Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Friday, July 25, 2014

Kanye West afunga camera kibao kwenye nyumba anayoishi ili kumuona mwanae North hata akiwa ziarani

Kanye West amefunga idadi kubwa ya camera kwenye nyumba yake ili kumchunga na kumuona binti yake, North popote pale duniani.

Rapper huyo mwenye miaka 37 amedaiwa kumkera mke wake Kim Kardashian kwa kufunga camera hizo kwenye kila chumba ndani ya nyumba yao ya Los Angeles hadi kwenye bafu ili kuhakikisha anamuona North muda wote. 

Chanzo kimoja kimesema: Kanye anamchunga sana North na anataka kuhakikisha anamuona wakati akiwa mbali ziarani. Hivyo ameongea na kampuni ya LA iitwayo VIA international kuinstall ‘high-tech cameras’ katika nyumba yake nzima. Kisha ataweza kuwa na link ya moja kwa moja ya nyumba yake na kumuangalia North kwa chochote atakachokuwa anakifanya akiwa popote duniani. Kanye ana utaratibu wake kichwani wa jinsi anavyotaka mwanae alelewe na anataka kuona kuwa utaratibu huo unafuatwa.” 

Chanzo hicho kilichoongea na gazeti la Daily Star kiliongeza: Lakini Kim hajafurahishwa na mpango huo. Anachukia wazo la kuangaliwa muda wote. Alimuambia Kanye kuwa anahisi haamini uwezo wake (Kim) wa kulea.” 

Hata hivyo chanzo hicho kimedai kuwa Kanye hana wasiwasi na ulezi wa mke wake kwa North bali mara nyingi hummiss mwanae. Rapper huyo anadaiwa kutaka North awe na ratiba ya kucheza na midoli ya kumfundisha, kufanya yoga ya watoto na kuogelea kila siku. 
Alimuambia Kim kuhakikisha kuwa mtoto wao anacheza na watoto wengine walau mara nne kwa wiki.