Kumekuwa na taarifa na picha zinazoeleza kuwa hotel ya kifahari ya Sanawari iliyoko karibu na mataa ya Sanawari jijini Arusha inateketea kwa moto.
Hata hivyo, kamanda wa polisi wa mkoa Arusha, Liberatus Sabas ameiambia 100.5 Times Fm kuwa habari hizo sio za kweli kwani hata yeye yuko karibu na eneo hilo kiasi cha kuweza kuiona hotel hiyo kwa mbali.
“Mimi siko kwenye hotel ya Sanawari lakini niko karibu na hotel hiyo na kama kungekuwa na moto nigeona.” Amesema Kamanda Sabas.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichoko jijini Arusha, kikosi cha zima moto kimefika katika hotel hiyo na kukuta mambo yako shwari na hakuna dalili zozote za moto katika jengo hilo.
Credit Times FM
Friday, July 18, 2014
Baada ya kusambaa picha zinazoonesha hotel ya Sanawari ikiungua moto, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha akanusha
Labels:
News