Mjukuu wa rapper na muigizaji Ice-T amekamatwa na polisi wiki iliiyopita baada ya kumfyatulia risasi kwa bahati mbaya rafiki yake anaeishi nae chumba kimoja.
Kwa mujibu TMZ, polisi waliuambaia mtandao huo kuwa kijana huyo anaefahamika kwa jina la Elyjah Marrow alikuwa ameshikilia bunduki katika chumba chake huko Georgia na bahati mbaya risasi ikafyatuka na kumpiga rafiki yake, Daryus Johson mwenye miaka 19.
Kwa mujibu wa polisi, walipofika katika eneo la tukio walimkuta kijana huyo na baada ya kumpekuwa walipata madawa ya kulevya aina ya marijuana ambayo alikuwa na nia ya kuyauza. Kijana huyo amefunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusidia, kukutwa na bangi na kumiliki bunduki ambayo ilitajwa kuwa ya wizi.
Marrow aliwahi kuonekana kwenye reality show ya Ice Cube, “Ice Loves Coco.”
Wednesday, July 2, 2014
Mjukuu wa Ice-T akamatwa baada ya kumuua rafiki anaeyeishi nae chumba kimoja kwa kumpiga risasi
Labels:
Entertainment,
News