Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Friday, July 4, 2014

Ukweli juu ya kilichosikika kwenye kipindi cha XXL July 02 juu ya kuhusiana na ugomvi wa B12, Adam na Fetty

Jumatano July 02 kupitia kipindi cha XXL zilisikika kelele za ugomvi hewani ambazo asilimia kubwa tuliamini kuwa ni za kweli hasa kutokana na baadhi yao kusikika kama wamekabwa huku wengine wakitaja majina ya viongozi kuja studio kuamulia ugomvi huo.

Kila mmoja kwa nafasi yake anatamani kujua chanzo hasa cha kugombana lakini kupitia kipindi cha XXL leo July 04,wameeleza ukweli juu ya kilichotokea na kusema hii wamefanya kwa ajili ya kampeni ambayo Clouds Media Group wanaiendesha kwa sasa waliyoipa jina la Paza Sauti.  xxl3

Kampeni hii inalenga kuhamasisha utoaji wa taarifa ambazo unaziona mtaani kwako kama haziko sawa kutoa taarifa hasa kwa vyombo vya dola ikiwemo Polisi ili kwa pamoja tuidumishe amani tuliyonayo Tanzania,Paza Sauti,Ukimya Hausaidii..

Bonyeza play kusikiliza maana halisi ya Paza sauti.

Credit Millard Ayo.