Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

‹
›

Shooting

Racing

News

Bottom

Showing posts with label Fashion. Show all posts
Showing posts with label Fashion. Show all posts

Tuesday, September 23, 2014

Picha za mtindo wa vazi la usiku kwa wanawake

Baadhi wanawake siku hizi wamekuwa wakijiuliza vazi gan ambalo linafaa kuvaliwa wakati wa usiku na likawapendeza sasa unaweza kutazama picha hizi


Wednesday, August 6, 2014

Picha za wanamitindo kwenye basi zikionyesha mwanamke akionekana kama anayebakwa na wanaume, zazua utata

Picha za wanamitindo zilizopigwa kwenye basi zikionyesha mwanamke akionekana kama anayebakwa na wanaume, zimezua hisia kali kwenye mitandao ya kijamii nchini India
Watu wengi wamesema kuwa picha hizo zinaonekena kusifu kitendo cha ubakaji kilichomkuta mwanafunzi mmoja mjini Delhi kwenye basi mwaka 2012.

Mwanafunzi huyo ambaye aliga baadaye, alibakwa na genge la wanaume. 
Picha za mpiga picha Raj Shetye ambaye alipiga picha hizo, zinaonyesha mwanamke akioenekana kupigania maisha yake akiwa amezuiliwa na wanaume wawili kwenye kiti cha basi. 
Ni kitendo ambacho kinaleta hisia kali kwa watu wengi na kumbukumbu za unyama uliotendewa msichana wa shule kwenye basi hadi akafa.

Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanasema picha hizo ni za kukera na zinatisha . 
Bwana Shetye hata hivyo amejitetea akisema picha hizo ni za kuonyesha tu hali inayowakumba wanawawake wengi nchini huo wala sio kuonyesha ubakaji. 
Hata hivyo picha hizo ziliondolewa kwenye mtandao huo wa Behance baada ya hisia kali kutoka kwa watumiaji waTwitter na Facebook. 

Ubakaji wa msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 ulisababisha maandamano makubwa nchini humo na hata kulazimisha maafisa wakuu kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na ubakaji  BBC ilijaribu kumtafuta Bwana Shetye aweze kujieleza kuhusu picha hizo ingawa hatukufanikiwa badli vyombo vya habari vilimnukuu akisema hakua na nia ya kuleta kumbukumbu mbaya kuhusu kitendo cha ubakaji kilichozua hasira kote nchini India.

Sunday, August 3, 2014

Quick Rocka azungumzia nguo zake za ‘Switch Like Me’ zilizoingia sokoni hivi karibuni

Rapper Quick Rocka amezindua nguo za kampuni yake ‘Switch Clothing Line’ alizozipa jina la ‘Switch Like Me’. Akiongea na Kikwetu Blog, Quick amesema kwa kuanza ameanza na t-shirt za rangi mbalimbali ambazo tayari zipo sokoni. “Tumeanza na t-shirt lakini ndani ya mwezi nimeplan kufanya kitu kikubwa zaidi. Tunataka kufanya kwa quality kubwa, kwenda kuprintia China ambayo itakuwa ni t-shirt na kofia pia,” amesema Quick.
Pamoja na biashara ya t-shirt, Quick Rocka alifungua studio yake ya muziki iitwayo Switch Studio.

Perfume mpya ya Rihanna itakayofanya wanawake waondoke wa T Shirt za wapenzi wao

Baada ya kuongelea manukato yake kwa muda wa mwezi mmoja sasa Rihanna yupo tayari kuweka sokoni bidha hii mpya,Wale wa Rihanna Perfume hii mpya inaitwa Rogue Man na inatoka September.
Rihanna akiongelea perfume hii amesema “Inamanukato mazuri sana mpaka wanawake watakuwa wanaiba T Shirt za wanaume wao”

Tuesday, July 22, 2014

Picha: Agnes Masogange azidi kumake headline nyingine Instagrm kwa hizi picha

Video queen wa Bongo ambaye kwa sasa inasemekana amehamishia asilimia kubwa ya maisha yake Afrika Kusini 'Bondeni' Agnes Masogange ame share picha hizi nakusababisha ku make headline nyingine kwa umbo lake la uzuri alilo nalo.
Moja ya picha akiwa amendika haya maneno
''Nimejizuia weeee nimeshindwa kuvumilia nimeamua bora niweke tu😃😃 kwani nikipigia sehem moja nyie inawahusu nin lol jus joking I need photographer lol''
 

Monday, July 21, 2014

Picha na Videoa: Mdada ajirora mwilini mchoro ulio fanana na vazi na kupita mtaani bila kuwa na vazi

Unaweza ukasema mdada amevaa nguo ila si nguo bali amechorwa rangi kwenye mwili wake na kutembea mtaani bila watu kujua au unaweza ukasema amevaa pants.

Sarah Baboro and David Lesage, students of Public relations from a school in Belgium, were asked to make a video for their final examination which would create a lot of publicity and views. So in order to achieve desired grades in the examination duo recruited a French makeup artist who is also a friend of Sarah, named Marie P and their mutual model friend for the concept. The concept of the duo was to make a model walk on the local street of France with just a G String on her lower body and with a illusion of faded blue jeans with the help of body paint.

Tazama video:

Tazama picha zaidi:





Sunday, July 20, 2014

Picha: Mastaa wenye tattoo kali duniani

Staa wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham 39, ambaye kwasasa amejikita katika fani ya uwanamitindo ‘Modal’
Staa wa zamani wa timu ya ligi kuu ya Uingereza Liverpool  Djibril Cisse, mwenye tattoo 40 katika mwili wake.
Raul Meireles mchezaji wa zamani wa timu za Chelsea na Liverpool.
Daniel Agger beki wa timu ya taifa ya Denmark na klabu ya soka ya Liverpool, huku viganja vyake vikiwa na maandishi ya YNWA (You Will Never Work Alone).
 Stephen Ireland akionyesha tattoo yake aliojichora mabawa ya malaika.
 Kevin Prince Boateng, wa timu ya taifa ya Ghana pamoja na klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani.
 Daniel Alves wa Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Brazil.
 Nigel de jong wa uholanzi pamoja na klabu ya AC Milanya nchini Italia.
Clint Dempsey wa timu ya taifa ya Marekani.

Friday, July 18, 2014

Miriam Odemba akava jarida la New African Woman

Mrembo na mwanamitindo waa Tanzania, Miriam Odemba amekava jarida la New African Woman la Afrika Kusini. 
Jarida hilo linahusika na urembo, mitindo, afya, familia na mambo mengine na linalenga katika kuonesha utamaduni na urembo halisi wa mwanamke wa kiafrika.  

“Finally….and…drumroll…to our esteemed South African readers….heading your way soon…here is the August/September edition South African cover. Our African Rose Miriam Odember.” Wameandika. 
Naye Miriam Odemba amepost picha ya jarida hilo kwenye Instagram na kuwashukuru waandaaji wa jarida hilo kwa kumpa nafasi hiyo.

Thursday, July 17, 2014

Ukaribu wa Kope za bandia na uwezekano mkubwa wa kuusababisha upofu

Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia. 
Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa. 

Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume.
Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi. 

Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji. 
Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa ‘kuona’.

Endapo mtumiaji ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae. 
Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika.

Ukwepaji wa gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye hatari zaidi. 
Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.

Picha: Selena Gomez ajichora tattoo ya kiarabu yenye ujumbe wa mapenzi

Mwimbaji na muigizaji wa kike, Selena Gomez ameamua kutumia mwili wake kuweka ujumbe wa mapenzi kwa lugha ya kiarabu kwa kujichora tattoo mpya. 
Mrembo huyo ambaye ni mpenzi wa Justin Bieber amepost picha kwenye Instagram Jumatano, July 16 ikionesha tattoo iliyochorwa upande wa kulia juu kidogo ya mgongo ikiwa na ujumbe wa kiarabu uliotafsiriwa kuwa ni ‘Love Yourself’, yaani Jipende. 
Mchoraji wa tattoo hiyo pia alipost picha hiyona kuandika ‘Little gift for my friend @selenagomez”.

Wednesday, July 16, 2014

Japokuwa na muonekano wa mvuto, Kardashian akerwa na muonekano wake wa sasa

Picha ya Kim Kardashian
ya mwaka 2010, aliyoituma kwenye
ukurasa wake wa instagram kabla
Baby North hajazaliwa.
Inavyoonekana mwanadada mrembo Kim Kardashian 33, ameli ‘misi’ umbo lake la zamani kabla ya kumpata binti yake North West mwenye umri wa  miezi 13 mpaka sasa. 

Katika ukurasa wake wa Instagram Kim alituma picha ya mwaka 2010 ikimuonyesha umbo lake kipindi alivyokuwa mwembamba. 

Katika picha hiyo aliambatanisha maneno yafuatayo; ‘Throwback to a few years ago#skinnyDays’.

Hata hivyo staa huyo maarufu kama Mrs. West yupo katika diet pamoja na ratiba ya mazoezi ya mwili ili kuhakikisha anapunguza uzito alioupata baada ya kujifungua ili kurejea katika umbo lake la mwanzo lililokuwa likikosha nafsi za wengi.

Picha: Atumia zaidi ya Milioni 49 kufanya upasuaji afanane na Kim Kardashian

Kupenda ama kutamani kuwa kama star fulani unaemkubali hakuna sheria ya mipaka zaidi ya mwenyewe kuthibiti hisia zako zisipitilize, lakini wapo wengine ambao wamechoka kutamani kuwa kama fulani na wameamua kutumia nguvu kuwa kama yeye. 

Claire Leeson, msichana mwenye umri wa miaka 24, mkaazi wa Landani ametumia zaidi ya $30,000 (Tsh 49,755000)kufanya upasuaji ili afanane na Kim Kardashian. 

Claire ameiambia This Morning kuwa aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa shuleni wenzake walikuwa wanamcheka na kuuita ‘mbaya’ kuliko kitu chochote kilicho hai. 

“Nilikuwa naambiwa kila siku mimi ndiye mbaya kuliko kitu chochote kilicho hai na kwamba inabidi nijiue. Nilipoacha shule marafiki zangu waliniambia kuwa ninavitu ambavyo vinafanana na Kim Kardashian.” Amesema Claire. 

Ameeleza kuwa baada ya kuambiwa hivyo na marafiki zake aliamua kuanza kuangalia kwa makini Keeping Up With The Kardashians na akagundua kuwa kweli kuna vitu ambavyo wanafanana na Kim Kardashian. 
“Tunafanana katika mabishano na vitu vingine. Nikafikiri ni mzuri sana na kwa kweli nilitaka kufanana nae.”

Boob Job- $8500  
Teeth Whitening-$4300 
Hair Extensions-$7700 
Make-up-$1700 
Spray Tans-$1700 
Nails-$850 
Bum Padding-$600 
Shoes and Clothes-$5400
Hata hivyo, msichana huyo ambaye kwa kiasi fulani zoezi hilo limemuweka katika madeni amesema anaona alichokifanya kinathamani ya fedha aliyotoa.

Picha: Muonekano mpya wa Chris Brown

Baada ya kutoka jela, Chris alioanekana kubadilika umbo na kunenepa kiasi cha wengi kuhisi aliishi maisha mazuri akiwa jela. 
Mwimbaji huyo wa New Flame ameonekana kuendeleza mabadiliko kwa kutengeneza mtindo mpya wa nywele na kuzitoa rangi za awali zilizokuwa kichwani kwake.

Saturday, July 12, 2014

Picha: Muonekano mwingine wa rapper Nicki Minaj

Nicki Minaj kwenye huu muonekano ikiwa
Dress by: Fuasto Puglisi - Shoes by: Versace - Jewelry by Tom Ford & Michael Kors




Picha: Baada ya kujibadilisha hivi ndivyo anavyo onekana Vera Sidika bila weave

She shocked all of us when she made the revelation that her Brazilian weave costs more that a second hand Vitz or a plot in Kiserian; a whooping Ksh450,000! By the way, we are yet to come to terms with that story. 

Anyway, as you’re there lamenting how last evening your weave was rained on by the unanticipated Nairobi rain, video vixen Vera Sidika, is not sharing your woes. The bodacious vixen has now ditched her weave for a new look.  She unveiled her new look (my deskie, Sue, tells me it’s called a pixie cut) earlier today and made it clear that she’s “Just trying out something different”. How do you like her new look? Check out;


Tuesday, July 8, 2014

Mwanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda alitamani Wema Sepetu awe wake na sio wa Diamond Platnumz!

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda amesema kabla hajawa kiongozi wake, awali aliwahi kumtamani kimapenzi mcheza filamu Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa kudekadeka.

Kadinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akipiga stori na paparazzi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.

Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika mara ya kwanza.

Credit GPL.

Madhara ya nguo zinazobana



Katika maisha ya kawaida ya binadamu, kila mtu huwa anavaa akiwa na lengo flani kutokana na haiba yake.

Japo malengo kwa wakati mwingine hutofautina, ila wote huwa na lengo kuu ambalo ni la kupendeza, kuvutia  na kuonekana nadhifu mbele ya watu na jamii kwa ujumla.

Mitindo tofauti tofauti inayo endana na wakati huwa inabuniwa na kukivutia kizazi cha wakati huo na pia hukumbana na misuko suko mingi toka kwa jamii za wakati huo, wengine wakipinga mitindo husika na wengine wakikubaliana nayo.

Kelele na malalamiko mengi huwa yanakuwa juu ya uvunjaji wa maadili ya jamii husika. Jamii nyingine zikisema inavuunja maadili na nyingine zikisema hakuna tatizo juu ya mitindo husika
.
Kitu cha muhimu ambacho jamii huwa inasahau ni madhara ya mitindo iyo katika mwili  wa mvaaji.
Hakuna ubishi na ni ukweli usiopingika kuwa  kwa wakati wa sasa na kizazi cha sasa, mtindo wa uvaaji wa nguo zinazobana na kuonyesha maumbile ya mvaaji ndio ambao unakubalikwa na kila jinsia ya sasa.

Kwenye mitaa mingi kwa sasa,ni kawaida kukutana na  kina mama na mabinti wenye maumbile  makubwa (kibantu) ambapo mara nyingi utakuta wakiwa wamevaa suruali za kubana.

Kwa aina ya watu hawa, utagundua kuwa suruali zao zimebana kwakuwa wengi wao huwa hazifungi kwa juu kutokana na maumbile yao na hata kupata tabu  pale wanapo kuwa wanatumia usafiri wa wote mfano daladala, hujikuta kila baada ya dakika wanavuta nguo zao za juu ili ziwasitiri maana nguo zao za ndani huwa zinaonekana. 

Pia wale kina mama na mabinti wembamba ambao miili yao na maumbile sio makubwa, lakini nao utawakuta wamebanwa kuendana  na ngozi za miili yao.

Kwa vijana wa kiume, wanaamini ya kuwa uvaaji wa suruali na mashati yanayo endana na miili yao ndio mtindo wa kisasa na unafanya waonekane nadhifu na kupendeza mbele za watu.

Pia uvaaji wa  nguo za ndani zinazo bana, huifadhi vizuri maumbile yake na humfanya mvaaji awe huru na kutokuwa na wasi wasi haswa pale inapo tokea kwa bahati mbaya, akasisimka maumbile yake akiwa kwenye umati wa watu, hii humfanya asigundulike na yeyote yule na humwepusha pia na aibu na tafsiri mbaya toka kwa wanao mzunguka maana atakuwa kashikiriwa sawa sawia na nguo yake.

Hii ni tofauti na aina za nguo za ndani ambazo huacha sehemu zake za siri kuwa huru zaidi na hata kumfanya mvaaji asiwe huru pale inapotokea maumbile yake yakasisimka akiwa katikati ya umati wa watu ambapo kunaweza pelekea akagundulika na mara nyingine kumwachia aibu kubwa.
Kwa upande wa kina mama na wadada pia, uvaaji nguo zinazobana sana (skintight) ambapo mara nyingi huwa zinavaliwa pamoja na nguo za ndani na huendana na aina ya maumbile ya mvaaji. Kwa mfano wale wenye maumbile makubwa kama mapaja, inawalazimu kuvaa ili kuepuka kuchubuka mapajani.

Pia mtindo  wa uvaaji wa suruali iliyo bana kwao lazima uendane na kuvalia ndani nguo inayo bana (skintight) ili kuepuka kuonekana kwa nguo ya ndani au tofauti na hapo na kutokana na mtindo mvaaji atalazimika kuvaa nguo ya ndani inayo unganishwa na mikanda midogo midogo tu (bikini) ili tu asichoreke. Japo sio lazima na huwa inategemea na ustaarabu au mapenzi ya mtu husika juu ya mtindo wa uvaaji wa suruali inayo bana. 

Tofauti na wengi tufikiliavyo kuwa uvaaji wa nguo za namna iyo inakufanya uwe huru, kupendeza na hata kuendana na wakati, bila ya kutambua kuwa upande wa pili wa shilingi kuna madhara makubwa sana ambayo yanasababishwa na uvaaji wa nguo zinazobana mwili sana.
Tafiti mbali mbali zilizofanyika na madaktari bingwa sehemu tofauti duniani, zimekuja na majibu ambayo yanalenga juu ya madhara ya uvaaji wa nguo za aina iyo.
 Yafuatayo ni madhara yanayo sababishwa na uvaaji wa nguo za kubana upande wa wanaume na wanawake pia. 




1: Kuharibika kwa mishipa ya fahamu
Hii inatokana na ukweli ambao haupingiki kuwa  damu katika mwili wa binadamu inasfiri kwa kasi, na kwa kubana sana misuli ya damu kunako sababishwa na uvaaji wa mtindo huo, hupelekea kuharibu na kuua neva za fahamu.

2: Ugumba
Kwa kiasi pia huchangia ugumba kwa wanaume na wanawake. Ubanaji mkubwa sehemu za siri, huvuruga mishipa na mirija midogo midogo ambayo huusika katika utengenezaji wa mbegu ambazo hutumika katika kutunga mtoto, ivyo kusababisha kutokuwa na ubora unao takiwa kwa hali ya kawaida ili kuwezesha utungwaji wa mtoto. Utengenezwaji katika ubora wa chini na pia Usafirishaji wake duni, hupelekea mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika mimba na hata mwanaume kutokuwa na uwezo wa kuwezesha mimba kutungwa

3:  Kupungua kwa nguvu za kiume
Hili ni tatizo ambalo linawapata haswa wanaume. Korodani za mwanaume zina hifadhiwa na ngozi ambayo hutengeneza joto hitajika kwa ajiri ya utengenezaji wa manii. Kunapokuwa na baridi kali, ngozi husinyaa na kurudisha korodani ndani ili kupata joto na kunapokuwa na joto sana, korodani hurudishwa nje ili kupata joto la kawida. Ivyo kulibana sana kunafanya uvurugaji wa kuingia na kutoka nje kwa korodani na pia  kuharibu mishipa midogo midogo ambayo husambaza na kusafirisha mbegu ivyo kuathiri uzalishaji na usambazaji wa mbegu.

4: Kupata fangasi sehemu za siri.
Hii inatokana na joto kubwa ambalo husababishwa na uvaaji wa nguo inayo bana ivyo kutoa nafasi kwa bacteria ambao husababisha fangasi katikati na pembeni mwa sehemu za siri

5: Kuharibu kibofu cha mkojo.
Msukumo usio wa kawaida unao ongezeka kwenye kibofu cha mkojo unao sababishwa na uvaaji wa nguo zinazo bana, hupelekea bacteria kuzaliana kwa wingi na kuingia kwenye njia ya mkojo na ivyo kuharibu kibofu na njia pia ya mkojo.

6: Mapaja kufa ganzi (Meralgia Paresthetica)
Pia hii inatokana na kukazwa sana kwa mishipa inayo safirisha damu, na misuli pia hushindwa fanya kazi yake kwa ufasaha, ivyo kufanya mapaja kufa ganzi.
Makala kwa msaada wa kampuni ya TENA inayo husika na kampeni ya usalama wa watumiaji wa bidhaa mbali mbali pamoja.

Urembo wa nyusi/Shaping your eyebrows



Nyusi ulizonazo kabla ya kutumia wanja zitatengeneza base ya kushape na kudefine.
Mfano nyusi hizo kwenye picha mwishoni ni nyembamba zinahitaji kupunguzwa kidogo na kuzipa mkunjo kidogo.

Nyusi zianzie wapi?






Zisianze mbali na macho yako yanapoanzia, unapozipunguza uwe makini na hili.

Mkunjo/Arch ya nyusi ianzie wapi?


Mkunjo wa nyusi zako uanzie karibu na nusu ya nyusi zako kama nyuzi 90 (90 degrees) kutoka kwenye pua .Usipandishe mkunjo wa nyusi sana, haitapendeza na nyusi zitakupa muonekano tofauti kidogo.

Nyusi iishie wapi?


 Nyusi isipitilize sana mwisho wa macho yako kwa mtazamo wa uhalisia zaidi (natural look).
Kunyoa nyusi mno mara nyingi inasababisha zipoteze kujaa kwake na kupungua ujazo.
Jazia sehemu ambazo hazina nyusi kwa kutumia wanja unaoendana na rangi ya nyusi zako, make-up ni kwa ajili ya kuongezea uzuri wako wa asili na si kubadilisha mwonekano wako wa uhalisi. Hakuna mwenye nyusi nyekundu, kijani au bluu jitahidi utumie wanja wa brown au mweusi unaoendana na rangi ya nyusi zako kwa kuchora kwa mbali kiasi na si kwa mgandamizo ili uvutie zaidi



Nyusi zikitengenezwa vizuri uzuri wa macho na shape ya macho inaonekana sawia kama picha hapo juu.
Ikiwa unakutana na mtu na kitu cha kwanza unachokiona kwake ni nyusi zake, hakika zitakuwa hazipo katika shape inayotakiwa au ametumia wanja wa kupitiliza.