Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 3, 2014

Urban Boys waanza 'kushine' wamelamba dili la kurekodi na kundi nyota la muziki Mafikizolo

Nyota imeanza kung'ara kwa kundi la Urban Boys ambao hivi karibuni wasanii hao wamelamba dili la kurekodi na kundi nyota la muziki Mafikizolo kutoka nchini Afrika Kusini.
Urban Boys
Dili hilo limetua punde tu walipotoa wimbo wao mpya uliobatizwa jina 'Tayali' wakimshirikisha nyota wa nchini Nigeria Iyanya ukiwa ni wimbo unaofanya vyema katika stesheni mbalimbali nchini humo. 
Mafikizolo
Memba wa kundi hilo la Urban Boys Said Safi, amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha nyaraka zote muhimu kwa ajili ya msafara wa kuelekea nchini Afrika Kusini kurekodi nyimbo na kundi hilo maarufu la Mafikizolo.