Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

‹
›

Shooting

Racing

News

Bottom

Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Wednesday, August 6, 2014

Michuano ya klabu Bingwa Afrika mashariki na kati maafuru Kagame Cup inaanza Agosti 8 mwaka huu

Kindumbwe ndumbwe cha michuano ya klabu Bingwa Afrika mashariki na kati maafuru Kagame Cup kinaanza kesho ambapo mechi ya ufunguzi ya Kundi A ni kati Atlabara ya Sudan Kusini ambayo itamenya na KMKM ya Zanzibar kuanzia saa saba mchana.

Mechi ya pili itakuwa ni mechi ya kundi B kati ya Gor Mahia ya Kenya ambao watapepetana vikali na KCCA ya Uganda . 

Wenyeji Rayon sports ya Rwanda itashuka dimbani kumenyana na Azam ya Tanzania katika mechi nyingine ya kundi A. 

Azam ya Tanzania imepata nafasi ya kucheza michuano hiyo baada ya Yanga pia ya Tanzania kuondolewa kwa kutotimiza vigezo vya michuano hiyo ambapo ni pamoja na kupeleka kikosi cha pili cha timu hiyo.

Thursday, July 31, 2014

Soma hapa mambo kumi yanayomweka juu zaidi mchezaji Neymar wa Brazil

1: Kabla ya Barcelona, Neymar ameichezea klabu moja tu ambayo ni Santos. Hii ilikuwa baada tu ya kutoka kwenye shule ya soka ya Santos aliyojiunga nayo mwaka 2003 akiwa na miaka 11. 
2: Alifunga goli lake la 100 kwenye maisha yake ya soka tarehe 5 February 2012, ilikuwa siku yake ya kuzaliwa na alikuwa anafikisha miaka 20. 

3: Real Madrid walitaka kumsajili toka akiwa na miaka 14, walifatilia maisha yake ya soka mpaka kumpa dili,Neymar alipitia mambo yote mpaka vipimo vya afya ila mwaka 2011 ilishindikana kwenda Real pale Santos walipotoa pesa nyingi zaidi kumbakiza Brazil. 
4: West Ham ndio klabu kubwa ya kwanza kutaka kumsajili Neymar baada ya kuona kipaji chake, Ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 12, ndio chanzo cha Neymar kutambulika kama mchezaji wa kimataifa zaidid,ikafwatiwa na Chelsea. 

5: Neymar alikosa namba kwenye kikosi cha timu ya taifa ya brazil ya kombe la dunia la mwaka 2010 kilichopangwa na Dunga, hakuwepo hata kwenye wachezaji wa dharura ingawa Pele na Romario walipendekeza awepo. 
6: Neymar amekuwa baba akiwa na miaka 19,mtoto wake wa kwanza wa kiume anaitwa David Lucca na mpaka sasa Neymar hajaijulisha dunia mama wa mtoto ni nani. 

7: Neymar ni mchezaji wa tisa kwenye orodha wa wachezaji wa Barcelona walionunuliwa kwa ada kubwa zaidi. Ada yake ya uhamisho ni €57 million. 
8: Ukizingatia wachezaji wakali wanaotoka Brazil, Neymar ndio mchezaji wa kwanza wa Brazil kukava jarida la Time, Na Wabrazil wengi waliokava jarida hili ni wanasiasa. 

9: Neymar alivyojiunga na Barcelona alipewa dili linalomlipa dola milioni 74 ndani ya mwaka mmoja, mwaka 2012 alitajwa kuwa mchezaji wa saba tajiri zaidi duniani huku jarida la Forbes likimtaja kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani mwenye miaka chini ya 25. Kwa sasa ni wa sita kwenye wanasoka na wanamichezo matajiri zaidi duniani. 
10: Mwaka 2012  na 2013 Neymar ametajwa kuwa mchezaji anayeuza zaidi akiwekwa kwenye matangazo na Jarida la SportsPro na kuwafunika wachezaji kama Ronaldo, Messi,Rory McLlroy na Usain Bolt.

Wafahamu mastaa wa soka wasiokuwa na muonekano wa mchezo huo

Unaambiwa iliuweze kuwa shabiki mzuri wa soka baadhi ya vitu kama ftina na majungu huna budi kukutana navyo iwe katika shughuli zako za kutafuta pesa , au kwenye viwanja vya soka wakati wakuzishuhudia mechi haswa zile za watani wajadi. 
Bila kusahau kwenye ‘vibanda-umiza’ ambako ndiko utamu pamoja na mzuka wa soka ulipo. 

Katika ushabiki huo pia utapata fursa za kuzifahamu a.k.a za baadhi ya mastaa mahiri kwa mfano mashabiki wengi wa soka hupenda kumuita Luis Suarez zombi (Vampire),  kutokana na tabia zake za kung’ata wachezaji wa timu pinzani pale anapoona amezidiwa. 
Pia unaambiwa wapo baadhi ya mastaa wa soka wasiokuwa na muonekana wa mchezo huo, baadhi ya mastaa hao ni kama wafuatao pamoja na kazi wanazopaswa kuzifanya njee ya soka;

Mario Balotteli (Gangster Rapper/hip hop), 
Wayne Rooney (Boxing) 
Gerrald Pique (Taxi Driver), 

Bacary Sagna (Native doctor) 
Oliver Giroud (Modelling),  
Daniel Osvaldo (Actor) 
Aristedi Bance (Armed Robber), 

Ramires (Sugar-cane seller) 
Scott Parker (Choir master), 
Raheem Sterling ( Athletics) 
Kaka (evangelist), 

Ronaldo (love-vendor) 
Messi (house boy), 
Bale (hunter) 
De Gea (sales boy),  

Luis Suarez (vampire) 
Kompany (military), 
Demba Ba (imam) 
Ibrahimovic (looking like Colombian drug dealer)

Thursday, July 24, 2014

Picha: Angalia starehe zinazofanywa na shujaa wa Ujerumani Mario Gotze akiwa na mpenzi wake

Shujaa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Mario Gotze ameonekana kama mtu mwenye kichaa baada ya kuendelea kujivinjari katika kipindi hiki cha mapumziko, kabla ya kurejea Allianze Arena kujiunga na wachezaji wenzake wa FC Bayern Munich. 

Gotze, aliefunga bao la ushindi dhidi ya Argentina wakati wa mchezo wa hatua ya fainali kwenye michuano ya kombe la dunia ameonekana katika hali hiyo akiwa na rafiki yake wa kike, Ann Kathrin Brömmel.

Wawili hao walikutwa wakiogelea kwenye dimbwi la matope katika moja ya fukwe huko nchini Ujerumani, na kisha walijitokeza hadarani wakiwa na mandhari ya kama watu waliorukwa akili, lakini mwisho wa siku imefahamika ilikuwa ni moja ya starehe yao wakiwa mapumzikoni. 

Ann Kathrin, kwa mara ya mwisho alionekana akiwa na Mario Gotze mara baada ya mchezo wa hatua ya fainali wa michuano ya kombe la dunia dhidi ya Argentina, uliochezwa nchini Brazil katika uwanja wa Maracana, akishangilia ushindi wa bao moja kwa sifuri.



Video: Mashabiki wa Palestina wavamia mchezo wa Macabi Haifa ya Israel

Mchezo wa kirafiki kati ya klabu ya Lille ya nchini Ufaransa dhidi ya Macabi Haifa uliochezwa nchini Uturuki, umeingia dosari baada ya kundi la mashabiki waliokuwa wamebeba bendera ya Palestina kuingia uwanjani.

Kitendo hicho ambacho kilizua vurugu kwa dakika kadhaa, kilijitokeza datika dakika ya 84 ya mchezo ambapo katika hali ya kushtukiza mashabiki hao walijitosa uwanjani pasina uwoga wowote.

Mbali na kundi la watu kuingia uwanjani, picha za televisheni zilimuonyesha mmoja wa wavamizi hao wa uwanja akipigana na mchezaji wa klabu ya Macabi Haifa, kitendo ambacho kimeashiria tofauti zilizopo kati ya Palestina na Israel.
Hata hivyo klabu ya Maccabi Haifa ina historia kubwa ya kuwa na wachezaji wengi kutoka nchi za kiarabu kama Taleb Tawatha, Mohammadou Idrissou, Weaam Amasha, Ataa Jaber, Mohammed Kalibat pamoja na Ismaeel Ryan.

Monday, July 21, 2014

Nahodha wa England na Liverpool Steven Gerrard astaafu soka

Nahodha wa England na club ya Liverpool Steven Gerrard hatimaye ametundika daruga kuichezea timu ya taifa lake la England akiwa na miaka 34. Gerrard amejiimarisha kwenye kikosi cha uingereza tangu mwaka 2000 walipoipiga Ukraine kwa mabao mawili kwa nunge. 
Steven Gerrard

Kiungo huyo wa Liverpool amesema aliufurahia muda wote alipoichezea timu ya taifa na kwa kweli ni siku ya masikitiko kwake. 
Hivi sasa Gerrard atakuwa katika nafasi za juu za ubalozi katika chama cha soka cha England. 

Anastaafu akiwa amecheza michuano mikubwa sita na kufunga mabao 21. Na hivyo kushika nafasi ya tatu baada ya Peter Shilton na David Beckam.

Thursday, July 17, 2014

Wachezaji hawa walikuwa na mvuto mkubwa kiasi cha kuotewa na vilabu vyenye thamani ya mamilioni duniani

Huenda sio wachezaji wageni , lakini michuano ya kombe la dunia Brazil iliwaleta wachezaji hao kwa sura tofauti sana kwa mashabiki wa soka duniani. 
Hata cha muhimu zaidi ni kwa mawakala wa wachezaji hao, wachezaji wao walipata kuvutia vilabu ambazo bila shaka ni vilabu vyenye thamani ya mamilioni ya dola kuvutiwa na talanta zao. 
Hawa ni wachezaji watano waliokuwa na mvuto wa kipekee na ambao walivutia vilabu ambavyo huenda wakasaini mikataba nao.

James Rodriguez

Mshindi wa Golden Boot, alikuwa mchezaji aliyewavutia wengi na ambaye amekuwa gumzo katika vilabu vikubwa barani Uropa. 
Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 23, aliingiza mabao sita katika mechi tano na kufikisha klabu yake katika robo fainali kabla ya kushindwa na Brazil  Rodriguez alihamia Monaco kutoka Porto mwaka jana lakini mchezo wake ulikuwa wa kufana Brazil, hasa katika mechi yao dhidi na Uruguay. 
Mechi hiyo, ilimuweka machoni mwa vilabu vikubwa Ulaya hali ambayo bila shaka imepandisha thamani yake kutoka pauni milioni 38.5.


Toni Kroos

Mchezaji huyu hafichiki katika timu ya Ujerumani. Ana nguvu na sifa yake haina doa. Ametajwa kuwa mchezaji mahiri sana katika timu ya Ujerumani. 
Mchezaji huyu anaonekana kuwa tayari kuondoka ligi ya Bundesliga.  Alivyocheza katika mecho zote sana imemfanya kusakwa na Real Madrid.  Kroos anayechezea Bayern Munich, aliingiza mabao mawili katika ushindi wa mabao saba dhidi ya Brazil na alionekana kusaidia sana wenzake katika kuingiza mabao. 
Mchezaji mwenzake kiungo cha kati, Sami Khedira, huenda akamtengezea nafasi katika klabu ya Real huku ripoti zikisema yeye anaonekana kuelekea Arsenal.

Paul Pogba

Mchezaji huyu anaonekana kuwa na 'injini' kubwa inayompa kasi kama alivyoonekana akichezea Ufaransa. 

Alitajwa kama mchezaji mwenye umri mdogo katika kombe la dunia na kupata sifa kedekede wakati wote wa mashindano baada ya kusaidia timu yake kufika robo fainali ambapo walichabangwa na mabingwa Ujerumani. 

Pogba mwenye umri wa miaka 21, aliingiza bao lake la kwanza dhidi ya Nigeria katika awamu ya timu bora kumi na sita na atakuwa katika msitari wa mbele wakati Deschamps ikipanga kuwa mwenyeji wa kombe la mabingwa wa ulaya miaka miwili ijayo. 

Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, huenda akarejea nyumbani hivi karibuni kwani klabu ya Paris St-Germain inamuotea.

Xherdan Shaqiri  

Amebandikwa jina la Alpine Messi, kama jina lake la utani. 
Mchezaji huyu raia wa Uswizi ametajwa kama nambari moja kuingia Liverpool huku klabu hiyo ikitafuta mchezaji atakayejaza nafasi ya Luis Suarez. 
Mchezaji huyu wa Bayern Munich, aliingiza bao la pekee kwa mguu wake wa kushoto katika kombe hilo walipokuwa wanacheza dhidi ya Honduras, na alitajwa mchezaji bora wa mechi mara mbili.  Hii ni baada ya kusaida timu yake kufika awamu ya kumi na sita bora dhidi ya Argentina.

Guillermo Ochoa

Kwa sasa mchezaji huyu hana mkataba na klabu yoyote hasa baada ya kuondoka Ajaccio nchini Ufaransa. 
Raia wa Mexico, alicheza vyema sana na vilabu vimeonekana kumuotea sana vikitafuta kipa mpya. 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alifanikiwa kutajwa kama mchezaji bora zaidi alipoinyima Brazil fursa katika awamu ya makundi kabla ya kung'olewa makali na vijana wa Louis van Gaal. 

Timu hiyo iliondoka katika awamu ya makundi kumi na sita bora lakini Ochoa alisemekana kuwa mchezaji bora zaidi katika mechi yao ya mwisho. 
Anajiunga na Manuel Neuer, Tim Howard naKeylor Navas - ambaye ana mvuto wake kwa vilabu baada ya mchezo wa kufana wa Costa Rica, kama kipa bora zaidi wa michuano ya kombe la dunia.

Tuesday, July 15, 2014

Video: Angalia kikosi cha Ujerumani kilivyopokelewa kwa shangwe nyumbani

Mabingwa wa soka duniani timu ya taifa ya Ujerumani wamewasili nyumbani hii leo na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wa soka wa nchi hiyo.

Kikosi cha Ujerumani ambacho kilitwaa ubingwa wa kombe la dunia mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuifunga Argentina, katika mchezo wa fainali huko nchini Brazil kimewasili mjini Berlin majira ya asubuhi kwa saa za nchini humo.

Wachezaji pamoja na maafisa wa shirikisho la soka nchini Ujerumani ambao walikwenda nchini Brazil wameonkana wakishuka kwenye ndege kwa furaha, huku nahodha Philip Lahm akiwa ameshikilia kombe la FIFA la dunia.

Mashabiki mbalimbali wamejitokeza katika mitaa ya mji wa Berlin kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa ambao walikuwa kwenye gari la wazi.


Monday, July 14, 2014

Picha: Baada ya ushindi wa Ujerumani FIFA World Cup 2014, Hihi ndivyo Rihanna alivyo jirusha na wachezaji hao

Kwenye fainali ya kombe la dunia msanii Rihanna aliweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa Ujerumani tangu mechi inaanza. Rihanna alikuwa kwenye jukwaa la watazamaji akiwa na jezi ya Ujerumani na alionekana akishangilia sana baada ya goli lililoipa ushindi ujerumani likifungwa. 

Baada ya mechi kuisha Rihanna alijumuika pamoja na wachezaji wa Ujerumani kusherekea ubingwa mara baada ya mechi. Hizi ni picha zake akiwa na wachezaji wa nchi hiyo.






Kocha wa timu ya taifa ya Brazil,Luiz Felipe Scolari, ameacha kazi kama meneja wa timu hiyo

Scolari amelaumiwa kwa kichapo ilichopata Brazil
Ripoti nchini Brazil zinasema kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil,Luiz Felipe Scolari, ameacha kazi kama meneja wa timu hiyo. 

Scolari alilaumiwa pakubwa sana kwa timu ya Brazil kupata kichapo kibaya ilipocheza na Ujerumani ambao wameibuka mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu. 

Kichapo hicho kilikuja wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani. 
Taarifa rasmi huenda ikatolewa baadaye leo na shirikisho la soka la Brazil.

Credit BBC.

Video: Magoli 10 bora ya FIFA World Cup 2014, Brazil

Video: Magoli 10 bora ya FIFA World Cup 2014, Brazil


Sunday, July 13, 2014

Ujerumani ni bingwa wa kombe la dunia, tuzo za wanasoka bora wa michuano

Mario Götze anaipatia Ujerumani bao la ushindi.  

Ujerumani wanakuwa timu ya kwanza ya kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika mchuano ulioandaliwa Kusini mwa Marekani. 
Ujerumani ilihitaji bao la muda wa ziada la Mario Gotze kuinyamazisha Argentina katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Maracana. 
Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.

Kipa Nuer wa Ujerumani alituzwa ''Golden Glover''
Huku Messi akituzwa kama mchezaji bora 'Golden Ball''
Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''. 
Ijapokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo la ''Golden Ball''. 

Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwepo Maracana kwa mualiko wa rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Brazil Dilma Rousseff. 

Putin alipewa ithibati rasmi ya kuwa mwenyeji wa makala yajayo ya kombe la dunia la mwaka wa 2018. 

00:25 Mario Gotze anaiweka Ujerumani mbele 
00:24 GOOOOOOOOAL 
00:08 Palacio anapoteza nafasi nyengine huku Messi akionekana kulemewa na walinzi wa Ujerumani.
00:02EXTRA Time imeanza .

Mechi imekwisha .
Argentina 0-0 Ujerumani 90''.
Gotze aiweka Ujerumani mbele 1-0
Sasa ni Muda wa Ziada (Extra Time) 
00:90 Argentina 0-0 Ujerumani 90''. 
00:90Muda wa kawaida umekamilika katika fainali hii .

00:87 Miroslav Klose anaondoka 
00:86 Joachim loew anajibu kwa kumuingiza Gotze 
00:85 Argentina inajiandaa kufanya mabadilikokatika safu ya kati Gago anaingia

00:81 Argentina 0-0 Ujerumani 82''. 
00:80 Krooooooooos anapoteza nafasi nyengine 
00:70 Ujerumani inakosa tena Schurrle

00:65 Kadi ya njano Mascheranona na Aguero 
00:60 Argentina 0-0 Ujerumani 60''. 
00:58 Argentina 0-0 Ujerumani

00:55 Nuer anambonda Higuain lakini refarii anasema ni Freekick kuelekea lango la Argentina 
00:48 Goalkick kuelekea upande wa Argentina 
00:46 Messi anapoteza nafasi nyengine 
22:45 Sergio Aguero anaingia badala yake Ezequiel 
22:45 Ujerumani 0-0 Argentina 
22:45Kipindi cha pili kinaanza huko Maracana

Argentina 0-0 Ujerumani 10''
22:45 Halftime .Ujerumani 0-0 Argentina 
22:45 Ujerumani wanapoteza nafasi nzuri mkwaju wa kichwa unapogonga mwamba na msaidizi wa refarii anasema ni Offside kwa Thomas Muller 
22:39 Lionel Messi ananyimwa fursa ya kufanya mashambulizi 
22:37 Ujerumani wanafanya shambulizi lingine . 
22:35 Higuan anafunga lakini refarii anakataa anasema aliotea . 
22:20 Gonzalo Higuan apoteza nafasi ya wazi akiwa amesalia pekee yake na na kipa Nuer 
22:18 Ujerumani 0- 0 Argentina 20'' 
22:14 Kona kuelekea upande wa Argentina. 
22:13Freekick kuelekea lango la Argentina lakini wapi unagongwa nje na unakuwa wa kurushwa kuelekea Argentina. 
22:10 Kona ya kwanza katika mechi hii kuelekea upande wa Ujerumani 
22:09 Messi anaongoza shambulizi hadi ndani ya eneo la lango lakini mjerumani hapishi.

22:05 Ujerumani 0- 0 Argentina 
22:03 Argentina wanashambulia lango la Ujerumani lakini wapi . 
22:01 Freekick kuelekea lango la Argentina . 
22:00 Mpira umeanza .

Argentina wakiwa wamevalia sare ya samawati Ujerumani ikiwa na Jezi Nyeupe . 
Timu zimeingia uwanjani tayari kwa fainali hii. 
Wimbo wa taifa wa Ujerumani unapigwa kisha ule wa Argentina . 
Vijana wa Joachim Loew wanamtarajia mfungaji wao nyota Miroslav Klose akisaidiana na Thomas Muller kuwapa mabao na hatimaye ushindi dhidi ya Argentina . 
Kwa Upande wao Ujerumani imesifiwa kwa kuwa na uwezo wa kipekee wa kucheza kama kikosi wala sio kumtegemea nyota mmoja kwa ufungaji mabao.

Je Historia itajirudia ?  

Argentina nayo inakumbuka vyema matukio ya miaka 28 iliyopita ilipoilaza
Ujerumani Magharibi wakati huo na kutwaa kombe lao la mwisho la dunia  Ujerumani ilishinda mara moja nayo Argentina ikaibuka mshindi mara moja kwa hivyo hii leo itakuwa mechi ya kukata na shoka . 
Wajerumani wakiandikisha rekodi kwa kuinyeshea wenyeji Brazil jumla ya mabao 7-1 katika nusu fainali huku Argentina nayo ikihitaji muda wa ziada na hata mikwaju ya penalti kuibandua Uholanzi na kufuzu.

Ujerumani itakuwa timu ya kwanza kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika Marekani ya kusini iwapo itaipiku Argentina. 
Timu hizi zimechuana mara 2 katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 1986 na 1990.

Katika mechi hii ya leo Mahasimu hawa wanafahamiana sana. 
Hayo yote ni kenda timu hizo zote zilikuwa zikiwania kuandikisha majina yao kwenye tuzo la kipekee la dhahabu yaani kombe la dunia. 
Mechi hiyo ndiyo itakayokuwa kilele cha majuma manne ya kipute hicho kilichojumisha timu 32 kutoka mabara yote 5 zikichuana miongoni mwao katika miji 12 ya Brazil kuanzia juni tarehe 12 .

Mahasaimu wa Jadi Argentina wanachuana na Ujerumani katika fainali yao ya tatu katika historia ya kombe la dunia. 
Macho yote duniani yanaelekea katika uwanja wa Maracana ulioko Rio Brazil ambapo mechi ya fainali ya kombe la dunia itachezwa muda mchache ujao. 
Jumapili ya tarehe 13 Julai mwaka wa 2014 hatimaye imewadia .

Uholanzi yailaza Brazil 3-0,Uholanzi yashika nafasi ya 3 kombe la dunia

Hatimaye michuano ya kombe la dunia inafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina, wakati usiku wa jana mshindi wa 3 wa michuano hiyo aliamuliwa kwa mechi kati ya Uholanzi vs Brazil. 

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo, Brasilia, uliisha kwa matokeo ya ushindi wa 3-0 kwa Uholanzi, kikiwa kipigo cha pili cha Brazil ndani ya juma moja tangu walivyopokea kipigo cha magoli 7-1 kutoka Ujerumani.  Magoli ya Uholanzi yalifungwa na Van Persie, Blind na Georginio Wijnaldum. 

Wakati kocha wa Uholanzi Louis Van Gaal akielekea Manchester United, kocha wa Brazil Luis Fellipe Scorali amesema pamoja na kuvurunda kwa Timu yake lakini hawezi kujiuzulu na hatma yake anaiacha mikononi mwa waajiri wake shirikisho la soka la Brazil.

Saturday, July 12, 2014

Neymar arejea kambini Brazil

Neymar Jr. atakosa mechi ya leo ya kuwania mshindi wa tatu kati ya Brazil na Uholanzi baada ya kupata majeruhi ya kuvunjika mshipa wa mgongo kwenye mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia.
Nyota mwenye majeraha Neymar amerudi kwenye kambi ya Brazil iliyopo Teresopolis kwa mara ya kwanza tangu avunjike mshipa mgongoni ambao ulizima ndoto za kumaliza Kombe la Dunia. 

Neymar aliweza kutembea bila msaada kwenda kuwasalimia wachezaji wenzake, ambao walikuwa wakifanya mazoezi wakati anawasili. Na atakuwa na timu hiyo wakati wa mechi ya kugombea mshindi wa tatu watakapominyana na Uholanzi siku ya Jumamosi. 
Brazil bila mfungaji wao, tumaini la kunyakua taji hilo la dunia kwa mara ya sita lilizimika baada ya kuchapika magoli 7-1 na Ujerumani siku ya Jumanne. 

Nyota huyo, 22, amekuwa akipona taratibu nyumbani kwake baada ya kupata majeraha kwenye mechi ambayo Brazil ilishinda 2-1 dhidi ya Colombia. 

Klabu ya Barcelona ilithibitisha kutuma madaktari wake kumtembelea mchezaji huyo na wanaamini atakuwa fiti wakati ligi yao itakayoanza Agosti 23. 
“Mchezaji wetu anaendelea vizuri, na ataendelea na matibabu mjini Barcelona yatakayoanza Agosti 5”, ilieleza taarifa ya klabu.

Mario Balotelli awalengeshea mtutu wote ‘wanaomchukia’

Picha hiyo imeshatolewa kwenye mtandao wa Instagram.
Mchezaji wa Italia na AC Milan Mario Balotelli ameibua utata mkubwa baada ya kutuma picha yake akiwa amelengeshea mtutu kwenye kamera. 
Picha hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, ilikuwa na ujumbe unaosema: “busu kwa wote wenye chuki”. 
Mchezaji huyo aliyejiunga na AC Milan akitokea Manchester City mwaka 2013, amekuwa katika mizozo na pia kutafutwa na wabaguzi wa rangi.

Hivi karibuni alikosolewa kwa uchezaji wake kwenye Kombe la Dunia. Tukio hilo la picha, halikutiliwa maanani na makamu wa rais wa AC Milan Adriano Galliani aliyedai kuwa kushughulikia suala hilo ni kuingilia haki za mtu binafsi. 
Balotelli amekuwa kwenye matatizo kwa miaka kadhaa. 
Mwaka 2010, alipiga risasi angani akiwa kwenye mgahawa wa pizza wa Della Republicca wa mjini Milan na 2011 maafisa wa Manchester City walimfanyia uchunguzi baada ya kurusha kimshale kwa mchezaji kinda kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo.

liwahi kuripotiwa kuwa Mario alikuwa akikusanya maelfu ya pauni kama faini za maegesho ya magari mjini Manchester, na aliitwa kuhojiwa na kocha Roberto Mancini.

Mapenzi yanoga licha ya kipigo Brazil

Beatriz Groxco na Federico Astorga
Wengi wamekiita kipigo cha karne baadhi wakasema kilikuwa kimbunga cha magoli, yote tisa, kumi ni kwamba majonzi yalijaa Brazil baada ya timu yao kupokea kipigo kutoka kwa Ujerumani katika nusu faiunali ya kwanza ya kombe la dunia. 

Lakini licha ya huzuni wote huo, kunao mashabiki ambao wameitumia fursa ya kuwepo kombe la dunia Brazil kujinawirisha kimapenzi.

Alejandro Yemes ni raia wa
Venezuela na Danielle Voellinger
ni mmarekani
Itakushangaza kuwa mapenzi yamenoga kati ya mashabiki wa timu hasimu ambao wamepata penzi tamu licha ya uhasimu wa timu na nchi. 
Kwa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25 raia wa Brazil,
Beatriz Groxco, ametupilia mbali uhasimu wake wa kihistoria na Argentina kwa kukutana na mtu ambaye sasa amekuwa mpenzi wake Federico Astorga, shabiki wa Argentina. 

Federico alikuwa njiani kuelekea Sao Paulo kwa mechi alipokatizia safari yake mjini Curitiba nyumbani kwa Beatriz. Tangu hapo mapenzi yamewanogea. 
Walikutana wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo tarehe 12 Juni, siku hiyo ilikuwa siku ya wapendano Brazil, hawajaachana tangu hapo. 

"nilikuwa naelekea mjini ambako kuna baa nyingi wakati aliponiomba kumuelekeza, '' asema Beatriz. 
''Mashabiki wa Brazil, huwakejeli mashabiki wa Argentina , lakini kwetu sisi mambo yalikuwa tofauti kwa sababu sote tunapenda soka.'' 
Mashabiki wengi mjini Rio walichagua Copacabana kama sehemu ya kukutana na kutazamia michuano hiyo.

Alejandro Yemes raia wa Venezuela na Danielle Voellinger mmarekani walikutania Vila Madalena.  "tulikutanahishwa na rafiki yetu, ambaye sote wawili tunamjua kwani tulisoma naye karibu na mji wa Sao Paulo na tukakubaliana kukutana katika kombe la dunia,'' asema Alejandro.

'Mitandao ya mapenzi'  

Douglas Rodriguez
Uhusinao wa kimapenzi pia umenawiri kwenye mitandao, kwa usaidizi wa programu za mapenzi au 'Apps'. 
Moja ya programu hizo ni Tinder, ambayo ilishuhudia ongezeko la kutumiwa wakati wa kombe la dunia. 
Valentina mwenye umri wa miaka 33 anasema amekuwa akitumia programu hiyo wakati huu kutafuta mapenzi. 
"kwangu mimi , sio tu kuwa na uhusiano wa mapenzi na watu, mimi hupenda kuwasaidia wageni wanapofika Brazil. ''

Hadi sasa amekutana na watu wawili, mmoja kutoka Uswizi na mwengine mmarekani.  Programu za mapenzi pia zimekuwa zikitumiwa na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. Programu ya mapenzi inayotumiwa na wapenzi wa jinsia moja 'Grindir' ilipata ongezeko la asilimia 31 ya watumiaji wakati huu wa kombe la dunia. 

Hili halijanishangaza, kuna wachezaji wengi ambao wamejitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja.Kwa hivyo iwe mchezaji au shabiki, wote wanatumia programu hiyo. '' 

Douglas Rodriguez,mwenye umri wa miaka 22 kutoka Porto Alegre, anasema kuwa tangu kuanza kutumia programu hiyo wakati huu wa mashindano, amekuwa akienda kurusha roho zaidi ya mara tatu kwa wiki na watalii ambao amekutana nao kwenye mtandao.

Friday, July 11, 2014

Neymar aeleza mkasa mzima, amuunga mkono Messi

Kabla yakufanya mahojiano na waandishi wa habari, Neymar, 22, katika hali ya majonzi alikwenda kuwasalimia wachezaji pamoja makocha wa timu yao ya taifa wakati wakifanya mazoezi katika kambi yao kwa ajili ya kujianda na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu dhidi ya Uholanzi, mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi. 

Katika mahojiano hayo Neymar alizungumzia juu ya kuombwa msamaha na mlinzi wa Colombia aliyemsababisha akose mechi yao ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani. 

“Carlos Zuniga alinipigia simu na kuniomba msamaha na nikakubali,  sidhani kama alikuwa amedhamiria kuniumiza lakini kwa watu wanaojua mpira wa miguu nadhani ile haikuwa rafuu ya kawaida”, alieleza Neymar. 

Inasemekana kwamba Neymar alizima televisheni yake mara baada ya Ujerumani kufunga goli la saba, katika mchezo huo ambao uliishia kwa magoli 7-1.  “Nilihisi kuchanganyikiwa na kutoamini kilicho tokea”, alisikika Neymar  Pia aligusia mchezo wa fainali ambapo watani wao wa jadi Argentina watacheza na Ujerumani. 

“Mimi sio shabiki wa Argentina ila nataka wachezaji wenzangu wa Barcelona Messi na Mascherano wachukue Kombe la Dunia, timu yangu ni Messi football club.”

Thursday, July 10, 2014

FIFA imeipiga marufuku Nigeria kwa muingilio wa serikali

Nigeria imepigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA. 
Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini. 

Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa. 
FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo. 

Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo. 
FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.

Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15)

Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil. 
Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil. 

Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn'goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF . 

Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia na Ufaransa . 
Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.

Wednesday, July 9, 2014

Nusu fainali ya pili Brazil, Waholanzi wawakebehi Argentina

Wakati mashabiki wa soka wa nchini Brazil wakiendelea kujiuliza KULIKONI? Vyombo vya habari vya nchini Uholanzi vimeanza mbwembwe kuelekea katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ambapo timu ya taifa ya nchi hiyo itapambana na Argentina. 

Gazeti la De Telegraph la nchini Uholanzi limetoa picha ya kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo ilimkebehi mchezaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi. 

Picha hiyo ya kejeli imeweka katika ukrasa wa mbele wa gazeti hilo, kwa kuashiria Argentina hawana chao kuelekea kwenye mchezo huo ambapo mshindi atakaepatikana ataungana na Ujerumani katika mchezo wa hatua ya fainali uliopangwa kuchezwa siku ya jumapili huko nchini Brazil.

Gazeti lingine la nrc nalo limetoa picha inayomkebehi Lionel Messi, ambaye ni nahodha wa kikosi cha Arngetina ambapo bado picha hizo zinachukuliwa kama ushindi wa vita ya nje ya uwanja. 

Katika gazeti hilo picha ya Lionel Messi inaonekana akiwa anakamua juisi ya machunga ambayo itanywewa na na wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi mara baada ya mchezo wa hii leo.

Kama umeipenda mechi ya FIFA World Cup 2014 Brazil vs Germany unaweza ku download hapa

Michuano ya kombe la dunia leo imechukua sura nyingine kabisa baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Ujerumani. 

Kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Belo Horizonte – Ujerumani wameweka historia ya mbili kubwa – kutinga fainali ya 8 ya kombe la dunia – hii ni mara nyingi kuliko timu zote duniani, pili kuifunga Brazil nyumbani kwao ikiwa ni mara ya kwanza kwa Brazil kupoteza mechi ya ushindani kwenye ardhi yao tangu mwaka 1975. 

Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Muller, Toni Kroos mawili, Sami Khedira, Ander Schurrle nae akafunga mawili huku Oscar akiifungia Brazil goli moja la kufutia machozi katika mechi iliyoishwa kwa ushindi wa 7-1. 

Ujerumani sasa anamsubiri mshindi wa kati ya Argentina vs Uholanzi hapo kesho ili kupata kujua mpinzani wake wa fainali itakayopigwa jumapili hii.

Ku download mchezo mzima tumia/copy link hapo chini kisha enjoy.
kickass.to/fifa-world-cup-2014-semi-final-brazil-vs-germany-720p-hdtv-x264-w4f-rartv-t9309250.html
Kama hukufanikiwa kutazama magoli yote tembelea hapa
FIFA World Cup 2014 Brazil 1-7 Germany, tazama video ya magoli yote hapa.

Usisahau kutupa maoni yako.