamond alimvisha pete hiyo kama urembo akijua kabisa kwamba yeye ni wife material (anafaa kuwa mke).
“Sijafunga ndoa jamani. Hii pete alininunulia baby wangu Nasibu (Diamond) wakati tukiwa South Africa (Afrika Kusini).

“Alininunulia na kunivisha tulipokwenda kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA). Nakumbuka tuliingia kwenye duka moja nikaiona hii pete ikanivutia sana, nikamwambia Nasibu ndipo akaninunulia na kunivisha palepale.

“Cha kushangaza ni kwamba imewatatiza wengi na kuhisi ndoa tayari. “Hii pete ndogo niliinunua mwenyewe  hapahapa Bongo na kuivaa kama urembo tu, hakuna tofauti na hilo kuhusiana na hizi pete nilizovaa kidole husika,” alisema Wema ambaye kidoleni kwake kunaonekana pete mbili, kubwa na ndogo.

Alipoulizwa kwa nini Diamond aliamua kumvisha pete hiyo kabla ya ndoa, Wema alifunguka: “(kicheko) hilo sina uhakika nalo but amegundua mimi ni wife material hataki kunipoteza. Kanipa heshima anayostahili kupewa mwanamke...”

Wakati huohuo, Wema amemshukuru mtabiri, Maalim Hassan Yahya ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alitabiri kuwa mastaa hao wataoana mwezi ujao (Agosti) mwaka huu akiomba Mungu na iwe hivyo.
“Natamani hiyo ndoa na nasubiria hiyo siku ili utabiri utimie, ni jambo la heri jamani,” alisema Wema.

Alipotafutwa Diamond ili afunguke kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa. Wakati huohuo, mashabiki wa mastaa hao, wamewashauri mama Wema na mama Diamond kuwa kitu kimoja ili kufanikisha ndoa hiyo ya watoto wao.

Ukiacha pete hiyo ya ndoa aliyovishwa na Diamond, Wema aliwahi kuvishwa pete kama hiyo alipofunga ndoa na jamaa aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe ambayo haikudumu hata mwezi mmoja.

Credit GPL.