Baada ya taarifa kutoka kwa msanii Cindy wa Uganda kuelezea nia ya kufanya kolabo na kundi nyota la nchini Rwanda-Kigali, tayari kundi hilo limeweka taarifa wazi kwa mashabiki wao kuwa wamekubali kufanya nae kazi.
 |
kundi la Urban Boys nchini Rwanda |
Kundi hilo linalofanya miondoko ya Afro-Beat limekubali kufanya kolabo na Cindy baada ya mwanadada huyo kulifagilia kundi hilo baada kutumbuiza vyema hivi karibuni katika sherehe za siku ya ukombozi zilizofanyika hivi karibuni nchini Rwanda.
 |
Cindy Sanyu |
Mmoja wa memba wa kundi hilo Humble Gizzo ameelezea kuwa wanashukuru kupata sapoti yake kwani kufanya nae kazi itawasaidia kuukuza muziki wao zaidi ndani ya nchi za Afrika Mashariki.