Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Friday, July 4, 2014

Kabla ya kuikabili Brazil, wakulima wa Kahawa wachapana kavu kavu mjini Fortaleza

Mashabiki wa timu ya taifa ya Colombia, wakiwepo watu maarufu wa nchi hiyo wamezichapa kavu kavu katika moja ya mijahawa mjini Fortaleza, ikiwa ni saa kadhaa kabla ya mpambano wa hatua ya robo fainali, ambao utashuhudia timu yao ya taifa ikipambana na Brazil. 

Miongoni mwa watu walioonekana kwenye zogo hilo ni waigizaji maarufu wa nchini Colombia Manolo Cardona na Carolina Guerra, huku mtoto waraisi wa nchi hiyo Yamid Amat akihusika pia. 

Chanzo cha ugomvi baina ya mashabiki wa Colombia walikuwa kwenye mgahawa huo hakijafahamika mara moja, lakini kila mmoja alionekana ni mwenye hasira kabla ya wasamaria wema hawajawatuliza. 

Ugomvu huo umeacha hasara kubwa katika mgahawa huo, kufuatia mashabiki hao wa Colombia kurushiana vitu vya kuvunjika kama sahani pamoja na bilauri, hali ambayo ilizua taharuki kwa wateja wengine waliokuwa wakiburudika mgahawani hapo. 

Timu ya taifa ya Brazil itapambana na Colombia katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia mishale ya saa kumi na moja kwa saa za nchini Brazil lakini kwa hapa nyumbani itakuwa saa tano usiku katika dimba la Estádio Castelão