Chifu Kiumbe amekanusha tetesi hizo katika kipindi cha ‘Mkasi’ na kueleza kuwa yeye hajawahi hata kuyaona madawa ya kulevya.
“Sijawahi kuuza madawa ya kulevya, wala sijawahi kuona unga unafanaje katika maisha yangu. Kwanza katika maisha yangu pombe sijawahi kugusa, sigara sijawahi kugusa wala kinywaji cha aina yoyote.” Amesema Chifu Kiumbe.
Amesema watu wengi katika jamii wana kasumba ya kumsema mtu kuwa anauza unga kwa sababu tu ana pesa nyingi kitu ambacho sio sahihi.
Katika hatua nyingine, Chifu Kiumbe ameeleza kuwa hivi sasa ameamua kumrudia Mungu baada ya kufanya mambo mengi na kwamba anataka kujikita katika kujenga misikiti.
“Nimeamua kurudi kwa mwenyezi Mungu. Nimefanya mengi katika hii dunia na hakuna ambacho sikijui katika hii dunia. Maisha ya kuishi duniani ni machache. Maisha mengi ni kwa mwenyezi Mungu kwa hiyo sasa nimeelekea kwa mwenyezi Mungu na hapa nilipo kiu yangu ni kufikiria jinsi gani ya kujenga misikiti.”
Akizungumzia kitu ambacho anakijutia katika maisha yake, amesema hana anachojutia zaidi ya kuwa na jina kubwa halafu anajikuta akiandikwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa habari zisizo za kweli.
Credit Times FM