Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Friday, July 4, 2014

Muigizaji filamu wa nchini Nigeria Adokiye angoja jibu la Boko Haram ili awape usichana wake

Mwimbaji maarufu wa nchini Nigeria Adokiye Kyrian, aliyeripoti kuwa yupo tayari kupoteza ubikra wake na achukuliwe na kikundi cha ugaidi cha Boko Haram, ashangazwa kutopata majibu yeyote kutoka kikundi hicho.

Adokiye ambaye pia ni muigizaji filamu amedai kushangazwa kuwa mpaka hivi sasa hajapata majibu yeyote kutoka kwa kikundi hicho kinachowashikilia wasichana zaidi ya 200 wa shule ya wasichana ya Chibok ambao walitekwa mnamo tarehe 14 mwezi May mwaka huu.

Adokiye amedai kuwa amewapa ofa hiyo bila kipingamizi na kudai kuwa kama wasichana hao ambao mpaka hivi sasa huenda wanapitia majanga mengi yakiwemo kutumikishwa kama watumwa wa ngono, basi ni bora waachiwe huru na wamchukue yeye.