Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Friday, July 4, 2014

Genevieve Nnaji awatuhumu waandishi kumuwekea maneno mdomoni kuiponda Nollywood

Muigizaji wa kike wa Nigeria, Genevieve Nnaji amekanusha vikali taarifa zilizoelekezwa kwake kuwa ameiponda kiwanda cha filamu cha Nigeria kuwa ni hakieleweki kwa ubora wake na hazina ladha.  Habari zilizoandikwa na waandishi wa habari na kukaririwa kuwa ni maneno aliyoyasema muigizaji huyo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja.  
Genevieve Nnaji
Genevive ameandika maelezo marefu kwenye Instagram. 

I never called my industry bland and mediocre. Truth or not, they were NOT MY WORDS. As a person/writer, you can "assume" what you like about my thought process but DO not project those thoughts as "quotes" by me. It's distasteful, insensitive and quite unprofessional. It's insulting to those limited few working hard to make a difference in the industry. I am a product of Nollywood and my loyalty remains unshaken.” 

Katika interview aliyofanya, Genevive aliulizwa kwa nini haonekani kwenye tasnia ya filamu za Nollywood kwa muda mrefu na hapo maelezo yake yakazua mengine. Maelezo haya ndio yaliyozua kesi ya kuwa ameiponda tasnia ya filamu Nigeria. 

“Nadhani bado sijapata script sahihi. Ubunifu na undani ni ubora ninautafuta kwenye script. Mwanzoni, kiwanda cha filamu kilihamasisha zaidi katika wingi lakini vitu vimebadilika na kuna maendeleo katika filamu. Mimi ni mmoja kati aya watu wanaojaribu kupigania ungezeko la ubora katika tasnia. Kwa hiyo, nipo naangalia aina ya story ninazoweza kuwa sehemu yake. Ninasapoti filamu ambazo zinaonesha weledi na ubunifu.

Kwa kuwa nimeshafanya kwa vitendo sanaa yangu katika level ya kimataifa na kwa weledi nimeandaa stories kama ‘Ije’, Mirror Boy’ na Tango With Me’. Sidhani kama ninaweza kurudi kwenye ubora usioeleweka na usiosisimua uliokuwa unachukuliwa kama sifa ya Nollywood huko zamani.”