Rapper Quick Rocka amezindua nguo za kampuni yake ‘Switch Clothing Line’ alizozipa jina la ‘Switch Like Me’. Akiongea na Kikwetu Blog, Quick amesema kwa kuanza ameanza na t-shirt za rangi mbalimbali ambazo tayari zipo sokoni. “Tumeanza na t-shirt lakini ndani ya mwezi nimeplan kufanya kitu kikubwa zaidi. Tunataka kufanya kwa quality kubwa, kwenda kuprintia China ambayo itakuwa ni t-shirt na kofia pia,” amesema Quick.
Pamoja na biashara ya t-shirt, Quick Rocka alifungua studio yake ya muziki iitwayo Switch Studio.
Sunday, August 3, 2014
Quick Rocka azungumzia nguo zake za ‘Switch Like Me’ zilizoingia sokoni hivi karibuni
Labels:
Entertainment,
Fashion