Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

‹
›

Shooting

Racing

News

Bottom

Showing posts with label Gospel. Show all posts
Showing posts with label Gospel. Show all posts

Monday, July 21, 2014

Kajala Masanja ‘K’ ameibuka na kukanusha madai ya kutoka kimalovee na mtangazaji wa Clouds aitwaye Perfect

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ ameibuka na kukanusha vikali madai ya kutoka kimalovee na mtangazaji wa Clouds aitwaye Perfect.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita jijini Dar, Kajala alifunguka kwamba madai hayo hayana ukweli wowote na wala hana ukaribu na mtangazaji huyo.

Mtangazaji wa Clouds aitwaye Perfect.
 
“Sina relation (uhusiano) kama huo na Perfect zaidi ya kazi tu,” alisema Kajala huku Perfect akiwa hapatikani hewani kila alipotafutwa.

Saturday, July 19, 2014

Mtunisi Awachana “LIVE” Diamond na Wema Sepetu

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Nice Mohamed aka Mtunisi amewapa makavu live mastaa wenzie , Diamond pamoja na hawara yake Wema Sepetu aka Mama Ubaya ,kwa kitendo alichokifanya staa huyo wa filamu (Wema) kufutarisha nyumbani kwake na kumkaribisha harawa yake (Diamond) pamoja na mama mkwe wake (haijulikani mkwewe kwa nani na kwa ndoa ipi) Bi Sanura kitendo ambacho mtunisi amekiona ni kinyume na dini yao hiyo ya Kiislamu

Credit Taarifa News.

Thursday, July 17, 2014

Mtangazaji wa Redio EFM,Penniel Mungilwa 'Penny' afafanuwa sababu za kufunga Ramadhani

Penny Wenny
Mtangazaji wa Redio  EFM aliyewahi kuanguka kimahaba na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amewafungukia wanaomshangaa kuhusu kufunga mwezi wa Ramadhani na kuwataka watu hao wasimshangae kuhusiana na jambo hilo.

Akifafanua ishu hiyo mbele ya mwandishi wetu, staa huyo alisema kuwa amezaliwa katika familia yenye dini mbili japokuwa yeye ni Mkristo, lakini hufunga Ramadhani na Kwaresma sambamba na kusheherekea sikukuu zote kwa kuwa familia yao huamini Mungu ni mmoja.

Friday, July 11, 2014

Pombe yatibua futari kwa Diamond, Maustadhi washangaa na shampeni ya Wema yazua gumzo

NIkama jina la wimbo wake mpya wa Mdogo Mdogo ambao ndani yake kuna kikorombwezo ‘mwendawazimu kaingiaje’, ndiyo hali iliyotokea kwenye futari ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipofuturisha nyumbani kwake ambapo pombe zilitibua shughuli nzima.

Pamoja na kufuturisha, pia Diamond alimwandalia pati mama yake mzazi, Sanura Kassim a.k.a Sandra aliyekuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa. 

WAALIKWA WATAZAMANA 

Katika tukio hilo lililojiri nyumbani kwa staa huyo maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar mapema wiki hii, wageni waalikwa walijikuta wakitazamana na kuhoji uhalali wa chupa za pombe kuwepo ndani katika sehemu ambayo walitakiwa kufanyia dua. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya wanahabari wetu, baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo maustadhi walioshangazwa na jambo hilo, walihoji kuwa kulikuwa na ulazima gani au kilishindikana nini wahusika kuziondoa pombe hizo halafu wazirudishe baadaye.

“Unajua huu ni mwezi wa imani zaidi, sasa linapotokea suala la ibada kama hili la kufuturisha basi kuna vitu vingine unatakiwa uvifiche ikiwezekana uachane navyo kabisa. “Sioni sababu ya zile pombe kuachwa pale sebuleni kila aliyeingia ndani kula keki anakutana nazo uso kwa uso,” alisikika akilalama mmoja wa waumini wa Dini ya Kiislamu walioalikwa. 

POMBE ZAONDOLEWA 

Hata hivyo, pombe hizo kali ziliondolewa mahali hapo mara moja kisha shughuli ikaendelea. 

SHAMPEINI YA WEMA YATILIWA SHAKA 

Katika kuendelea kuweka walakini, muumini mwingine alikwenda mbali zaidi na kuitilia shaka shampeini iliyofunguliwa kuwa ni nani aliichunguza kama ilikuwa na kilevi au la!.

“Wakati shampeini inaletwa niliona, aliileta kijana mmoja namjua kwa jina la James ambaye ndiye aliyempatia Babu Tale (meneja wa Diamond), naye akampatia Wema Sepetu (laazizi wa Diamond). 
“Sidhani kama walikuwa na muda wa kusoma kama ina kilevi au la ndiyo maana baada ya Wema kuifungua watu waliikataa wakidhani ina kilevi hivyo ikamdodea mrembo huyo kwani ilidaiwa kama ilikuwa na kilevi ni jambo baya kwa mwezi mtukufu. 

WAINYWA WATATU 

“Walioinywa ni watatu tu, Wema, mama Diamond na dada yake Diamond, Esma Platnumz,” alisema mmoja wa waumini hao akitoa hoja juu ya kuitilia shaka shampeini hiyo ambayo waandishi wetu hawakupata nafasi ya kusoma maelezo yake.

MSIKIE BABU TALE 

Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa lilijaribu kuhoji kwa wahusika ambapo Meneja wa Diamond, Babu Tale alisema kuwa licha ya kutokaguliwa kwa Shampeini lakini haikuwa na kilevi.
“Shampeini haikuwa na kilevi, lakini kuhusu suala la chupa za pombe pale sebuleni, ule ulikuwa ni urembo tu ambao upo siku zote. 
“Hata mama Diamond akitaka kuswali huwa anasogeza meza na kufanya ibada yake ya swala, zile chupa zinakuwa zipo palepale ila kwa Wabongo siku zote wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu tamaa tu.“Zile chupa huwa zipo kila siku zimekaa tu kama nilivyosema kuwa ni urembo,” alisema Babu Tale.

DIAMOND HAKUWEPO 

Katika shughuli hiyo, pamoja na kwamba alikuwa nchini Marekani, Diamond alimzawadia mama yake gari aina ya Toyota Lexus Harrier lililogharimu Sh. milioni 38.1 alilokabidhiwa na Babu Tale.

Sunday, July 6, 2014

Tazama video hapa kuhusu Dini ya Kanye West 'Yeezianity' na jinsi ya kujiunga

Rapper Kanye West ni miongoni mwa wasanii wanaopenda kujifunza na kugundua au kubuni mambo mapya kila siku ili kuonekana tofauti, kama unakumbuka mwaka jana alitangaza mpango wake wa kuanzisha dini yake na mpaka kupelekea kuipa album yake Jina Yeezus ambalo ni mchanganyiko wa Ye na Jesus.

Dini ya rapper na producer huyu itaitwa Yeezianity na wanaotaka kujiunga nayo wameshapewa nafasi ya kutembelea mtandao wa waumini wa dini hii ambao ni Yeezianity.com Na waumini hawa watakuwa wanatumia na kuva sanamu linalofanana na sura ya Kanye West ambaye ndio mwanzilishi wa dini hii.

Ukitaka kujiunga Unatakiwa kupiga picha umeshika karatasi iliyoandikwa ‘I Beleive In Yeezus’ ikionyesha sura yako na ui share kwenye account yako ya kijamii.

Tazama video ikitoa maelezo zaidi.

Saturday, July 5, 2014

Katy Perry ashtakiwa na marapa wa nyimbo za Injili kwa uizi wa mistari

Nyota wa muziki kutoka nchini Marekani Katy Perry ameshtakiwa na marapa nyota wa nyimbo za Injili akiwemo mwanamuziki Flame ambaye amedai kuwa nyimbo ya Dark Horse ya Katy imeiba baadhi ya mistari kutoka kwenye nyimbo yao ya Joyful Noise. 
Wanamtuhumu Katy Perry kwa kutumia nyimbo yao iliyotoka mwaka 2008 waliyomshirikisha Lecrae bila ruhusa na kuharibu ujumbe wa kidini uliopo ndani ya nyimbo hiyo na kutumia picha za “kichawi” na nguvu za kidunia.

Nyimbo ya Dark Horse iliongoza katika chati za muziki za Billboard kwa wiki kadhaa mwezi January. 

Kundi la marapa wa nyimbo za injili Flame aka Marcus Gray, Lecrae Moore, Emanuel Lambert na Chike Ojukwu wanataka kulipwa fidia na mwanamuziki huyo,, studio yake ya Capitol, na waandishi wa nyimbo Dr Luke na Max Martin kwa kuiba hakimiliki za wimbo wao.

Isome hapa barua ya Emmanuel Mbasha akielezea mchungaji Gwajima alivyotembea na mkewe na njama ya kumfunga

Emmanuel Mbasha ambaye ni mume wa mwimbaji wa injili maarufu, Flora Mbasha ameandika barua ndefu iliyobeba mengi yanayohusu sakata lilizua uhasama kati yake na Mchungaji Gwajima kuhusu mkewe. 

Mbasha amabaye hivi sasa anatuhumiwa kwa kesi ya ubakaji amedai kuwa hata kesi yake ni sehemu ya njama za mchungaji huyo juu ya mkewe. 

Hata hivyo, Mbasha amemtumia ujumbe mkewe na kueleza imani yake kuwa ipo siku watarudiana. 

Isome hapa:

“Mchungaji…yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’… wa ghafla wa mke wangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!

Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!! Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine??

Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama??

Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda.

Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!!

Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe.

Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu?? Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!!

Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!! Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!

Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!! Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!! Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti! Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda…”Kwako- Mchungaji Gwajima.”

Kuhusiana na Sheikh ajeruhiwa kwa bomu Arusha

Sheikh wa Msikiti wa Qiblatan,Sood Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini hapa amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku nyumbani usiku wa kuamkia jana. 

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.
Pamoja na Sheikh Sood, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu. Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote. 

Akizungumza hospitalini hapo, Sheikh, Sood alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la Majengo ya chini, usiku wa kuamkia jana saa 5:00 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni.

“Nikiwa sijui hili wala lile nilishtushwa na mlipuko ulioambatana na vyuma mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumba tulichokuwamo,” alisema Sheikh Sood. 

Alidai anawajua waliotekeleza shambulio hilo kwa sababu amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu anaowafahamu na tayari alikuwa ametoa taarifa kwa vyombo vya dola. 

Alisema kuwa siku tatu kabla ya tukio hilo alikoswakoswa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na akatoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha kuhusu tukio hilo. Sood anasema kuna baadhi ya vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.

Sheikh huyo ambaye ni Kiongozi wa dhehebu la Answar sun Kanda ya Kaskazini amekuwa akitofautiana na waumini wenzake kutokana na msimamo wake wa kutokukubaliana na baadhi ya waumini wenye msimamo mkali wa msikiti huo. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alikemea matukio ya mabomu yanayolitikisa Jiji la Arusha katika siku za karibuni na kuviagiza vyombo dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wote ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. 

“Uchunguzi wa awali unaonyesha tukio hili limetekelezwa na watu walio karibu na Sheikh. Polisi wanaendelea na uchunguzi kwa sababu baadhi ya watu wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili pia ni miongoni mwa watuhumiwa kwenye matukio mengine ya milipuko ya bomu Arusha,” alisema Mulongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabasi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea vyema huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika. 

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alielezea kusikitishwa na matukio ya milipuko ya mabomu Arusha na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwakamata wahahalifu “Arusha tunapita katika kipindi kigumu sana. Kwanza tulishuhudia mlipuko wa bomu kanisani, ikafuatiwa na lile la mkutano wa hadhara wa Chadema, kabla ya mwingine kulipuka kwenye baa na sasa nyumbani kwa Sheikh,” alisema Lema.usika bila kujali vyeo, nyadhifa, dini, itikadi wala rangi zao. 

Chanzo: Mwananchi.

Friday, July 4, 2014

Picha za kudhalilisha: Wema, mama yake kusoma Albadiri!

SIKU chache zimekatika tangu kusambazwa kwa picha feki inayodaiwa ni ya mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu, wawili hao wako kwenye mkakati mzito wa kuwasomea kisomo cha Albadili wale wote waliohusika kwa namna yoyote ile kuitengeneza picha hiyo na kuitupia mitandaoni.

Picha hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na kichwa cha mama Wema, lakini sehemu ya kuanzia shingoni kwenda chini si yeye na mhusika alikuwa hana nguo, ilizua gumzo kwa wiki mbili sasa huku watu wanaojiita Timu Dengue wakitajwa kuhusika. 

Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.

KINYWANI MWA CHANZO CHA HABARI 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Wema na mwanaye wameamua kusoma Albadili ili kuwaadabisha wale wote waliohusika na sakata hilo lenye kufedhehesha. “Mama Wema na mwanaye walikasirishwa sana na watu waliotengeneza ile picha na kuitupia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram. 

“Wiki iliyopita baadhi ya wasamaria wema walikwenda nyumbani kwa mama Wema na kumtajia majina ya wahusika, lakini hawakuwa na ushahidi hivyo yeye na Wema wameamua kujiunga kiimani zaidi kwa kusoma Albadili''.

“Wamesema kwanza kabla ya tukio hilo la Abdadili wametoa siku saba kwa yeyote anayejijua amehusika na picha zile za kutengeneza aende mwenyewe kwa mama Wema, nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar) ili kuomba msamaha.''

“Kama zitapita siku saba na hakuna atakayejitokeza, Albadili itasomwa na mmoja baada ya mwingine watakufa. Tayari wameshawasiliana na mashehe ambao watasoma Albadili hiyo,” kilisema chanzo hicho.''

WEMA AYEYUKA HEWANI 

Baada ya kusikia kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika, juzi Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo lakini muda mwingi wa maandalizi ya habari hii, simu yake haikuwa hewani! 

MAMA WEMA SASA 

Baada ya kumkosa Wema, Risasi Jumamosi lilimtafuta mama yake, naye kwa njia ya simu na alipopatikana aliombwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo. 

KUHUSU ALBADILI

Akizungumza kwa hasira huku sauti yake ikionesha dalili kwamba bado hayuko sawa, mama Wema alisema:

“Ni kweli, nimeshapanga kufanya hivyo, nitasoma Albadili. Haiwezekani watu wakae na kuamua kunichafua mimi, nimewakosea nini cha mno mpaka kufikia kufanya vile! Siwezi kukubali hata kidogo.”

KUHUSU MASHEHE 

“Ni kweli pia, nimeshawasiliana na mashehe. Wao wako tayari wanachosubiri ni kupita kwa siku ambazo nimetoa. Kama hakuna atakayejitokeza kuomba radhi, kisomo cha Albadili kitasomwa, wataanza kupukutika mmoja baada ya mwingine kweli nasema.”  SIKU SABA

ZINAANZA LINI? 

“Jumamosi ijayo (leo) itakuwa siku ya kwanza. Kwa hiyo mpaka Ijumaa ya Julai 11 (mwaka huu), itakuwa siku ya mwisho.” 

NENO LAKE KWA WAHUSIKA 

“Nawaambia wale wote wanaojijua walihusika na ile picha ya uongo, ya kutumbukiza kichwa changu kwenye picha nyingine na wale waliohusika kuitupia kwenye mitandao, waje waniombe radhi kabla siku saba hazijaisha, sitanii jamani.”

UKWELI WAKE 

“Mimi ni Muislamu safi, nasema sijawahi kupiga picha za namna hiyo katika maisha yangu tangu nizaliwe mpaka utu uzima wangu huu na wala sijawahi kufikiria.” 

KUMBUKUMBU YA WEMA 

Katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Toleo la Juni 25, mwaka huu, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; Wema azimia! Habari ile ilimhusu Wema kupoteza fahamu kufuatia kuiona picha hiyo kwenye mitandao akidai ililenga kumchafulia mama yake jina. 

KILIO KWA TCRA 

Kumekuwa na wimbi la watu  kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu, pia wanafunzi wa vyuo wamekuwa waathirika wakubwa. 

Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliowahi kuzungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walitoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa picha chafu mitandaoni.

Credit GPL.

Thursday, July 3, 2014

Rose Muhando kuwashirikisha waimbaji toka Afrika Mashariki katika uzinduzi wa albamu yake ya 'Kamata Pindo la Yesu'

Mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini Tanzania Rose Muhando anatarajia kuwashirikisha waimbaji nyota wa miondoko hiyo Afrika Mashariki katika uzinduzi wa albamu yake aliyoibatiza jina 'Kamata Pindo la Yesu'.
Mwimbaji wa muziki wa injili Tanzania Rose Muhando
Gwiji huyo yupo katika mpango wa kuizindua albamu hiyo tarehe 3 mwezi Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo amegusia kuwa bado hajaweka hadharani orodha nzima ya waimbaji ambao watamsindikiza stejini japo kuwa ana mpango wa kumwalika mwanadada Anastazia Mukabwa kutoka nchini Kenya aliyeshirki katika wimbo wake Rose uitwao 'Kiatu Kivue'.

Rose Muhando ameelezea kuwa albamu yake hiyo mpya imesheheni nyimbo zikiwemo Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Kamata Pindo la Yesu, Facebook na nyinginezo nyingi.

Baada ya kushambuliwa kwa picha akiwa kama anasagana, Amber Rose atupia tena hizi

Hivi karibuni kupitia account yake ya Instagram, Amber Rose ambaye ni mama wa mtoto mmoja na mke wa mwimbaji wa HipHop nchini Marekani 'Wiz Khalifa' alishambuliwa kwa kutupia picha ikimuonyesha akipigwa 'kiss' mdomoni na msichana mwenzake 'Amber Rose, mke wa Wiz Khalifa ashambulia kwapicha inayo muonyesha akiwa kwenye kitendo cha usaganaji' kitu ambacho kilionekana kama usaganaji.
Lakini hizi ndizo picha mpya alizo tupia.


Picha ya Diamond akiwa na mbwa yazua kasheshe, Je ni kweli Dini hairuhusu?

Diamond Platinumz ambaye jina lake halisi la dini ya kiislamu ni Naseeb Abdul ameshambuliwa Instagram na baadhi ya mashabiki baada ya kupost picha akiwa beach huko ughaibuni huku ameshikilia kamba iliyomfunga mbwa. 

Mashabiki wengi walimshambulia wakielekeza point yake kwenye suala la imani ya dini ya kiislamu huku wakiunganisha tukio hilo na mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Rashyalhambeshy: ramadhan acha kupost pc zisizo eleweka ww umaaruf ww una umaaruf km mtume muhammad s.w.a na yote kakataza acha mambo yk ayo jua kuna kufa muangalie firauna laanatullah ila me lng jicho. na ktk dini tumeambiwa tukumbushaneni me nimekemea kwa mdomo ok. 

Hata hivyo sio wote waliomshambulia, wapo wengi pia waliomtetea kwa points tofauti kama Leanlilie aliyetumia point hiyo hiyo ya imani. 

leanlilie :I jus keep wondering who a u to judge another person?kumhukumu mwenzio tuu ni dhambi wew je ni mwema sana?huu ni wakati wa toba jisalie na uombee makosa yako,mwachie Allah ndio mtoa hukumu we Tanzanians tumezidi jaman khaaaaa!!can we atleast think abt our sins and pray acheni watu ma maisha yao.!  

Nimejaribu kuwauliza watu wawili watatu ambao wamejikita katika masuala ya dini ya kiislamu kuhusu picha hiyo na imani ya dini hiyo, lakini wao wamenieleza kuwa sio kosa kumgusa mbwa bali ni haramu ‘mbwa kumnusa muumini wa dini ya kiislamu’. 

Tafakari pia, mambo ya imani yanahitaji zaidi ya upeo wa kawaida.