Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Showing posts with label Health. Show all posts
Showing posts with label Health. Show all posts

Sunday, August 3, 2014

Fahamu kuhusiana na Magonjwa ya uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke

Kwa wanawake tatizo lao kubwa ni ‘Fibroid’ ambao ni uvimbe katika sehemu za uzazi (uterus) ambapo hutengenezwa na kambakamba zilizofungamana yaani muscle fibre. Fibroid huanza kwa ukubwa kama punje ya njugu mawe lakini huweza kukua na kuwa kama boga. 

Fibroid hupatikana zaidi kwa wanawake wa umri kati ya miaka 30 na 40 na hupungua ukubwa mara tu wanapoingia katika umri wa utu uzima, ingawa sababu au chanzo hasa cha fibroid hakijulikani, utafiti unaonyesha kuwa huchochewa na ‘oestrogen’ mwilini. 

Mara nyingi fibroid hukua kwa mwanamke pale kiwango cha ‘oestrogen’ kinapoongezeka mwilini na pia fibroid hupungua wakati kiwango cha ‘oestrogen’ nacho kikipungua.

Oestrogen ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia. Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi. 

Pia wanawake wenye uzito wa zaidi ya kilo 70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata tatizo hili kutokana na kiwango kikubwa cha oestrogen katika umri huo.Zamani fibroid ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa sababu vidonge hivyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha oestrogen. Hivi sasa vidonge hivi havina kiwango kikubwa cha oestrogen kama ilivyokuwa zamani. 

Fibroid zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Zipo zinazotokea ndani ya mji wa mimba na nyingine zinatokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba. Karibu asilimia 75 ya wanawake wenye fibroid hawajui kama wana tatizo hilo. Utambuzi wa dalili za fibroid hutegemea ukubwa wake na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mtu.Fibroid ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na fibroid kubwa inayoota nje ya kizazi.

DALILI 

Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na  maumivu ya tumbo.
Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa, na mgonjwa kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo, kutopata mimba na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa. 

Fibroid zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na fibroid, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus). 

Mwanamke anapokuwa mjamzito pia akawa na fibroid, mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye fibroid na kuifanya isinyae hivyo kusababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake. 

Wakati wa kujifungua, kama fibroid itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

USHAURI  

Dalili zikiwepo na kuhisi unalo tatizo la fibroid, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo kujua kama unao ugonjwa au la. Daktari atafanya vipimo vya ‘Ultrasound’ (mionzi) au kitatumika kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke kitaalamu huitwa hysteroscopy au kufanyiwa upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke kitaalamu huitwa Laparosopy.

TIBA   

Kuna njia kuu mbili za kutibu fibroid. Moja ni kwa kutumia dawa. Mkusanyiko wa dawa zijulikanazo kama ‘GnRH analogues’ hupunguza kiwango cha oestrogen mwilini na hivyo kusababisha fibroid kusinyaa.
Dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa fibroid pia hupunguza mzunguko wa hedhi.

Matumizi ya dawa za ‘GnRH analogues’ yasizidi miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa baadaye.
Mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi,wanawake wengine baada ya wiki chache hujikuta wakirudiwa na tatizo hili ambalo huanza kukua tena na mwanamke huanza kupata hedhi kama awali lakini ikiambatana na maumivu makali.
Baadhi ya wanawake huwa hawapati hedhi tena kwa maisha yao yote. 

Upasuaji ni njia nyingine ya kutibu ugobnjwa huu na huhusisha mambo yafuatayo: Kuiondoa fibroid yenyewe na kuacha kizazi jambo ambalo kitaalamu huitwa myomectomy; kukiondoa kizazi kabisa kitaalamu huitwa hysterectomy na kuzuia damu kwenda kwenye fibroids  yaani uterine artery embolisation. 

Pia iko njia ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni kwa ajili ya kuziua kwa kemikali maalumu.

Credit GPL.

Saturday, August 2, 2014

AFYA YA UZAZI: Tatizo la kutopata ujauzito

Mtu anaposema tatizo la kutopata ujauzito, ana maana mume na mke walio katika uhusiano wa kutafuta mtoto ndani ya mwaka mmoja, lakini wameshindwa. 
Inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani wa kiwango cha chini ni mwaka mmoja. 

Ni tatizo kubwa katika jamii kwani kila mmoja anataka afikie malengo ya kuwa na familia. 
Mwanamke na mwanamume wote wanahusika katika tatizo hili japo mara nyingi huonekana ni la mwanamke. Kutoshika mimba kwa muda mrefu ni ugumba ua infertility kwa kitaalamu. Mwanamke au mwanaume anaweza kuwa mgumba.

Ugumba umegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni ‘primary infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kuwa na mimba wala mwanaume hana historia ya kumpa mwanamke mimba. 

Ugumba wa aina ya pili ni ‘secondary infertility’ ambapo mwanamke anayo historia ya kuwahi kupata ujauzito, haijalishi kama alizaaa au mimba ilitoka na mwanamume anayo historia ya kumpa mwanamke mimba na pia haijalishi kama mtoto alizaliwa au mimba ilitoka. 

Tatizo la mwanamume kutoweza kumpa mwanamke mimba linaweza kusababishwa na kukosa nguvu za kiume hivyo kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Hali hii ya kukosa nguvu inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali kwani yenyewe si ugonjwa.  Kwa hiyo kitu cha msingi siyo kuongeza nguvu bali ni kufanya uchunguzi kuona tatizo ni nini na kulipatia ufumbuzi. 
Tatizo lingine kwa mwanamume ni kutotoa mbegu za kiume za kutosha ua kutoa mbegu zisizo na ubora. 

Hii ni baada ya kupima kipimo cha mbegu za kiume. Mbegu zinaweza zisizalishwe ua zikazalishwa pasipo na ubora unaostahili kurutubisha yai la mwanamke. 

Matatizo mbalimbali yanaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume kama uvutaji wa sigara,  unywaji wa pombe kali, maumivu ya korodani na utumiaji wa dawa za kulevya kama mirungi na bangi.

Mazingira ya joto katika korodani pia huathiri uzalishaji wa mbegu. Kutofahamu mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kipindi gani mwanaume anaweza kumpa mimba ni changamoto nyingine kwa upande wa mwanaume. 

Itaendelea wiki ijayo...

Credit Mwanancvhi.

Friday, August 1, 2014

AFYA YA NGOZI: Maradhi ya ngozi kwa njia ya ngono

Baadhi ya maswali tuliyopokea, mengi yalihusu maradhi ya sunzua ambayo kitaalmu yanajulikana kama warts.  
Sunzua ni ugonjwa wa ngozi unaofahamika na wengi. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo kitaalamu huitwa human papilloma virus. 

Karibu asilimia 10 ya wanadamu wamewahi kupata athari za virusi vya ugonjwa huu, achilia mbali kuumwa sunzua. 
Kwa sababu hiyo ndiyo kusema kila mtu anapaswa kufahamu ugonjwa huu kwa undani ili unapojitokeza awahi hospitali ili kuudhibiti.

Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya ngono. 
Ugonjwa huu hutokea sehemu mbalimbali za mwili, lakini huwatokea wengi sehemu za siri. 
Sunzua kama ugonjwa wa zinaa, huathiri sehemu za siri pamoja na njia ya haja kubwa. 

Wagonjwa ambao wanaishi na Virusi vya Ukimwi wako kwenye mazingira hatarishi zaidi ya kupata sunzua.   
Virusi vinavyosababisha maradhi ya sunzua huambukizwa kwa njia ya ngono na ni mara chache huweza kusambaa kwa njia ya kugusana.

Virusi wa maradhi haya wanajulikana kama papilloma na hujitokeza kwenye eneo la ngozi ambapo virusi hivi vimepenya. Mara nyingi hujipachika kwenye mchubuko au mpasuko wa ngozi. 
Maradhi haya huweza kujitokeza kwenye ngozi kati ya miezi miwili hadi tisa baada ya kupenya kwenye ngozi. 
Maradhi haya husababisha ngozi kutokuwa na muonekano wake wa kawaida.

Husababisha ngozi kuwa na milima na mabonde kiasi cha kusababisha kukatika kwa urahisi na kufanya virusi kuendelea kupenya. 
Dalili za maradhi haya ni kuwa na ngozi iliyoinuka, iliyopoteza unyoofu wake na yenye muonekano mfano wa maua. 

Sunzua ziko za aina tofauti kulingana na mahali ugonjwa unatokea na kuonekana kuiathiri ngozi. 
Sunzua ya sehemu za siri au kwa kitaalamu condyloma acuminatum (venereal warts).

Aina hii ya ugonjwa kwa wanawake huathiri sehemu za nje za maumbile ya siri na mara nyingine huweza kujitokeza na kuathiri shingo ya kizazi. 
Kwa wanaume sunzua huathiri uume wenyewe, korodani, nyonga mpaka kwenye mapaja. 

Sunzua hii ya sehemu za siri kwa watu wa jinsia zote hujitokeza kama uvimbe ulioinuka au zikawa sawia bila uvimbe wa aina yoyote. 
Sunzua zinaweza kuwa kubwa au ndogo, zikawa mojamoja au zikajikusanya pamoja kama mafungu zikafanana kabisa na maua.

Huwa zinaweza kutokea usoni, hasa sehemu karibu na kope ama maeneo mengine kama vile vidole vya miguu na mikono. 
Sunzua huwa haziumi na sanasana huwa zinawasha na huweza kujitokeza katika kipindi cha miezi miwili mpaka tisa baada ya maambukizi ya virusi. 

Kwa wanawake, sunzua ya kwenye shingo ya kizazi huweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi. 
Kwa sababu hiyo, mwanamke anapaswa kujichunguza ili kuchukua hatua mwafaka za matibabu.

Ndugu msomaji, kwa jumla magonjwa ya ngozi ni mengi na yanaathiri binadamu kwa namna tofauti. Kama nilivyoeleza hapo awali, yanayotokana na bakteria, fangasi, virusi na hitilafu nyingine katika damu au ngozi. 
Tutaendelea kujibu maswali mbalimbali ya wasomaji kulingana na mtakavyouliza. Kwa wale ambao maswali hayakujibiwa wasikate tamaa kwani kadri tutakavyopata nafasi, yataendelea kujibiwa.

Mawasiliano: isaac.I.Maro@gmail.com  

Credit Mwananchi.

Thursday, July 31, 2014

Ebola:Shule zote zafungwa Liberia

Rais wa Liberia,Ellen Johson Sirleaf ametangaza amri ya kufungwa kwa shule zote nchini humo kama mpango wa taifa hilo wa kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Ebola.  

Mpango huo pia unashirikisha kuzitenga baadhi ya jamii zilizokatika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Hatua hiyo inajiri huku maafisa wa afya wakidaiwa kuzongwa na kazi katika mji mkuu wa Monrovia ambapo vyumba vya kuwatenga waathiriwa wa ugonjwa huo vimejaa. 

Katika visa vingine wagonjwa wamelazimika kutibiwa nyumbani kutokana na ukosefu wa vituo vya kutoa matibabu.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Thomas Fessy anasema huu ni mpango huo ambao mamlaka inaamini utapunguza mtagusano baina ya jamii na hivyo basi kusitisha kuenea zaidi kwa Ugonjwa huo unaoua. 

Shule zote nchini humo zimefungwa ,na tayari wafanyikazi wa mashirika na Wizara za Serikali zisizo na umuhimu mkubwa wamepewa likizo ya siku 30. 
Baadhi ya jamii zimetengwa-na kupewa madawa na chakula. 

Serikali inajaribu kuzuia watu kutembea kutoka eneo moja hadi jingine ikiwa na imani kwamba watu walioathirika watajulikana na kutibiwa. 
Vikosi vya usalama vimeagizwa kutekeleza hatua hiyo.

Wakati huohuo baadhi ya raia wamepinga kubuniwa kwa eneo jipya la kuwatenga watu na kuwalazimu maafisa wa afya kuwatibu hadi wagonjwa 20 katika makaazi yao. 

Bado haijulikani ni vipi serikali itafanikiwa kutekeleza hatua hiyo wakati ambapo kuna hofu na shauku. 

Hadi kufikia sasa Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 672 katika matifa matatu ya Afrika Magharibi yaani Liberia Sierra Leone na Guinea huku mtu mmoja akifariki nchini Nigeria.

Shirika la Marekani linalotoa misaada ya huduma kwa jamii (Peace Corps) limewaondoa mara moja wahudumu wao katika mataifa yaliyoathirika pakubwa Liberia, Sierra Leone na Guinea baada ya mmoja wao kupatikana ameambukizwa. 

Kulingana na takwimu Ebola huua asilimia 90% ya watu walioambukizwa homa hiyo ambayo huchukua kuanzia siku 2-20 kujulikana iwapo mtu ameambukizwa. 

Hiyo ndiyo sababu asilimia kubwa ya wahudumu wa afya waliokuwa wakiwatibu wagonjwa walidhania kuwa ilikuwa ni Malaria na hivyo kuambukizwa homa hiyo kali. 

Ugonjwa huu ulitubuka nchini Guinea mwezi Februari. 

Homa hiyo ilienea kwa haraka hadi Liberia na sasa Sierra Leone.

Friday, July 25, 2014

Kaswende, mawazo, vyaweza kukusababishia uwe na kipara

Kipara ni kitu ambacho kinawapata watu wengi walioko sehemu mbalimbali duniani. Takwimu zinaonyesha kuwa takriban asilimia 50 ya wanaume kwa nyakati tofauti maishani mwao hujikuta wanapata kipara. 
Siyo wote wenye vipara mitaani vinatokana na uasilia. wengine ni kutokana na magonjwa na wengine ni mawazo

Kwa wanaume, mara chache kipara, kinaweza kuanza mapema kati ya umri wa miaka 14 na 20, lakini wanaume walio wengi hupata kati ya umri wa miaka 30 na 60. 

Wanaume wanaopata kipara huanza kuona nywele zikipungua kichwani hatua kwa hatua, kuanzia upande wa mbele au katikati ya kichwa na hatimaye sehemu hiyo huwa haina nywele kabisa.

Ingawa kimsingi kipara hufikiriwa kuwa ni tatizo la kawaida kwa wanaume, wanawake pia wanaweza kukabiliwa na tatizo hili.

Inasemekana kuwa karibu asilimia 40 ya wanawake nchini Marekani, kutokana na sababu mbalimbali wana tatizo la kipara au kunyonyoka nywele kichwani.  Kila unywele huota na kukua katika kifuko cha nywele kiitwacho kinyweleo kilichoko kwenye ngozi. 

Chini ya kila kinyweleo kuna kituta ambacho hushikilia unywele na kituta hiki hujulikana kama foliko ya nywele. 

Katika hali ya kawaida wastani wa nywele 50 hadi 100 huchomoka kila siku kutoka katika vifuko vyake katika ngozi ya kichwani na kuanguka chini.

Jambo hili linaweza kugunduliwa kwa urahisi kwa kuona nywele kwenye vitana, chanuo au foronya tunazotumia wakati wa kulala. 

Nywele zinapochomoka kwa wingi kuliko kawaida kila siku au zisipoota na kukua ili kuziba pengo la nywele zilizotoka, baada ya muda mtu huwa na kipara. Wakati mwingine nywele hupungua bila kutoka kichwani. 

Hali hii inaweza kusababishwa na kupungua kwa unene wa unywele au kutofautiana kwa kasi ya kukua kwa nywele. 
Ingawa chanzo hasa cha upara hakifahamiki vizuri, wanasayansi wanasema kuwa kukosekana kwa usawaziko sawia wa homoni ya kiume ya androjeni aina ya dihydrotestosterone (DHT) mwilini, ni moja ya vyanzo vya tatizo hili. 

Homoni hii inapoongezeka mwilini hasa katika ngozi ya kichwa, husababisha mgandamizo wa ngozi ya katikati ya kichwa na kuathiri foliko za nywele kwa kuzifanya ndogo kiasi kwamba zinapoteza taratibu uwezo wake wa kutokeza nywele mpya.

Hii ni kwa mujibu wa Dk Emin Tuncay Ustuner, daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha sura katika Jiji la Ankara nchini Uturuki. 

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa kutokea kwa kipara kuna uhusiano wa karibu na urithi wa vinasaba au viasili vya kijenetiki vinavyoathiri kuota na kukua kwa nywele katika kipindi fulani. 

Utafiti uliofanyika nchini Japan na kuongozwa na Profesa Yumiko Saga wa taasisi ya taifa ya vinasaba katika Jiji la Mishima, ulibaini kuwa viasili vya kijenetiki aina ya Sox21 vinahusika kwa namna moja ama nyingine na utokeaji wa kipara.

Utafiti mwingine, uliofanywa na timu ya watafiti waliokuwa chini ya uongozi wa Dk Krzysztof Kobielak, unahusisha viasili vya kijenetiki aina ya Wnt na BMP (Bone Morphogenetic Protein) na kutokea kwa kipara. 

Utafiti huo ulibaini kuwa protini aina ya Wnt inapopungua na BMP inapoongezeka, husababisha seli zinazozalisha foliko za nywele kushindwa kufanya kazi na nywele hushindwa kuota au kukua. 

Matokeo ya utafiti huo yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Stem Cells, la Septemba na Novemba 2013. 

Katika utafiti wao, Dk Lin-hui Su na Tony Hsiu-His Chen uliochapishwa katika jarida la Archives of Dermatology, toleo la 143 la Novemba 2007, walibaini kuwa sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku pia zinaweza kuathiri foliko za nywele na kuharibu usawaziko wa homoni za kiume mwilini.

Jambo ambalo huchangia kutokea kwa tatizo la nywele kushindwa kuota na kukuwa vizuri hasa kwa wanaume wenye homoni nyingi. 

Matatizo mengine ya kiafya yanayohusishwa na kutokea kwa kipara ni tatizo la muda mrefu la msongo mkali wa mawazo, ugonjwa wa kaswende, tiba ya mionzi, matumizi ya dawa za kutibu saratani na matumizi ya dawa zenye homoni. 
Matatizo mengine ni pamoja na lishe duni kwa muda mrefu, ugonjwa wa tezi la shingo pamoja na matumizi yaliyokithiri ya dawa za kulainisha nywele zenye kemikali kali. 

Ingawa kipara hakiwezi kusababisha mtu apoteze maisha, kinaweza kuwa na athari za kisaikolojia kwa watu wengi hasa vijana wanaopenda mitindo mbalimbali ya urembo wa nywele. 
Jambo hili katika nchi zilizoendelea huwafanya baadhi ya watu kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha kipara.

Hapa kwetu Tanzania, hospitali za rufaa zinao madaktari wa magonjwa ya ngozi wanaoweza kutoa msaada na ushauri kuhusu namna bora ya kukabiliana na tatizo la kunyonyoka kwa nywele au kipara. 

Ili kukabiliana na athari za kisaikolojia zitokanazo na kipara hasa pale inapokuwa vigumu kupata fursa ya kumwona daktari, mtu mwenye tatizo hili anaweza kuvaa wigi au kunyoa nywele zote mara kwa mara. 

Kwa ajili ya kukinga ngozi ya kichwa isiathirike kwa mionzi ya jua, mwenye kipara anaweza kuvaa kofia hasa wakati wa jua kali.

Hata hivyo, wapo watu wanaopenda kuwa na kipara kutokana na sababu mbalimbali lakini hushindwa kuwa na hicho cha asili. 
Ili kutekeleza kiu yao wao hunyoa upara kwa kumaliza nywele zote kichwani na hii imekuwa ikafanyika kwa vijana, wazee bila kujali jinsi. 

Mtaalamu wa magonjwa ya ngozi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Baraka Chaula anasema kuwa kwa hapa nchini hakuna utafiti juu ya kipara uliowahi kufanyika katika miaka ya nyuma. 
Labda iwe kwa miaka ya karibuni lakini katika miaka iliyopita, sijaona kumbukumbu yoyote ya utafiti wa kipara kufanyika,” anasema Dk Chaula. 

Pamoja na hali hiyo, anasema suala la kipara linaweza kuchukuliwa ni sehemu ya tatizo la ngozi kutokana na namna lilivyo, sehemu linapotokea pamoja na athari zake.

Wao kama wataalamu, anasema wanaamini tatizo la kipara linaweza kusuluhishwa iwapo chanzo chake kitagundulika mapema na hatua za kitiba kuchukuliwa. 
Anasema kipara kinachosababishwa na kaswende kinaweza kuzuilika iwapo tiba ya ugonjwa itafanyika kwa wakati. 

Kuhusu kuwakumba zaidi wanaume kuliko wanawake, Dk Chaula anasema kipara ni tatizo la homoni za kiume zaidi.“Hata wanawake hupata kipara lakini hili huwapata wanaume zaidi kwa sababu ni tatizo la homoni za kiume,” anasema Dk Chaula.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na,: 0787 032 458

Credit Mwananchi.

Tuesday, July 22, 2014

Je sabuni inaweza kurejesha ubikira? Haya ndiyo matokeao ya sabuni hiyo

Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia sabuni inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'.  Sabuni hizo zinadaiwa kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha wakati wa kushiriki tendo la ngono na mwanaume. 

Baadhi ya wasichana waliohojiwa na BBC mjini Nairobi wamekiri kutumia sababu hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na kurejesha hali ya ubikira. 

Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini Tanzania anasema kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine kwenye uke ni hatari. 

Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali kwani pia inaweza kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani.

Tiba ya Methadone kwa hisani ya Ray C yamuokoa Video Queen wa Ice Cream, Doreen

Ray C Foundation wameanza kuyaona matunda ya kazi yao ya kuwasaidia watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya baada ya kumtibu video Queen wa Ice Cream ya Noorah, Doreen kwa kutumia Methadone. 
Ray C amepost instagram  picha ya Doreen akionena kuwa na afya nzuri tofauti na awali walipomchukua, na kuandika ujumbe kuhusu hali ilivyo.
Doreen akiwa na Ray C kabla ya kupata matibabu ya Methadone

Video queen aliecheza kwenye video ya Noorah Ice cream Amerudi katika Hali yake ya kawaida baada ya kuanza Tiba ya Methadone......Nafurahi sana nikiona matunda ya Ray C Foundation..............Keep it up girl!!!Nafurahi kukuona ukiwa na afya njema!!!!!!!Say No to Drugs!

Thursday, July 17, 2014

Ukaribu wa Kope za bandia na uwezekano mkubwa wa kuusababisha upofu

Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia. 
Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa. 

Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume.
Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi. 

Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji. 
Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa ‘kuona’.

Endapo mtumiaji ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae. 
Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika.

Ukwepaji wa gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye hatari zaidi. 
Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.

Thursday, July 10, 2014

Wanasayansi wagundua mapya kuhusu Malaria

Kulingana na uchunguzi wa vimelea vinavyosababisha Malaria huweza kuishi kwenye  uboho (bone marrow) na kuepuka kinga za mwili na hivyo basi kusababisha maradhi. 

Uchunguzi huu umedhihirishwa na bwana Marti ambaye alizungumza na shirika la habari la Uingereza, BBC. 

Swala la vimelea hivyo kujificha kwenye uboho si jambo geni, lakini kundi la wanasayansi wakiongozwa na Profesa Matthias Marti katika idara ya Afya ya umma kule Harvard, Boston, walifichua hasa ambako vimelea hivyo hujificha na kutoa maonyesho. 

Uzinduzi huu una umuhimu mkubwa kwa misingi kuwa umeleta ujuzi unaohitajika sana na huweza kupelekea kuundwa kwa dawa na kinga mpya za kukabiliana na vimelea hivyo ili kuzuia maambukizi. 

Kwa mujibu wa wanasayansi huko Harvard, uchunguzi huu uliochapishwa na jarida la kisayansi la Science Translational Medicine, umeongeza ujuzi wa kibaiologia utakaotumika kuchunguza ugonjwa wa Malaria hata zaidi. 

Vimelea vinavyosababisha Malaria huambukizwa hasa kupitia mbu, na husababisha vifo zaidi ya nusu kila mwaka ulimwenguni. 

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la afya duniani, zinapendekeza kuwa Malaria ilisababisha vifo 600,000 mwaka wa 2012, na takriban asilimia 90 ya vifo hivyo vilitokea Afrika.

Saturday, July 5, 2014

Picha: Mwalimu msamaria aanzisha mahusiano na mapacha walioungana India

Mapacha hao walioungana wanasema wana furaha kukutana na mwalimu msamaria Jasimuddin Ahmad aliyetokea kuwapenda.
Baada ya kuishi maisha ya usiku wenye upweke barabarani na usafiri wao, mapacha walioungana Ganga na Jamuna Mondal hatimaye wamepata mpenzi. 

Wakiwa na umri wa miaka 45, na wakijulikana kama Spider Girls, wamekuwa peke yao maisha yao yote na kuumia baada ya kukataliwa kutokana na muonekano wao wa ajabu.
Mapacha hao wenye umri wa miaka 45, Ganga na Jamuna Mondal ambao pia wanaojulikana kama Spider Girls wamekuwa wapweke maisha yao yote kutokana na kukataliwa na watu ila kwa sasa wana furaha maishani.
Ila kwa sasa wana furaha kuzidi – baada ya kupata nafasi ya kukutana na mwalimu msamaria mwema, Jasimuddin Ahmad. 
Ulikuwa upendo wa kwanza kuuona”, alisema Ganga, ambaye anatumia pamoja na dada yake mikono yake minne na miguu mitatu. 

“Tulipokutana na Jasimuddin, wote tulihisi tumekutana na mtu ambaye angejaribu kutupenda sisi. Na ndivyo anavyofanya – anatupenda kutoka kwenye moyo wake.
Kama ilivyo kwa mahusiano mengine mazuri, mazaha na utani ni sehemu ya mapenzi.
Tumekuwa na furaha sana tangu awe nasi maishani, tumeumia sana kipindi kilichopita ila kwa sasa hatutoumia tena. Tunamatumini kuwa tutaishi naye pamoja mpaka kifo kitutenganishe”, aliongeza Jamuna.
Wakiwa na familia yao, mapacha hao ambao wanatumia tumbo moja ila kila mmoja ana moyo, figo na ini lake, wamezaliwa katika familia maskini ya huko Kolkata, Bengal Magharibi.

Fahamu hili, Tattoo husababisha maradhi ya ngozi, kuzaa watoto walemavu

Siku hizi hapa nchini ni jambo la kawaida kuona watu hasa vijana wakiwa wamejiremba miili yao kwa michoro, maarufu kama tattoo. 
Dawa zinazotumika kuchora tattoo nyingi zina sumu na mashine zinazotumika husambaza maambukizi ya magonjwa.
Michoro hii huwa inalenga sababu na maana mbalimbali, ingawa jambo hili kwa vijana huonekana kama kwenda na wakati. Wakati mwingine michoro hiyo huandamana na imani za kishirikina katika kutekeleza malengo fulani. 

Mara nyingi alama hizi zinaweza kuwa ni michoro ya maua, picha za watu au wanyama, ramani na hata wakati mwingine inaweza ikawa haieleweki.

Alama au michoro zisizoeleweka huchorwa maeneo ya wazi au yaliyojificha ambayo huonekana pale tu mtu akiwa amevua nguo. 

Alama kwenye maeneo ambayo huweza kufichwa ni kama vile misuli ya mikono, mabega, kifua, tumbo, mgongo, mapaja, makalio na maeneo yanayozunguka sehemu za siri. Maeneo ya wazi ni paji la uso, mikono, vidole, visigino au miguuni. 

Michoro hii huweza kuchorwa kwa ajili ya kipindi fulani tu au ya kudumu kulingana na malengo na kusudio la mhusika. 

Yale ya muda huweza kuchorwa kwa ajili ya tukio kama vile michezo, kuolewa ama sherehe mbalimbali ambazo huhusisha wanawake.

Kuna wanaotumia rangi zinazotokana na mimea ya kawaida na wengine hutumia dawa maalumu zinazouzwa madukani pamoja na vifaa vya kuchorea. 

Wanasayansi wa afya ya jamii wanaonya kuwa michoro iliyotokana na rangi za madukani pamoja na vichoreo vyake, inaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa wahusika. 

Baadhi ya rangi zinazotumika kuchora mapambo mwilini zinaweza kusababisha mzio wa ngozi katika eneo la mwili mahali palipo na tattoo. Mzio huu unaweza kutokea kipindi kirefu baada ya kuchora tattoo. 

Tafiti nyingi za kitabibu pia zinaonesha kwamba, wino au rangi za tattoo zinaweza kusababisha uambukizo wa bakteria aina ya mycobacterium cholonae
Bakteria hawa wanaweza kusababisha magonjwa ya ngozi na nyama za mwili, matatizo ya njia ya mkojo, tatizo kwenye mfumo wa kupumua, magonjwa ya uambukizo kwenye mifupa, uambukizo katika nyama za moyo, homa ya uti wa mgongo na tatizo la macho.

Vilevile vifaa vinavyotumiwa kuchora mapambo hayo hutumika kwa watu mbalimbali kwa wakati mmoja bila utaalamu sahihi wa kuvisafisha na hivyo kuweka uwezekano wa vimelea vya ugonjwa fulani kubebwa na kuhamishiwa kwa wengine. 

Hali hii inaweza kusababisha uambukizo wa magonjwa yatokanayo na virusi hatari kama vile virusi vya Ukimwi, virusi ninavyosababisha homa ya ini (hepatitis B na C) au virusi vya malengelenge (herpes simplex virus).

Kumbuka wakati wa kuchora tattoo, ngozi hutobolewa kwa mashine au sindano hadi kuifikia sehemu ya ndani kabisa.  Vifaa hivyo pia vinaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa kama vile pepopunda (tetanus), majipu na hata kaswende.

Kwa sababu hiyo, katika baadhi ya nchi zilizoendelea mtu anapochora mwili wake tattoo, haruhusiwi kumwongezea mtu mwingine damu yake hadi mwaka mmoja upite baada ya kuweka michoro hii.  Hii ni kutokana na hofu ya uambukizo wa maradhi anayoweza kupata wakati wa kuweka tattoo yasijekuambukiza mtu mwingine. 

Lakini pia mapambo haya yanaweza kusababisha manundu ya ngozi (keloids), kupata hisia ya kuungua mwili wakati wa uchunguzi wa kitabibu kwa kutumia mionzi (Magnetic Resonance Imaging,  MRI) na saratani mbalimbali.

Miongoni mwa saratani hizo ni pamoja na saratani za limfu na tishu (primary non-Hodgkin lymphoma na leiomyosarcoma).

Katika utafiti uliofanywa mwaka 2006 na Paradisi A, akishirikiana na timu ya watafiti wengine, ilithibitika kuwa tattoo pia zinaweza kusababisha saratani za ngozi. 

Dk Elizabeth Tanzi, daktari bingwa na mtafiti wa magonjwa ya ngozi, anasema kuwa matatizo ya kiafya yatokanayo na kuchora tattoo, siyo jambo geni. 

Dk Tanzi anaongeza kusema kuwa licha ya kusababisha uambukizo na mzio kwenye ngozi, wino wa tattoo pia unaweza kusababisha uvimbe wa ngozi wakati wa kufanya kazi kwenye jua kali. 

Tafiti mbalimbali za kisayansi zimeonyesha kuwa aina nyingi za wino unaotumika kuchorea tattoo, una madini ya sumu kama vile zebaki, nickel, lithium, cadmium sulfite, lead na benzo (a) pyrene. 

Sumu hizi zinajulikana kwa uwezo wake wa kusababisha saratani na kudhuru tishu za mfumo wa limfu (lymph nodes) katika mwili wa binadamu. 

Mnamo mwaka 2005, Fredrik Ljungderg, mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya Arsenal wakati huo, alipata madhara makubwa katika mfumo wa limfu kutokana na tattoo kiasi cha kupata mitoki na kufanyiwa upasuaji. 
Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyoandikwa na Sam Coates mwezi Mei, 2005 katika mtandao wa www.timesonline.co.uk.

Matatizo ya kisaikolojia pia yanaweza kutokea pale sababu au mtindo wa kuchora mapambo kwenye ngozi unapopitwa na wakati na akatamani kuondoa alama hiyo bila mafanikio. 

Akili ya vijana wengi inaendelea kukua na kupitia katika mabadiliko ya maamuzi kila mara na kutaka kwenda na wakati.  Mitindo ya mapambo mengi ya urembo hubadilika kulingana na mabadiliko ya kitamaduni katika jamii yoyote ile. 

Hina nyingi za madukani zinazotumika kuchora tattoo au mapambo ya ngozi ya muda mfupi na dawa za kubadili rangi ya nywele, pia zina sumu ya para-phenylediamine (PPD) ambayo inaweza kusababisha mzio wa ngozi au mzio katika njia ya hewa.

Mzio utokanao na hina hii unaweza kumfanya mtumiaji aathirike pale anapotumia dawa za hospitalini zenye kemikali aina ya sulfa na baadhi ya dawa za nusu kaputi zitumikazo wakati wa upasuaji hospitalini. 

Lakini pia baadhi ya kemikali katika wino wa tattoo zinapotumiwa wakati wa ujauzito, zinaweza kumsababishia mtoto ulemavu wa kuzaliwa nao. 

Wagonjwa wa kisukari na wale wenye upungufu wa kinga mwilini wanaojitambua, wajiepushe kuchora tattoo kwa sababu zinaweza kuwasababishia vidonda visivyopona kwa haraka. 

Clifford Majani ni mtaalamu kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Mbeya (NIMR-MMRC).  0784 688 409

Wednesday, July 2, 2014

Huyu naye Aliuza figo kwa kudanganywa kuwa ingeota nyingine

Kathmandu, Nepal: Katika mitaa ya Jiji la Kathmandu, nchini Nepal kukutana na watu wakiomba msaada wa matibabu ya figo ni jambo la kawaida. 

Duniani kote, tatizo la figo siyo jambo geni masikioni mwa watu. Wapo wengi wanaosubiri kubadilisha na wengine kupata matibabu ya kawaida. 
Maharamia wa biashara ya figo wanatumia umaskini na ukosefu wa elimu, kuwarubuni watu mbalimbali duniani kama ilivyomtokea mwanamume huyu. 
Inakadiriwa kuwa watu wapatao 300 katika kipindi cha miaka mitano, wameingia katika mtego wa wafanyabiashara wa figo na wamezitoa bila wao kujua.

Hata hivyo, kwa Nepal ni habari nyingine kabisa. Siyo kwamba watu hawa wanataka kubadilishwa figo kama wale wengine duniani ambao wana matatizo ya kawaida. Hawa hawana kwa sababu walirubuniwa na zikachukuliwa bila wao kujua.
Pariyar akionyesha jeraha ilipotolewa ‘nyama’ ambayo aliambiwa ingeota. Picha na mtandao

Hivi sasa wanaugua magonjwa mbalimbali kwa sababu hawana uwezo wa kugharimia matibabu ya figo (dialysis) kutokana na umaskini uliotopea. 

Inakadiriwa kuwa watu wapatao 300 katika kipindi cha miaka mitano, wameingia katika mtego wa wafanyabiashara wa figo na wamezitoa bila wao kujua.  Mwathirika wa biashara hiyo, Nawaraj Pariyar anasimulia jinsi alivyodanganywa kuwa nyama wanayoitoa tumboni mwake ingeota tena bila kujua kinachotolewa ni figo. 

Kama walivyo wakazi wengi nchini humo,  Pariyar naye alikuwa akiishi kwa kutegemea biashara ya maziwa kutoka katika ng’ombe wawili anaowamiliki.

Pariyar ni maskini ambaye hakwenda shule hata darasa moja, mbali na kumiliki ng’ombe hao. Analo shamba dogo ambalo halimtoshelezi kulima mazao yatakayompa chakula cha angalau kwa miezi sita. 

Katika kujiongezea kipato, alikuwa akienda mji mkuu wa nchi hiyo, Kathmandu kutafuta vibarua vya ujenzi.  Akiwa katika moja ya vibarua hivyo mwaka 2005, kiongozi wa ujenzi katika jengo alilokuwa akifanya kibarua alimfuata kumpa ‘mchongo’ ambao ungemfanya apate chapchap Dola 30,000 za Kimarekani 30,000. 

“Aliniambia kuna kipande cha nyama kitatolewa tumboni nami nitapewa kiasi hicho cha pesa. Nilipotaka kuhoji zaidi aliniambia nisiwe na wasiwasi kwani kipande hicho kitaota tena baada ya muda,” anasema  Pariyar. 

“Nilifikiria  kama nyama itaota tena kwa nini nisikubali tena ninapata pesa nyingi kiasi hicho.”

Anasema kabla ya kukubaliana naye alimuuliza itakuaje kama atakufa wakati wa kuitoa nyama hiyo, lakini alimhakikishia kuwa itatolewa na wataalamu waliobobea hivyo asiwe na wasiwasi. 

Anasema maisha yalibadilika kuanzia pale alipokubali kwani alipewa nguo nzuri na chakula. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake alipelekwa katika jumba la sinema. 

Wahalifu hao walimpeleka katika hospitali moja nchini India katika mji wa Chennai.

“Tulipofika hospitali daktari aliniuliza kama nina undugu na mgonjwa, nilikubali kwa kuwa ndivyo nilivyoambiwa niseme,” anasema Pariyar. 
“Nilisikia mara kadhaa wakisema kidney (figo) lakini sikuelewa kwa sababu katika lugha yetu huwa inaitwa mirgaula,” anaongeza. 

Anasema kama angejua kama kinachozungumziwa ni figo, asingekubali kuendelea na  zoezi hilo. 

Baada ya kutolewa figo, Pariyar aliondolewa na kurudishwa kwao huku akiambulia Rupee 20,000 tu ambazo hazifikii hata robo ya makubaliano yao. 

“Baada ya muda nilipata wasiwasi. Nikaamua kurudi kwa daktari kuulizia kwa sababu hata wale watu sikuwaona tena, ndipo nilipogundua kuwa figo yangu imechukuliwa,” anasema Pariyar.

Hivi sasa Pariyar anaugua mara kwa mara. Ana matatizo katika mkojo na mgongo unamuuma mara kwa mara. 

“Najua nitakufa hivi karibuni. Natumaini nikifa leo Serikali itanisaidia kuwatunza watoto wangu wawili. Sijui kama nitakufa leo au kesho lakini siku zangu zinahesabika,” anamalizia. 

Wito wake kwa serikali ya nchi hiyo ni kuwaelimisha wananchi wake ili wasirubuniwe kwa sababu ya umaskini wao na kukosa elimu. 

Kwa mwaka jana pekee, watu 10 walikamatwa katika majaribio ya kutaka kuwasafirisha watu ili wakawatoe figo na kuziuza.

Tuesday, July 1, 2014

Msanii Nazizi wa nchini Kenya aamua kuingia gym

Msanii Nazizi wa nchini Kenya ambaye ametalikiana kwa muda na mumewe, hivi sasa ameamua kuelekeza nguvu zake katika kufanya mazoezi kwa kuingia rasmi Gym.

Nazizi Hirji ambaye hivi sasa ni mama mlezi wa mtoto wake mmoja ameelezea kuwa ameamua kutumia muda wake mwingi kuujenga mwili wake na kupunguza uzito na sio kwamba anauchukia mwili wake huo. 

Aidha rapa huyo wa kike aliyepitia misukosuko mingi ya ndoa na mahusiano ya hapa na pale, amerejea kwa kasi na albamu yake mpya inayotarajia kumrudisha rapa huyo mkali kwenye gemu.

Vinywaji vyenye sukari nyingi vinachochea ugonjwa wa 'gout'

Gout, inasemekana uliwahi kuwa ugonjwa wa watu wa hadhi za juu kama wafalme. Lakini sasa unazidi kuenea kwa kasi kwa watu kama mimi na wewe, huku vinywaji vyenye sukari vikilaumiwa kwa ongezeko hilo, kwa mujibu wa watafiti. 

Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu tangu mwaka 1970 na ugonjwa huo wenye mauvimu makali ndiyo wenye kusumbua zaidi wanaume miongoni mwa magonjwa ya aina hiyo. 
Mtu mmoja kati ya 35 anasumbuliwa na gout, kwa mujibu wa utafiti kuhusu vyanzo na maambukizi ya gout.    

Gout inahusishwa na mkusanyiko wa tindikali ya uric katika damu, mabaki yatokanayo na mwili kumwaga uchafu kupitia figo. 
Vinywaji vinavyosababisha ni pamoja na baridi na vikali kama whisky. 
Inajitokeza wakati mwili unapomeng’enya kemikali  zijulikanazo kama purines.