Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Sunday, July 6, 2014

Vita vikali vyazuka Yemen kati ya jeshi la taifa hilo na waasi wa ki-shia kazkazini mwa taifa

Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa kumekuwa na vita vikali kati ya jeshi la taifa hilo na waasi wa ki-shia kazkazini mwa taifa hilo kufuatia kuvunjwa kwa mkataba wa kusitisha vita uliowekwa mwezi uliopita. 
Jeshi la Yemen
Ripoti moja iliowanukuu maafisa wa eneo hilo imesema kuwa jeshi la angani liliwashambulia waasi hao wanaojulikana kama Houthi siku ya jumamosi na kwamba takriban watu 70 waliuawa. 
Pande zote mbili zili-laumiana kwa kuvunja makubaliano hayo ya kusitisha vita. 

Waandishi wanasema kuwa migogoro ya kidini pamoja na hatua za kuimarisha uhuru wa kikanda ndani ya Yemeni umekandamiza maridhiano ya kitaifa.

Na BBC.