Neymar Jr. atakosa mechi zilizobaki za Kombe la Dunia baada ya kupata majeruhi. |
Kiongozi wa vyombo vya habari wa Fifa Delia Fischer alisema: “Kamati ya nidhamu inalitathmini tatizo hilo. Uchezaji wa mpira unatakiwa uwe wa haki na tunataka uepuka matatizo uwanjani”.
Naye mshambuliaji wa zamani na bingwa wa Kombe la Dunia Ronaldo anaamini Zuniga alidhamiria kumuumiza Neymar. Aliongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Rio kuwa:
“Ushindani ulikuwa wa kikatili sana – naamini mchezaji wa Colombia alikuwa na nia ya kumdhuru.
“Sidhani kama ule ni uchezaji wa kawaida, sijui kuwa alipanga ila naamini alionekana mwenye hasira, mkatili”.
Zuniga alitetea uchezaji wake baada ya mechi, akisema hakudhamiria kumuumiza Neymar.
Alisema: “Ilikuwa kawaida, sikudhamiria kumuumiza. Nilikuwa uwanjani, nikichezea jezi ya nchi yangu, na sio kumuumiza yeyote. Nilikuwa nikiitetea nchi yangu”.