Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Showing posts with label Gossip. Show all posts
Showing posts with label Gossip. Show all posts

Wednesday, August 6, 2014

Ile kauli ya Diamond kwamba hawezi kuoa kamwe, yamchefua Wema

KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.

Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari; ‘DIAMOND: SITAOA KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka kisanii.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond. 
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein. 

“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.

“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine haiwezekani kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho ndicho kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema Diamond,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: 

“Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife material (mke mwema) kwa hiyo  anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo mahaba niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito.”

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mlimbwende huyo anayeshikilia Krauni ya Miss Tanzania 2006 ili kumsikia mwenyewe ambapo alifunguka yake ya moyoni. Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa haumizi tena kichwa kuhusu  suala la ndoa na Diamond na kwamba hana haraka nalo. 
“Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.

“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond). 

“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi,” alisema Wema.

Paparazi wetu alimtwangia simu mama yake Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo mawili, kuhusu bintiye kuvishwa pete ya ndoa na Diamond na suala la Mbongo Fleva huyo kusema hataoa kamwe!
“Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini mnipigie mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?” alisema mama huyo kwa sauti ya utulivu.

Katika hali ya kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya kutooa au kuoa. 
Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa. Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri katika maisha yake.”

Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni wakiwa nchini Afrika Kusini, Amani lilifanikiwa kuzungumza na shehe mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa Wema ni usanii. 

“Diamond amemfanyia usanii mwenzake. Pete gani bila kufunga ndoa. Halafu katika Uislam, hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete, hayo mambo wanayafanya wenyewe, ” alisema shehe huyo.

Wema alipopewa nafasi ya kuizungumzia pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu akaamua kumnunulia na kumvisha lakini haihusiani na ndoa. 

“Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini, baby wangu akaipenda pete, akainunua na kunivalisha, haina uhusiano na ndoa,” alisema Wema.

Credit GPL.

Kesi nzito yafunguliwa tena dhidi ya Michael Jackson, mlalamikaji atoa ushahidi wa kulawitiwa utotoni

Wakati Michael Jackson akiwa amelala kwenye nyumba yake ya milele, bado familia yake imeendelea kuandamwa na tuhuma nzito zinazomhusu mfalme huyo wa Pop duniani. 
Mlalamikaji, James Safechuck mwenye umri wa miaka 36 hivi sasa ambaye alikuwa katika kesi ya Michael Jackson ya mwaka 2005 kuhusu ulawiti, ameibuka tena na kufungua kesi na kutoa ushahidi mpya wa jinsi alivyokuwa akilawitiwa na marehemu mwaka 1988 wakati akiwa mtoto mwenye umri wa miaka 10 tu.

James ambaye sasa ni baba wa familia hakuonesha ushirikiano wakati wa kesi ya mwaka 2005 licha ya kutajwa kama sehemu ya ushahidi. 

TMZ wameeleza kuwa wamepata nyaraka zilizowasilishwa na Safechuck mahakamani ambazo zinaeleza kuwa Michael Jackson alimfundisha lugha ya ishara wakati akiwa na umri wa miaka kumi, lugha ambayo alikuwa akiitumia kutaka kumueleza kuwa anataka kufanya nae mapenzi. 

Ameeleza kuwa moja kati ya ishara hizo ni pale walipokuwa wakishikana mikono kusalimiana, alikuwa anambinya au kumtekenya katikati ya kiganja. 

Katika nyaraka hizo ameendelea kueleza kuwa MJ alikuwa anamchukua na kumpeleka kwenye majumba ikiwa ni pamoja na sehemu inayoitwa ‘The Hideout’ ambapo walikuwa wakinywa vinywaji laini, pink wine na kuangalia video za ngono. 
Amesema marehemu aliendelea kumfanyia vitendo hivyo  hadi pale alipoanza kubalehe. 

Hata hivyo, mwanasheria wa Michael Jackson, Howard Weitzman ameiambia TMZ kuwa kesi hiyo inatakiwa kutupiliwa mbali kwa kuwa imeletwa kwa mara ya kwanza miaka 20 baada ya tukio hilo analolieza na kwamba James Safechuck aliwahi kula kiapo na kueleza kuwa Michael Jackson hakumfanyia kitu chochote kibaya.

Kuhusiana na madawa ya kulevya, Agnes Gerald ‘Masogange’ ahojiwa zaidi ya masaa 10 kwenye uwanja wa ndege

Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.

Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gedfrey Nzowa alisema jana kuwa Masogange alianza kuhojiwa juzi usiku baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini. 

Nzowa alisema baada ya kuhojiwa, Masogange aliruhusiwa na kwamba yupo huru, ameachiwa bila masharti yoyote. 
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani naye alithibitisha kuhojiwa kwa msanii huyo akisema: “Hapa kuna kikosi kazi, kila mmoja alimhoji kwa wakati wake lakini kwa upande wa polisi tulimpekua na kumhoji lakini tumemwachia.

Kamanda Selemani alisema Masogange alianza kuhojiwa juzi saa mbili usiku hadi jana saa nne asubuhi. 
Hata hivyo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Masogange alikana akisema kwa kifupi na kukata simu: “Hilo unalosema siyo kweli na sipo tayari kuzungumzia hilo… Siwezi kuzungumza na chombo cha habari kwa sasa, shida yako nini?” 

Masogange alitawala vyombo mbalimbali vya habari nchini katikati ya mwaka jana baada ya kukamatwa Afrika Kusini akiwa na nduguye Melisa Edward wakiwa na ‘mzigo’ wa dawa hizo zenye thamani zaidi ya Sh6.8 bilioni. 
Wasichana hao walinaswa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Nzowa alisema jana kuwa katika mahojiano hayo walimuuliza kuhusiana na ushahidi alioutoa huko Afrika Kusini kuwa dawa hizo za kulevya alipewa na mtu kutoka JNIA. “Ni kweli tulikuwa tunamuhoji Masogange ili atueleze mtu gani aliyempa crystal methamphetamine kama alivyodai kuwa amepewa na mtu wa hapa JNIA,” alisema Nzowa. 

Katika mahojiano hayo, Nzowa alidai kuwa Masogange alidai kuwa alipewa dawa hizo na mtu ambaye hamfahamu kwa jina lakini anaikumbuka sura yake. Alisema baadaye walikwenda eneo ambalo walipeana dawa hizo na mtu asiyemjua jina lake kwa ajili ya kuweza kumtambua kama alikuwapo eneo hilo. 

Chanzo: Mwananchi

Video: Msichana anayedaiwa mchepuko wa Jay Z atoa ngoma akimchana Beyonce ‘Sorry Mrs. Carter’

Inaonekana familia ya Mr and Mrs Carter haiwezi kukaa siku moja ikatulia bila kupata msukosuko. Tangu ugomvi wa kwenye lifti kati ya Jay Z na Solange, familia hiyo imeendelea kutawala vichwa vya habari kwa taarifa za mpasuko katika ndoa yao.

Na sasa rapper aitwaye Liv, ambaye amekuwa akidaiwa na mitandao ya udaku kuwa mchepuko wa Jay Z ameachia video ya akichana kwenye beat ya wimbo wa zamani wa kundi la Outcast ‘Mrs Jackson’ kurekodi wimbo wake alioupa jina ‘Sorry Mrs. Carter’ na kumchana vibaya Beyonce japo anadai hajawahi kuwa na uhusiano na rapper huyo.
Hata hivyo Liv anadai kuwa ni Jay ndiye anamtaka hadi sasa akiwa tayari amemuona Beyonce.

Tuesday, August 5, 2014

Chifu Kiumbe ajibu madai ya kuuza 'unga', asema sasa ameamua kumrudia Mungu

Mfanyabiashara maarufu ambaye amekuwa akitoa misaada mikubwa kwa wanamuziki na watu mbalimbali, Chifu Kiumbe amejibu tetesi zilizokuwa zikielezwa na baadhi ya watu kuwa anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya. 

Chifu Kiumbe amekanusha tetesi hizo katika kipindi cha ‘Mkasi’ na kueleza kuwa yeye hajawahi hata kuyaona madawa ya kulevya. 
“Sijawahi kuuza madawa ya kulevya, wala sijawahi kuona unga unafanaje katika maisha yangu. Kwanza katika maisha yangu pombe sijawahi kugusa, sigara sijawahi kugusa wala kinywaji cha aina yoyote.” Amesema Chifu Kiumbe.  

Amesema watu wengi katika jamii wana kasumba ya kumsema mtu kuwa anauza unga kwa sababu tu ana pesa nyingi kitu ambacho sio sahihi. 

Katika hatua nyingine, Chifu Kiumbe ameeleza kuwa hivi sasa ameamua kumrudia Mungu baada ya kufanya mambo mengi na kwamba anataka kujikita katika kujenga misikiti. 
“Nimeamua kurudi kwa mwenyezi Mungu. Nimefanya mengi katika hii dunia na hakuna ambacho sikijui katika hii dunia. Maisha ya kuishi duniani ni machache. Maisha mengi ni kwa mwenyezi Mungu kwa hiyo sasa nimeelekea kwa mwenyezi Mungu na hapa nilipo kiu yangu ni kufikiria jinsi gani ya kujenga misikiti.”  

Akizungumzia kitu ambacho anakijutia katika maisha yake, amesema hana anachojutia zaidi ya kuwa na jina kubwa halafu anajikuta akiandikwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa habari zisizo za kweli.  

Credit Times FM

Friday, August 1, 2014

Ni kweli Diamond Platnumz hataoa kamwe ili asishuke ki muziki!

Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa.

Kauli hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine (AFRIMMA) 2014. 

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa anahofia kuoa kwa madai kwamba akifanya hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu ambacho hataki kimtokee maishani mwake. 

Jamaa huyo ambaye siku hizi anajiita Dangote (jina la tajiri wa Nigeria, Aliko Dangote) alitiririka kuwa zamani alikuwa na wazo hilo la kuoa lakini akiwatazama wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku, makali yao hupungua na wengine kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki. 

“Unajua unaweza kuona kama vile nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli wenyewe. “Kuna wanamuziki wengi walikuwa kwenye peak (kileleni) lakini walipooa tu ‘kiki’ yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine wamepotea kabisa.

“Ukifuatilia kwa umakini wapo mastaa wengi duniani ambao umri umekwenda sana lakini hawajaoa. Hata hapa nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni kuona kuwa wakifanya hivyo watashuka kimuziki,” alisema Diamond.

Alipoulizwa kama ni kweli amemvisha pete ya uchumba Wema, msanii huyo hakuwa tayari kufafanua kwa kigezo kwamba pete ni urembo kama urembo mwingine kwa mwanamke. 

Baada ya kusikia msimamo wa Diamond, gazeti hili lilijiongeza na kutoka nje ya boksi ambapo lilizungumza na baadhi ya wasanii waliooa na wasiooa ambapo walieleza mambo mazito.

Katika mazungumzo yao kwa sharti la kutochorwa gazetini, wasanii hao walidai kwamba Diamond anahofia kupoteza kiki kwa warembo ambao wengi ndiyo mashabiki wake wanaoamini nao wanaweza kupata zali la kuolewa naye ndiyo maana humzingira na kumuomba namba ya simu kila anakokwenda.

Ilielezwa kwamba kwa kuwa jamaa huyo hupenda kuwa juu ndiyo maana alisharipotiwa kutoka na msururu wa wanawake mastaa ambao huchangia jina lake kuendelea kuwa juu.
Ilidaiwa kwamba wakati anatafuta namna ya kuchomoka kimuziki alidaiwa kutoka kimapenzi na warembo waliokuwa na majina madogo kama Rehema Fabian aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Miss Kiswahili.

Ilisemekana kwamba baada ya hapo alidaiwa kuwa na msururu wa wanawake mastaa kama waigizaji Jacqueline Wolper Massawe na Aunt Ezekiel Grayson na Jokate Mwegelo. Baadaye jamaa huyo alidaiwa kuruka na wasichana ambao hawakuwa na kiki hivyo aliwamwaga ndani ya muda mfupi kama Najma na Natasha. 

Baadaye Diamond alitua kwa Wema hadi akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba mwaka 2012 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki jijini Dar. 

Kumbukumbu zinaonesha kwamba muda mfupi baada ya kumvisha Wema pete ya uchumba walimwagana ambapo Diamond alitua kwa Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Diamond hakudumu na Penny kwa madai kwamba mrembo huyo hakuwa na kiki kama ilivyokuwa kwa Wema ambaye jina lake halijawahi kushuka tangu alipovaa Krauni ya Miss Tanzania 2006/07.

Ilisemekana kwamba hata tuzo zilipungua ndipo akampiga Penny chini na kurudi kwa Wema ambaye inasemekana ndiye anayemng’arisha. 

Hawa wameoa, je, wameshuka? 

Baadhi ya mastaa waliooa ni pamoja na Mohamed Ahmed ‘Z-Anto’, Nurdin Bilal ‘Shetta’, Amini Mwinyimkuu, Lawrence Marima ‘Marlaw’, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ na wengineo.

Chanzo GPL.

Friday, July 25, 2014

Jokate azungumzia filamu, muziki, biashara, Alikiba vs Diamond, Wema na mapenzi, msikilize hapa

Jokate Mwegelo yupo jijini Nairobi, Kenya ambapo hata hivyo hajaweka wazi ameenda kufanya nini lakini aliweza kukutana na Mzazi Willy M Tuva kwenye show ya redio inayosikilizwa zaidi nchini humo, ‘Mambo Mseto’ ya kituo cha Radio Citizen kuzungumzia masuala mbalimbali kuanzia filamu, muziki, biashara, ushindani kati ya Alikiba na Diamond na uhusiano.

Kuhusu nyimbo mpya za Alikiba  

Nimesikiliza ni nzuri, zipo tofauti, they are actually very Alikiba so I am proud of him. Pengine anataka kubadilisha muonekano wake kwasababu nikisikiliza zile nyimbo nampata Alikiba which is a good thing kwasababu kama artist lazima uwe na ile signature yako kwahiyo I still get that from him. But I think right now because ana management mpya anataka kujibrand, take it to the next level sasa hivi kwasababu kuna watu kama akina Diamond they are doing great stuff so it’s a great thing for him.

Kuhusu ushindani uliopo sasa kati ya Diamond na Alikiba  

Watu wanataka kuwashindanisha lakini kwasababu it comes with the nature of the business huyu anataka kufanya vizuri, huyu anataka kuwa on top kwahiyo mashabiki nao lazima waseme ‘muziki huu mzuri, ahh yule mzuri zaidi’ kwahiyo ni kitu cha kutegemewa. Lakini mimi nahisi kila mtu kutokana na muziki wake anaofanya, kutokana na personalities zao ambazo ni tofauti, personality ya Diamond sio personality ya Alikiba so they each have their own selling point kwahiyo sidhani kama kuna shida sana hapo.

Kuhusu ushauri anaompa Alikiba  

I just wish Alikiba achangamke kidogo, huo ndio ujumbe wangu kwake, awe more aggressive. Unajua sasa hivi artist walivyo, they are very up front like they are always on your face, he should be like that.

Kuhusu uhusiano wake na Diamond kwa sasa  


Tuko poa kwasababu tuko wote kwenye industry moja hatuwezi kuwa na beef, it will be crazy. Yeye beef yake inabidi awe na Alikiba man (anacheka).

Kuhusu nani mkali kati ya Alikiba na Diamond  

Alikiba ana fan base kubwa Tanzania wanampenda and Diamond is a hustler he does well so it’s a tie. Kila mmoja ana nafasi yake, kila mmoja anafanya muziki mzuri.

Kuhusu kama bado ana ugomvi na Wema Sepetu  

Obvious kama female mkicross paths inakuwa vile lakini we are cool, she is a great girl and it’s all love.

Kuhusu kama ana uhusiano na mtu mwingine tayari  

Nina prospects wengi.

Sikiliza interview nzima hapa.

Credit Bongo5.

Mchepuko! Achezea kichapo kwa kuchepuka na mke wa mjomba wake

TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
Mjomba wa Kelvin(Joseph) akimsihi Mpwa wake amsamehe mara baada ya kukutwa gesti na mke wa Kelvin.

Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam. 
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema:

Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.

Kufuatia taarifa hiyo, mkuu wa zamu wa OFM aliwaagiza mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao walitumia muda usiozidi robo saa kutoka walipokuwa kufika eneo la tukio ambapo walimkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!

Mapaparazi wetu bila kuzubaa nao walianza kuchukua picha za tukio  hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake. 
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za OFM.

Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana)  ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.

Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.

Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe. 

Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.

Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.

Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi. 

Credit GPL.

Tuesday, July 22, 2014

Ray C: Chid Benz ataozea jela, na haya ndiyo majibu ya Chid Benz

Nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.

NYOTA wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye hivi karibuni aliripotiwa kupokea kipigo cha maana kutoka kwa msanii mwenzake, Rashid Makwilo almaarufu Chid Benz, ameibuka na kudai kuwa atahakikisha rapa huyo anaozea jela kwa kitendo hicho alichomfanyia.

Akizungumza na gazeti hili, Ray C alisema amejikuta akipatwa na dhamira hiyo kutokana na msanii huyo, licha ya yeye mwenyewe na mama yake kumpigia simu za kutaka amsamehe, lakini anakana mbele za watu anapoulizwa, tena hadi redioni. 

Chid na mama yake wamenipigia simu kutaka nimsamehe lakini ninashindwa kwa sababu akiulizwa na watu anakataa hajanipiga, sasa kama hajanipiga anaomba msamaha wa nini, nimekwenda kwao na polisi kama mara tano lakini haonekani, inaonekana amejificha sehemu, mimi nasema awaonee haohao wasiojua sheria,” alisema msanii huyo ambaye hivi sasa anaendesha vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Chid Benz mwenye tuzo tano za Kili, licha ya kukiri kumpigia Ray C simu pamoja na mama yake, alikataa kupiga kwa ajili ya kuomba msamaha kwa sababu hakumpiga msichana huyo mkongwe katika Bongo Fleva. 

Msanii wa Bongo Fleva, Rashid Makwilo almaarufu Chid Benz.



“Mimi nimpige Ray C? Halafu achubuke mguuni? Chid Benz angempiga angepasuka sura na angevimba kila sehemu. Yeye anajua nini kilitokea lakini anasema maneno yasiyokuwepo ilimradi apate huruma ya watu. Nilishamkataza kuwa karibu na mzazi mwenzangu kwa kuwa najua kampuni yake haina future. 

“Mbona hasemi kama nilishawahi kwenda pale na kumweleza sitaki na akaniomba msamaha?
 “Mimi sikumpiga, mchubuko alioupata ni mchecheto wake tu baada ya kujikwaa na kuanguka wakati akinikimbia, mimi nichukue cheni?
Hayo ni mambo ya kizamani kwamba mtu ukimpatia sababu unasema amechukua pesa sijui na nini, siwezi kuchukua cheni ya Ray C, kwa maisha gani aliyonayo? 

“Anasema nilimpigia simu kumuomba radhi, ni kweli lakini siyo kumwomba radhi, nilimpigia na kumwambia tuachane na haya mambo, sisi wote tunaonekana mateja tu mbele za watu ambao tumeshindwana huko sasa tunataka publicity. 
“Wanaosema mimi ni mkorofi hawanijui, kama ni hivyo mbona ile kesi ya kumpiga msichana kule Ilala nimeshinda?” alihoji Chid Benz.

Monday, July 21, 2014

Maimartha Jesse ‘Mai’ aamuwa kumsuta mvulana kwa keki yenye maneno yasemayo 'Sajo acha umbea ndoa tamu'

Dume lililofahamika kwa jina moja la Lusajo au Sajo anayefanya kazi maeneo ya Kijitonyama, Dar jirani na duka la mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ amejikuta akitaharuki na kuaibika baada ya kusutwa laivu katikati ya wanawake huku akilishwa keki na kufunguliwa mvinyo kisa umbeya.
Mwanaume aliyesutwa akilishwa keki na Maimartha.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wikiendi iliyopita kabla ya gazeti hili kutua, Maimartha alidaiwa kusuka ishu hiyo huku akiwakaribisha marafiki zake kushuhudia akiwemo Flora Mvungi.

Ilisemekana kwamba Mai alidai kuwa kilio chake kwa muda mrefu ni kwamba jamaa huyo amekuwa akimfuatafuata na kumwambia mumewe, Raymond Shayo ‘Shaa’ kila jambo analolifanya dukani hapo, ikiwa ni pamoja na kumweleza watu wa kila aina wanaoingia ndani hapo. 
“Nilishapata taarifa za Sajo kuwa huwa ananichunguza, sikutaka kuwa na haraka nikaenda naye taratibu bila kumwambia kwani nilikuwa nikimtafutia dawa ya kumkomesha. Leo ndiyo arobaini yake imefika.

“Nilishika simu ya mume wangu nikakuta SMS za Sajo zikimuomba fedha, ukweli nilichukia sana na nilishangaa kuona kumbe kazi anayoifanya ya kunichunguza analipwa, nikaona sasa ndiyo wakati wa kumkomesha kwani kwa kulipwa kwake ipo siku atatunga hata uongo kwa sababu fedha ni shetani,” alisema.

Keki ya msuto aliyoandaliwa Bw. Sajo.



Sajo, kabla ya kujua kinachoendelea, alikaribishwa keki na shampeini, akaenda kichwakichwa, alipomaliza kulishwa akaambiwa asome maneno yaliyoandikwa kwenye keki ‘Sajo acha umbeya ndoa  tamu’ ndipo akachanganyikiwa na moja kwa moja msuto ukaanza huku akiulizwa ni kwa nini anamwambia maneno mume wa Mai.


“Mh! Mimi mbona siyo kweli jamani,”  alisema Sajo na kushindwa kumalizia maneno. Alipobanwa na wanahabari wetu na Gea Habibu (wa Leo Tena ya Clouds FM) juu ya kuwa na namba ya simu ya mume wa Mai, Sajo alishikwa na kigugumizi na kuondoka ambapo alikimbilia dukani kwake na kujifungia kukwepa aibu kwani siyo tukio la kawaida kwa mwanaume kusutwa kwa umbeya.

Credit GPL

Saturday, July 19, 2014

Kuhusiana na skendo ya kujiuza mwili, Odama: 'Sikwenda nnje kujiuza'

WIKI iliyopita mwigizaji Jennifer Kyaka ‘Odama’ alifafanua mambo mbalimbali aliyopitia maishani likiwemo suala la kuficha ujauzito na mambo mengine ambayo yawezekana ulikuwa huyajui juu yake. Leo tunamalizia makala haya kwa kutazama majibu ya maswali mbalimbali ambayo nilimuuliza na kuyatolea ufafanuzi. UNGANA NAYE…

Mwandishi: Wasanii mnatajwa sana kwenye masuala ya ushirikina ili mng’ae kisanii, kwa nini msimtegemee Mungu? 
Odama: Uchawi upo, huwezi kuukwepa lakini inategemea na mtu anaundekeza kiasi gani. Binafsi siamini katika hayo mambo. Namtegemea Mungu zaidi. 

Mwandishi: Malengo yenu kama kampuni ni nini katika gemu la filamu za Kibongo?
Odama: Kama kampuni malengo yetu makubwa ni kuvuka mipaka ya Tanzania na kufanya vizuri zaidi ya Wanigeria ambao wanaonekana kututangulia kimaendeleo. 

Mwandishi: Kila mtu kwenye sanaa huwa anakuwa na mtu aliyemvutia hadi kuingia, kwa upande wako, ni nani alikufanya uingie kwenye sanaa? 
Odama: Msanii ambaye alikuwa akinivutia kabla sijaanza uigizaji ni Monalisa (Yvonne-Chery Ngatwika). Uhalisia wake katika uigizaji ndiyo kitu kilichokuwa kikinivutia kwake ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye sanaa. 

Mwandishi: Wasanii wengi mnatajwa kuwa mnakwenda nchi za nje kujiuza, hili unalizungumziaje? Odama: Kila mtu ana uhuru wa kusema kile anachojisikia lakini kwa upande wangu sina ‘comment’ (maoni) kwa sababu mimi huwa nikienda nje ya nchi nafuata ishu maalum. 

Mwandishi: Ishu maalum ndiyo ipi maana hata wewe uliwahi kutajwa katika sakata hili.
Odama: Weee, uniache kabisa. Mimi mara nyingi nakwenda kwa kazi maalum. Kwa mfano safari yangu ya mwisho kwenda (China) nilifuata vifaa vya ofisi kama kamera na vitu vingine.

Mwandishi: Tunafahamu huna muda mrefu tangu ujifungue, lini sasa utaanza kuingia mzigoni au utabaki kama mkurugenzi na hutaigiza tena?
Odama: Hobi yangu ni kuigiza, siwezi kuacha fani hii kwa sababu naipenda. Nasubiri tu mtoto atimize miezi mitatu, nitaanza kazi kama kawaida. Sasa hivi ana miezi miwili. Mwandishi: Naona umekuwa bongenyanya, huoni kama inaweza kukuharibia ukapoteza mvuto wa kimwonekano utakapoanza kuigiza?

Odama: Ni kweli kwa sasa nimenenepa sana, lakini nafikiria kuanza mazoezi taratibu na nina imani mwili wangu wa kawaida utarudi tu.
Mwandishi: Kwa nini usianze sasa mazoezi, huoni kadiri muda unavyozidi kwenda na wewe unazidi kunenepa? 

Odama: Siwezi kuanza mazoezi kwa sasa kwa sababu nilijifungua kwa oparesheni hivyo lazima nikae kama miezi sita hivi ndiyo nipige mazoezi ya nguvu kuepuka kufumua mshono bure.
Mwandishi: Wasanii kwa sasa mna makundi katika mitandao ya kijamii, utakuta timu flani imemdiss flani, hivi unaona kuna umuhimu wowote kwa msanii kuwa na hizo timu? 

Odama: Mimi sioni ubaya wa kuwa na hizi timu kwa sababu zinamfanya msanii azungumze kwa ukaribu na mashabiki wake ila tatizo linakuja kwa wale ambao wanazitumia kwa kurushiana matusi, hapo ndipo tatizo linapokuja. Tukizitumia vizuri, hazina madhara.
Mwandishi: Katika maisha yako ya sanaa, ulishawahi kukwazwa na jambo au msanii mwenzako ukateseka kila wakati. 

Odama: Huwa napenda kufurahi na kusahau kila wakati, siwezi kukaa na dukuduku moyoni hivyo kama yalitokea nimeshayasahau. Sikumbuki. 
Mwandishi: Msanii gani wa kiume anakuvutia jinsi anavyoigiza kwa sasa?

Odama: Walikuwepo wengi huko nyuma ila kama ulivyosema kwa sasa namkubali zaidi Gabo, ni msanii mzuri sana sema kama watu wengi hawajamshtukia.
Mwandishi: Mashabiki wako wangependa kumjua baba wa mtoto huyo na pengine mna mipango gani?
Odama: Mtoto wangu anaitwa Jason kuhusu baba yake watamjua siku si nyingi, wasikonde! Mipango inakuja wakae mkao wa kula.Mwandishi: Asante kwa ushirikiano wako tangu mwanzo hadi mwisho.

Credit GPL.

Thursday, July 17, 2014

Ni kweli Diamond aponda raha na Wema huku akiwa kamtelekeza baba yake akiwa mgonjwa wa miguu!

Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.

“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo?
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba. 
“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”

Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.

“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.

Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV. 

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers. Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu. 

“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.

Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake. 
“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo. “Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.

Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo. 

“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza: 
“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana. 

“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo. 
“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake. 
“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.

Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

Credit GPL.

Sangoma anaswa gesti na wake za watu akidaiwa alikuwa akiwatengenezea dawa ya mapenzi

Ama kweli uswazi hakuishi vijimambo! Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa amepata aibu ya karne baada ya kunaswa ‘live’ na wake za watu kwenye gesti moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku. 
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.

Ilidaiwa kuwa mbali na kuwachezea, amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa mmoja baada ya mwingine.Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa sangoma huyo amekuwa na tabia hiyo hasa akimuona mwanamke mwenye mvuto katika hali ambayo haikueleweka mara moja humuita majina yake matatu, yaani la kwake, baba hadi la babu yake, jambo linalosababisha anayeitwa kushtuka na kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu kiundani. 

Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na kumtajiwa hadi matatizo yanayowapata ndugu zake walio vijijini na sehemu nyingine za mbali.
Kiliendelea kudai kwamba, sangoma huyo amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea hivyo kuwachanganya na kumjengea imani kuwa ni ‘fundi’ wa masuala hayo.

Kufuatia vituko vyake, juzikati mume wa mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa), Huruka Hassan alirejea nyumbani kwake na kukuta mkewe hayupo.Alidai alipofanya uchunguzi wa haraka, aligundua ameenda kwenye gesti hiyo kupata tiba.

Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba lakini siku ya tukio machale yalimcheza, alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza ukumbini na kusikia sauti ya mkewe ikinong'ona chumbani na sauti ya 'besi' la sangoma huyo kwa mbaaali.

Ilisemekana kwamba uzalendo ulimshinda Huruka na kujikuta akivunja masharti ya kilinge cha sangoma huyo kwa kuchungulia kwenye tundu la kupitisha funguo."Haaamadi!" alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa kumfanyia ‘amshaamsha’.

Ilidaiwa kuwa Huruka alishindwa kujizuia, akagonga mlango kwa hasira ambapo sangoma alivaa 'chapchap' na kufungua.Ilielezwa kwamba walipokutana uso kwa uso, Huruka alitunishiana misuli na sangoma huyo wakataka kuzichapa lakini jamaa akaona amchukue mkewe na kutimka naye. 

Baada ya mke wa Huruka kuokolewa kufanyiwa ukenge, mwanamke mwingine wa eneo hilo, Tabu Abdallah naye alidai kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa amekalishwa kama alivyozaliwa, akitolewa vitu fulani tumboni na sangoma huyo. 

Akizungumza na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publisher ambayo ilifika eneo hilo usiku baada ya kutonywa na chanzo chake, Tabu alisema alimnasa mkewe na sangoma huyo baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia gesti hiyo. 

Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake jambo. Baada ya kutokea kwa mtiti huo, Mjumbe wa Shina namba 29, Azimio-Tandika, Faraj Neto, wanawake waliodhalilishwa, waume zao, polisi na mmliki wa gesti hiyo, Ebenezer Ngowo, walimchomoa sangoma huyo kwenye gesti hiyo. 

Katika hali ya kushangaza mke wa Tabu alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka kumpiga mganga wake ambaye alikuwa akitaka kummalizia matatizo huku wanawake wengine wakiwaomba radhi waume zao na kudai walirubuniwa.

Akizungumizia mkasa huo mke wa Tabu alisema kuna siku alikutana na mganga huyo njiani ambapo alimwita majina yake matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo akaanza kumtajia matatizo yake, jina la mama yake mzazi na kumwambia mama huyo huko aliko ana tatizo sugu la miguu jambo ambalo ni kweli ndipo alianza kumuamini. 

Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa nyumba kumi alimtaka sangoma huyo kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti hiyo alimtaka mganga  huyo kuhama kwenye gesti yake kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake. 
Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumuua.

Credit GPL.

Wednesday, July 16, 2014

Lulu azua kihoja kwa wasanii wa Marekani waliopo nchini, akiwadai namba za Justin Bieber!

Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, hivi karibuni alijikuta akiendelea kuwehukia penzi la mwanamuziki Mkanada anayefanya shughuli zake nchini Marekani, Justin Drew Bieber (20), Amani  lina cha kushika mkononi.

Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Ishu hiyo ilitokea Julai 14, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa BoT uliopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam ambapo wasanii wa Marekani waliotinga Bongo kwa mwiliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ walikuwa wakitoa semina kwa wasanii wa Bongo.
Lulu ambaye kwa miaka mingi amekuwa akiweka wazi mapenzi yake kwa Bieber alifika ndani ya ukumbi huo na kumwambia staa mwenzake wa sinema, Zuweza Mohamed ‘Shilole’ kwamba lengo la kufika kwake ni kuwaomba wasanii hao namba za simu za Bieber. 

Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa mbinu za namna ya kukuza na kupanua soko la muziki na sanaa zote Tanzania. 
Semina ilianza saa 3:00 asubuhi na wasanii wa Bongo waliitikia wito kwa kufika mapema, lakini Lulu alizama ukumbini hapo saa 8:12 mchana.

Lulu alishuhudiwa akiwasili ndani ya ukumbi huo kwa  mbwembwe nyingi huku akimwambia Shilole kwamba ametia timu kwa lengo la kuchukua namba za simu za mpenzi wake wa moyoni, Bieber kwa  vile alijua miongoni mwa Wamarekani hao lazima mmoja atakuwa na mawasiliano ya msanii huyo. 

Mwanahabari wetu, baada ya kuyanasa mazungumzo ya Lulu kwa Shilole, alianza kumfuatilia staa huyo hatua kwa hatua kama kweli atamvaa mmoja wa wasanii hao na kumuomba namba za simu za Bieber! 
Lulu alikwenda kukaa kwenye kiti mbele kidogo huku wasanii wengine wa Bongo wakiwa kwa nyuma yake na akaanza kufuatilia semina hiyo ilivyokuwa ikiendeshwa kwa usahihi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtoa semina mmoja alilitaja jina la Bieber katika mfano wa maelezo ya kuzingatia, ndipo Lulu akashtuka na kujishika sehemu ya kushoto kifuani kisha akamwelekea meneja wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ’Diamond’, Babu Tale ambaye alikuwa karibu yake na kumwambia maneno haya: “Naona sasa hawa Wamarekani wanaanza kugusa ninapopataka mimi.” 

Baada ya semina kumalizika, baadhi ya wasanii wa Bongo walipiga picha za pozi na Wamarekani hao huku Lulu akienda chemba kuzungumza na Diamond, jambo lililotafsirika kuwa huenda alitaka msanii huyo amfanyie wepesi wa kukutana na Wamarekani hao kwa vile yeye alikuwa huko hivi karibuni akiwania Tuzo za BET.

Mpaka mwisho, Lulu aliondoka kimyakimya tofauti na alivyowasili huku paparazi wetu akiendelea kumfuatilia. 

Baadaye mwandishi wetu alimpigia simu ya mkononi staa huyo na kumuulizia kama alikipata alichokuwa amekikamia ndani ya ukumbi huo.Paparazi: “Lulu nilikusikia pale ukumbini ukimwambia Shilole kuwa lengo lako kubwa la kwenda ni kuipata namba ya simu ya Justin  Bieber, vipi uliipata?”
Lulu: “Of course ni kweli nimekuwa nikimpenda Bieber tangu alipoibuka na Wabongo wanajua hilo, maana nimekuwa nikimsifia na kumzungumzia, ila pale ukumbini nilipongia Shilole ndiye alianza kwa kuniambia nimekwenda kuchukua namba ya Bieber.

“Hata mimi nilimkubalia kuwa ninavizia watakapomaliza kutoa semina niipate namba ya Bieber lakini sikumaanisha sana jamani!” 
Paparazi: “Je, ulipokwenda kuongea na Diamond nini ilikuwa hoja yako kwake, akuunganishe nao?”
Lulu: “Mambo mengine bwana. Kuna wakati Shaka Zulu (mmoja wa wagane hao) naye alimzungumzia Justin Bieber na baada ya kutaja jina tu nilishtuka sana, nilitaka nione akina Diamond watasemaje?”

Mwaka 2011 baadhi ya magazeti pendwa ya Bongo sanjari na mitandao ya kijamii yaliripoti jinsi Lulu alivyopagawa na mwanamuziki huyo kiasi cha kushindwa kuvumilia na kujianika kwenye ukurasa wake wa Twitter. 
Lulu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kuwa, kwa jinsi anavyompenda staa huyo alikuwa tayari kumpa chochote kile (hakufafanua). Alikuwa ‘akitwiti’ kwa Kiswahili wakati mwingine akitumia ‘yai’ (Kingereza).
Katika maelezo yake Lulu alikaririwa akisema kuwa endapo staa huyo atatua Bongo, atatembea utupu kutoka nyumbani hadi sehemu ambayo Bieber atakuwa anapafomu. 
Bieber mwenyewe anadaiwa kuwa na mashabiki zaidi ya 47,180,630 wanaomfuatilia kwenye Twitter hivyo huenda ilikuwa vigumu kumsoma Lulu.

Hivi karibuni ambapo hata mwezi mmoja haujapita wakati Diamond akiwa nchini Marekani kwenye Tuzo za BET, Lulu alimtupia kwenye Instagram maneno haya: “Hongera kwa levo uliyofikia. Huko ulinionea Justin Bieber wangu?” 
Ni nadra katika jamii ya Kiafrika mwanamke kuanika hisia za mapenzi yake kwa mwanaume asiyekuwa na habari naye huku jamii ikijua au kutambua hilo lakini Lulu amethubutu. Je, inakuwaje hapo?

Credit GPL.

Mtoto wa miaka 8 aiba benki kwa kutumia iPad!

Kuna baadhi ya matukio ya kivamizi tumezoea kuyaona kwenye filamu za kipelelezi huku yakituacha midomo wazi na sifa zote zinaenda kwa mtayarishaji, muongozaji na waigizaji wa filamu hiyo. 

Lakini hili ni tukio halisi na sio filamu, unapodhani kuna usalama wezi hubuni mbinu ambazo hata hazifiriki kirahisi. 

Maafisa wa Plainfield, New Jersey, Marekani walijikuta katika wakati mgumu wakimsaka mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye anadaiwa kuiba bank kwa kutumia iPad yake tu. 

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa sita mchana Jumatano June, 25 mwaka huu katika beki inayoitwa Greater Plainfield Bank & Trut. Maafisa walifika katika eneo la tukio haraka kuungana na walinzi kumsaka mtoto huyo baada ya kupigiwa simu na mkuu wa ulinzi wa bank hiyo ambapo awali walidhani alikuwa anatania. 

Walipofika eneo la tukio, wafanyakazi wa benki hiyo walieleza jinsi ambavyo tukio hilo limetokea, ambapo mtoto huyo kwa utulivu alitembea hadi kwa mmoja kati ya tellers ambaye jina lake halikutajwa. 

Alipofika kwa teller huyo kwa utaratibu tu alimpa iPad iliyokuwa na message juu iliyosomeka ‘giv me all of th money I hav a gun n my bookbag’. Kwa uoga mfanyakazi huyo ambaye aliishia kuuona mkono na iPad zaidi, alimkabidhi pesa zinazokadiriwa kuwa $12,000 na mtoto huyo alifanikiwa kuvuka mlango tu na kuchukua ‘motorized scoote’ akatoweka haraka kwenye jengo hilo. 

Camera za jengo hilo zinamuonesha mtoto huyo aliyekuwa amevaa fulana nyekundu iliyoandikwa mbele ‘TURN DOWN 4 WHAT?’. Na anaonekana akitereza na begi lenye pesa begani kwake.  Hakuna shuhuda mwingine aliyeshtukia wakati wa tukio hilo zaidi ya mfanyakazi wa benki.

Tuesday, July 15, 2014

Ramadhani yamaliza beef la Wema na Penny!

Star wa filamu Tanzania Wema Sepetu.
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.”
Mtangazaji wa DTV Peniel Mungilwa ‘Penny’

Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Linah aelezea wivu, majivuno na majungu yanavyowatafuna wasanii wa kike

Idadi ndogo ya wasanii wa kike Tanzania waliofanikiwa kimuziki na mbio za baadhi yao kuishia sakafuni husababishwa na mengi, lakini kumbe wao binafsi ni sehemu kubwa ya sababu za kuwapunguza kwenye mkondo mkubwa wa muziki.

Akiongea na Tovuti ya Times Fm, msanii wa kike, Linah ambaye ni mmoja kati ya wasanii watano wa kike Tanzania wanaopiga hatua kubwa kimuziki na kuleta ushindani ameelezea wadudu wanaoshambulia maendeleo ya muziki ya wasanii wa kike Tanzania.

Mimi nachoweza kusema ni wivu. Yaani sisi wasichana tuna wivu. Nakumbuka kuna wasichana kama wawili nilishawahi kuwafuata nikawaambia bana kuna wimbo huu hapa tufanyeje. Mtu aah sijui nini na nini…maneno pembeni ‘ah kwa sababu anaona mimi sasa hivi niko hivi na hivi’, yaani mambo kama hayo wasichana tunayo. Yaani hutaki mwenzio afanikiwe, unataka wewe tu ndio ukae na uwe wewe tu. Na ndio maana wasichana kwenye muziki tuko wachache kuliko wanaume. Yaani tuna ile tabia ya kwanini.” Ameeleza.

Amesema kwa upande wake alivyopata nafasi ya kwenda kufanya kazi Afrika Kusini alifikiria jinsi ya kuwavuta na wasichana wengine na kusafisha njia kama anavyofanya Diamond. Lakini badala yake wengi wameanza kumpiga majungu kuhusu safari yake.

Kwa sababu kuna maneno nimeshayasikia, yaani hivi nakwambia nimerudi nasikia ‘oooh ana mabwana, sijui kapelekwa. Which is not true kwa sababu mimi niko kazini. Hata kama napelekwa niko kazini na kuna faida naipata. Wewe ambaye uko hapo na unafanya muziki umefanya kitu gani? Nimesaini mikataba mikubwa na kampuni kubwa na sio mchezo. Lakini mara ‘oh katika hayo makampuni aah mabwana’, unajua watoto wa kike. Kwa hiyo vitu kama hivyo vinaturudisha nyuma huwezi ukafanikiwa hata siku moja. Lakini ukivaa miwani ya bati ukasonga mbele basi unafanikiwa.” 

Amefunguka Asterina  Sanga aka Linah.  Ameeleza kuwa wasanii wengi wa kike wa Tanzania hujivuna na ndio sababu ya kutokuwepo collabo za wasanii wakubwa wa kike.

Angalia wenzetu Shakira na Rihanna wametoa wimbo unafanya vizuri, wanaonekana. Shakira na Beyonce walifanya wimbo. Sijui akina Kelly Rowland na wengine wengi. Hapa ulishasikia collabo ngapi za wasanii wakubwa wa kike kwa sisi tuliopo? Zaidi ya mimi na Khadija ambayo imetoka juzi.

Amefafanua kuwa yeye aliamua kufanya wimbo na Khadija kwa sababu anaelewa kuwa yeye ni msanii mkubwa akifanya na msanii mpya wa kike na yeye atazidi kuwa mkubwa na ndio sababu hakuringa kama wengi wanavyofanya.

Linah ameachia kipande cha video yake mpya aliyoifanya Afrika Kusini na kampuni ya GodFather ‘ Ole Themba’.


Girlfriend wa Chris Brown aelezea vita kati yake na Rihanna

Girlfriend wa Chris Brown, Karrueche Tran ambaye hivi mapenzi yake na mwimbaji huyo yamekuwa ya kuachana na kurudiana mara kwa mara, ameelezea changamoto anazokutana nazo kwa kuwa na mtu aliyekuwa mpenzi wa Rihanna mwenye mashabiki wengi duniani. 
Akiongea na Just Keke, Karrueche ameeleza kuwa kutokana na umaarufu wa Rihanna ambao anaamini ni maarufu zaidi ya Chris Brown, amekuwa katika vita na mashabiki zaidi ya milioni 14 wa Rihanna. 

Katika hali hii boyfriend wangu ni mtu maarufu ambaye mpenzi wake wa zamani ni maarufu hata zaidi yake… kwa hiyo, sio tu kama napambana na yeye tu (Rihanna), napambana na mashabiki wake milioni 14 au vinginevyo.” Alisema Karrueche. 

Hebu vuta taswira, najisikiaje pale napoingia Twitter na kutakana na mambo yote …wanafanya kila kitu cha ajabu (crazy) na ni kama hawafahamu chochote kuhusu mimi.”Aliongeza. 

Mrembo huyo alisisitiza kuwa amejaribu kuwa na mtazamo chanya katikati ya mapenzi hayo ya pembe tatu (Chris Brown, yeye na Rihanna) lakini amekiri kuwa inamuwia vigumu sana.

Fumanizi: Mke wa mtu achanjwa kwa viwembe

MWANAMKE mmoja,  Rehema Juma (21) ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Mtaa wa Msamvu B, Kata ya Kihonda Maghorofani mkoani Morogoro amechanwa na nyembe mwilini na baadaye kutembezwa bila nguo mtaani mchana kweupe akituhumiwa kufumwa na mume wa mtu.

Tukio hilo la aina yake  ambalo lilivuta umati mkubwa, lilitokea Julai 5, mwaka huu saa 10 jioni katika Mtaa wa Msamvu B. 

Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mwandishi wetu walidai kuwa kwa muda mrefu, Zaitun Ally (30) ambaye pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu Rehema akidai anatembea na mumewe, hivyo akaamua kutega mtego bila mafanikio. 

Zaituni baada ya kushindwa kuwanasa leo aliamua kumuita Rehema nyumbani kwake na kudai amewafuma na mumewe hivyo kumchana nyembe baadaye kumvua nguo na kumtembeza bila nguo mtaani hadi nyumbani kwake umbali wa mita 300 mchana kweupe,” alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Ashura Ally.

Mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Rehema na kumkuta akiwa amefungwa bendeji sehemu za mwili wake na alipoulizwa alifafanua:
Ni kweli tukio hilo limetokea lakini siwezi kuzunguma peke yangu, twende kwa mama mkwe Mtaa wa Ngerengere.” 

Mwandishi wetu na Rehema walipofika kwa mkwe wa mtuhumiwa, Lilian Julius Sechonge ambaye ni mjumbe wa serikali za mtaa wa Ngerengere na kutakiwa kuzungumzia tukio hilo alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli Rehema ni mkwe wangu kwa mwanangu aitwaye Godfrey Sechonge anayeishi naye hadi sasa, Julai 5, mwaka huu mwanangu huyo alikuja na akaniambia mkewe anatembezwa bila nguo.
“Nilifika eneo la tukio na kumkuta mkwe wangu yuko uchi huku akivuja damu mwili mzima. 
“Aliniambia amecharangwa viwembe na Zaituni akimshutumu kutembea na mumewe, nilimchukua mwanangu na kumkimbiza polisi ambapo tulipewa PF3 na kufunguliwa jalada namba MOR/RB/4009/2014.”

Naye Rehema alipozungumzia kisa hicho alisema siku ya tukio saa 4 asubuhi, Zaituni alimtuma mwanaye nyumbani kwake na kumuomba aende kwake (Zaituni). 

“Nilipofika kwake aliniingiza ndani na kuniwekea kisu shingoni huku mwanaye akinirekodi na simu yake, akaniuliza nimetembea mara ngapi na mumewe! “
Alitaka kujua pia amenihonga shilingi ngapi, kwa hofu ya kuchinjwa nilikubali kwamba nilitembea naye mara moja na alinipa shilingi elfu tano. “Baada ya kusema hivyo akaniachia, nikarudi nyumbani. 

Saa kumi aliniita tena, nilipofika nikamkuta yuko na mumewe na watoto wao, akaniuliza unamjua huyu? Nikamwambia simjui, akatoa simu na kufungua mahojiano, mumewe alipojaribu kumpora, akamchanja na wembe.

“Ghafla akahamia kwangu na kuanza kunichanja kwa wembe huku nikipiga kelele na akanivua nguo kisha akanitoa nje na kunipeleka kwangu nikiwa na nguo ya ndani tu,” alisema Rehama.              

Akizungumza na mwandishi wetu diwani wa kata hiyo, Lydia Mbihaji alisema tangu aanze kuongoza watu hajawahi kukutana na tukio kama hilo ambalo aliliita ni la kinyama. Tayari Rehema amelifikisha sakata hilo polisi na Zaituni alikamatwa na kuwekewa dhamana na mumewe akisubiri kuburuzwa mahakamani wakati wowote. 

Baada ya kudhaminiwa, mwandishi wetu aliwashuhudia Zaituni na mumewe wakizungumza na Rehema ambapo inadaiwa wanataka ipatikane suluhu kabla kesi haijaanza kuunguruma mahakamani.

Monday, July 14, 2014

Isome hapa kuhusiana na Wema kulizwa mamilioni na mwarabu

Staa wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu.
KUNA STAA wa sinema za  Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa filamu Bongo mwenye asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la Chidy kwa kuingia mitini na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri filamu zake mbili lakini kazi haikufanyika.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect. 

MALIPO YAFANYWA, KAZI HAKUNA 

Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri (editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni. 

JAMAA AINGIA MITINI, AMKWEPA WEMA 

Habari zikazidi kudai kwamba, baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ndipo wiki iliyopita mlimbwende huyo akalazimika kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar es Salaam.

GHARAMA ZA FILAMU 

Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, alimsikia Wema akisema filamu zote zimemteketezea shilingi milioni 70,000,000 mbali na hizo alizomlipa huyo mhariri wa filamu ambazo zikiingizwa kwenye gharama nzima inafika shilingi 75,000,000. 

KAMA ZINGEINGIA SOKONI 

Habari zaidi zinasema kwamba kama filamu hizo zingehaririwa mwaka jana na kuingizwa sokoni, Wema angekunja mkobani kiasi cha shilingi 140,000,000 hivyo kurudisha gharama za kuandaa (75,000,000) na faida juu (65,000,000). 

WEMA ASWAKWA, AKATAE AU AKUBALI 

Kufuatia maelelezo hayo kutoka chanzo chetu, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimsaka mrembo huyo ili afunguke kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alipopatikana na kuulizwa sakata zima hakuwa tayari kupepesa macho, akakiri.

Alisema awali kijana huyo aliyemdhulumu alikuwa mfanyakazi wake katika kampuni ‘mufilisi’ ya Endless Fame, cha ajabu toka ampatie hiyo kazi ya kumtengenezea pamoja na kumkabidhi fedha amekuwa akimchenga toka mwaka jana. 

Mimi nashindwa hata kumuelewa ana dhumuni gani na hizo kazi zangu maana hapo ana kama shilingi milioni 140 zangu, kwa kuwa kila kazi nilikuwa nalipwa shilingi milioni 70, nilishafanya makubaliano na Kampuni za Proin Promotion  na Steps kuwapa filamu zangu lakini yeye ananizungusha, toka kipindi kile sijaende China, nikimuuliza majibu yake siyaelewi.

WEMA AMWAGA CHOZI, MTUHUMIWA MBARONI 

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wema aliendelea kulalamika  mpaka kufikia hatua ya kumwaga chozi: “Juzi kati Mtitu alitaka nifanye naye kazi lakini akanikumbushia Filamu ya Super Star, kwamba hajaiona sokoni mpaka sasa, ndipo nikamuelezea, akasema hawezi kukubali niipoteze kirahisi, lazima nisimame kidete kuipata ndiyo nikaenda naye mpaka Kituo cha Polisi Mabatini kufungua kesi na Chidy akakamatwa siku hiyo hiyo.”  

APEWA SIKU SABA 

Wema aliendelea kusema: “Polisi walimpa siku saba ahahakikishe ananikabidhi kazi zangu pamoja na kompyuta  moja ambayo aliichukua ofisini kwangu bila ridhaa ya mimi mwenyewe na akagoma kuirudisha.” 

AFISA WA POLISI 

Naye afisa mmoja wa polisi wa kituo hicho ambaye alizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini alithibitisha Wema kufungua kesi Mabatini na ikapewa jalada Namba KJN/RB/5850/14 WIZI WA KUAMINIWA 3/7/2014.
Ukweli ni kwamba zikipita siku saba bila kijana huyo kuleta fedha na kompyuta ya Wema hapa polisi, tutamsaka na tukimkamata sheria itachukua mkondo wake,” alisema afisa huyo wa polisi. 

UPER STAR, OMOTOLA ALIFIKA 

Kama itakumbukwa sawasawa Filamu ya Super Star ilizinduliwa Juni 24, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar na nyota wa muvi za Nollywood (Nigeria), Omotola Jalade Ekeinde alishiriki.

Credit GPL.