Mwimbaji na muigizaji wa kike, Selena Gomez ameamua kutumia mwili wake kuweka ujumbe wa mapenzi kwa lugha ya kiarabu kwa kujichora tattoo mpya.
Mrembo huyo ambaye ni mpenzi wa Justin Bieber amepost picha kwenye Instagram Jumatano, July 16 ikionesha tattoo iliyochorwa upande wa kulia juu kidogo ya mgongo ikiwa na ujumbe wa kiarabu uliotafsiriwa kuwa ni ‘Love Yourself’, yaani Jipende.
Mchoraji wa tattoo hiyo pia alipost picha hiyona kuandika ‘Little gift for my friend @selenagomez”.
Thursday, July 17, 2014
Picha: Selena Gomez ajichora tattoo ya kiarabu yenye ujumbe wa mapenzi
Labels:
Entertainment,
Fashion,
Life Style,
Photos