Diamond Platinumz ambaye jina lake halisi la dini ya kiislamu ni Naseeb Abdul ameshambuliwa Instagram na baadhi ya mashabiki baada ya kupost picha akiwa beach huko ughaibuni huku ameshikilia kamba iliyomfunga mbwa.
Mashabiki wengi walimshambulia wakielekeza point yake kwenye suala la imani ya dini ya kiislamu huku wakiunganisha tukio hilo na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Rashyalhambeshy: ramadhan acha kupost pc zisizo eleweka ww umaaruf ww una umaaruf km mtume muhammad s.w.a na yote kakataza acha mambo yk ayo jua kuna kufa muangalie firauna laanatullah ila me lng jicho. na ktk dini tumeambiwa tukumbushaneni me nimekemea kwa mdomo ok.
Hata hivyo sio wote waliomshambulia, wapo wengi pia waliomtetea kwa points tofauti kama Leanlilie aliyetumia point hiyo hiyo ya imani.
leanlilie :I jus keep wondering who a u to judge another person?kumhukumu mwenzio tuu ni dhambi wew je ni mwema sana?huu ni wakati wa toba jisalie na uombee makosa yako,mwachie Allah ndio mtoa hukumu we Tanzanians tumezidi jaman khaaaaa!!can we atleast think abt our sins and pray acheni watu ma maisha yao.!
Nimejaribu kuwauliza watu wawili watatu ambao wamejikita katika masuala ya dini ya kiislamu kuhusu picha hiyo na imani ya dini hiyo, lakini wao wamenieleza kuwa sio kosa kumgusa mbwa bali ni haramu ‘mbwa kumnusa muumini wa dini ya kiislamu’.
Tafakari pia, mambo ya imani yanahitaji zaidi ya upeo wa kawaida.
Thursday, July 3, 2014
Picha ya Diamond akiwa na mbwa yazua kasheshe, Je ni kweli Dini hairuhusu?
Labels:
Entertainment,
Gospel,
Gossip