Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Saturday, July 5, 2014

Katy Perry ashtakiwa na marapa wa nyimbo za Injili kwa uizi wa mistari

Nyota wa muziki kutoka nchini Marekani Katy Perry ameshtakiwa na marapa nyota wa nyimbo za Injili akiwemo mwanamuziki Flame ambaye amedai kuwa nyimbo ya Dark Horse ya Katy imeiba baadhi ya mistari kutoka kwenye nyimbo yao ya Joyful Noise. 
Wanamtuhumu Katy Perry kwa kutumia nyimbo yao iliyotoka mwaka 2008 waliyomshirikisha Lecrae bila ruhusa na kuharibu ujumbe wa kidini uliopo ndani ya nyimbo hiyo na kutumia picha za “kichawi” na nguvu za kidunia.

Nyimbo ya Dark Horse iliongoza katika chati za muziki za Billboard kwa wiki kadhaa mwezi January. 

Kundi la marapa wa nyimbo za injili Flame aka Marcus Gray, Lecrae Moore, Emanuel Lambert na Chike Ojukwu wanataka kulipwa fidia na mwanamuziki huyo,, studio yake ya Capitol, na waandishi wa nyimbo Dr Luke na Max Martin kwa kuiba hakimiliki za wimbo wao.