Rapper toka Mwanza, Young Killer Msodoki amepanga kuachia video mpya ya wimbo wake wa My Power aliomshirikisha Damian Soul.
Akiongea na The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Young Killer ameielezea video yake kuwa ni video itakayowasurprise mashabiki wake ingawa itakuwa simple na imeongozwa na muongozaji mpya kwenye tasnia ya video za muziki Tanzania.
“Sio video ambayo imenigharimu kiasi kikubwa cha pesa, hapana. Ila ni video fulani ambayo ni ya kiwango kidogo ila ni surprise nzuri kwa watanzania na watu ambao wanafuatilia muziki wangu na watu ambao wanaupenda muziki wangu. Ni surprise kubwa sana tofauti na watu ambacho wanaotemea wao kuiona.” Amesema Young Killer.
Katika hatua nyingine , rapper huyo mkali ameeleza alitoa mchango wake wa mawazo kuhusu watu mbalimbali wanaodaiwa kuwapa msaada wa pesa nyingi wasanii wa Tanzania ili wafanye video kali tofauti na pesa yao wanayoingiza kwenye muziki. Young Killer ameeleza kuwa yeye hajawahi kupewa msaada huo na inaweza kuwa sababu ya kuendelea kufanya video za kiwango anachopata.
“Kwa mfano wangu tu binafsi naweza kusema nakubaliana na hiyo issue, kwa sababu mimi katika upande wangu wa video hajawahi kutokea mtu akanidhamini ‘Young Killer napenda muziki wako nakusapoti, hebu fanya video hata ya milioni 9 au milioni 10’, haijawahi kutokea hiyo kitu. Lakini nakutana na ‘madon’ kibao tu wananiambia ‘ebana Young Killer napenda sana muziki wako’ na story zinaishia hivo.” Young Killer ameeleza.
Amesema yeye hivi sasa ataendelea kufanya video zenye kiwango anachoweza kulipia ila kwa ubunifu zaidi na kwamba endapo MTV watazipitisha itakuwa heri kwake, lakini wasipopitisha ataendelea kujitahidi kukusanya kiwango alichonacho kadri awezavyo ili siku moja afanye video yenye bajeti kubwa.
“Mimi kadri ninavyofanya show zangu najua ni kiasi gani nitenge bajeti ili nifanye video. Siwezi nikatoa milioni 50 kufanya video wakati mimi show yangu napokea milioni moja. Nimejipanga kwa gharama zangu. Kama MTV wataplay poa lakini wasipoplay nitajipanga upya mpaka nitakapoweza kumudu gharama.”
Credit TIMES FM.
Popular Posts
-
Download wimbo Kamili HAPA MKITO wa Msanii mdogo wa Umri Mkubwa wa akili aka "Jose G" akiwa amemshirikisha Legendary SpacDaw...
-
New Music: Chidi Benz Feat Bob Junior - Mahaba Niuwe
-
New Music: Monii ft Roma & GodZilla - Hatuhesabu Masaa
-
Siku 74 baada ya kufunga ndoa na Kanye West huko Florence, Italia Kim Kardashian amefuata taratibu za kisheria na kubadili jina lake rasmi k...
-
Baadhi wanawake siku hizi wamekuwa wakijiuliza vazi gan ambalo linafaa kuvaliwa wakati wa usiku na likawapendeza sasa unaweza kutazama pic...
-
Kindumbwe ndumbwe cha michuano ya klabu Bingwa Afrika mashariki na kati maafuru Kagame Cup kinaanza kesho ambapo mechi ya ufunguzi ya Kund...
-
Men have to love the fact that twerking has gone from the hood other countries around the world. I just hope they don't think Miley Cy...
-
Baadhi ya Mastar wa Tanzania wameamua kuweka wazi nia zao za kugombea nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali,miongoni mwa watu hao kwa ...
Advertisement
Advertisement
Advertisement With Us