Mapigano makali yanayoendelea kati ya Israel na Palestina na kusababisha mauaji ya watu wengi bila kuwepo dalili za kusitishwa hivi karibuni yamepelekea nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kupaza sauti kuzitaka pande zote mbili kusitisha mapigano hayo.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe amezungumzia mapigano hayo katika mkutano na mabalozi wa nchi mbalimbali nchini ambapo amezitaka nchi zote mbili kusitisha mapigano na pia jumuiya ya kimataifa kuingilia kati ili kurudisha hali ya usalama.
“Kuna mauaji makubwa sana yanayotokea kati ya pande zote mbili za Israel na Palestina, ya kutisha. Makombora yanarushwa na pande zote mbili, lakini huyu mmoja akirusha manati huyu mwingine anarusha bomu. Na matokeo yake wanakufa sana waparestina. Ningependa kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulaani mauaji yanayotokea na hasa dhidi ya Palestina kule kwenye mpaka. Na kuomba pande zote zinazohusika kuacha kufanya hivyo, na tunaomba jumuiya ya kimataifa waingilie tatizo hili badala ya kuacha ndugu zetu wakiumia na kufa kila siku.” Amesema Waziri Membe.
Amesema Tanzania ina uhusiano mzuri wa kidemokrasia na nchi hizo mbili lakini amesisitiza ombi lake zaidi kwa Israel kuacha kufanya mashambulizi kwa kuwa hulipiza kwa nguvu zaidi kwa mfano wa kumshambulia kwa bomu mtu aliyekupiga na manati.
Tuesday, July 15, 2014
Audio: Bernard Membe apaza sauti kwa Palestina na Israel kwa niaba ya serikali ya Tanzania
Labels:
News