Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Tuesday, July 15, 2014

Selena Gomez ajibu comment ya shabiki aliyemuombea afe kwa saratani

Wasanii wakubwa hupata likes na comments nyingi kutoka kwa mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha wengi kufikiria kwamba huenda huwa hawazisomi comments. Lakini mwimbaji na muigizaji maarufu wa kike Selena Gomez ameonesha kuwa hufuatilia comments za mashabiki wake. 

Kupitia Instagram, Selena amemjibu shabiki wa kike ambaye aliandika comment ya kumuombea afe kwa ugonjwa wa saratani, akaunti ambayo ilikuwa deactivated muda mfupi baada ya kupata jibu la busara la Selema Gomez. 

Comment ya Selena ilimueleza msichana huyo jinsi ambavyo hakupenda kile alichoandika kama msichana mdogo na kueleza kuwa yeye amepitia hayo na mashabiki na familia. 

Alimshauri kuwa unaweza kuwa haumpendi mtu lakini kumuombea kitu ambacho kinaweza kutokea kwako ama kwa familia yako hakukubaliki. Zaidi alimuomba ajifunze zaidi huku akimoumbea  abarikiwe. Tofauti na maelezo ya shabiki huyo, selena alimsifu kuwa ni mwanamke mzuri.