Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Sunday, July 6, 2014

Mtoto wa Eminem apewa tuzo ya heshima shuleni

Bintiwa rapa Eminem, Hailie Jade Scott Mathers, amehitimu masomo yake kwa kupata alama za heshima kutoka kwenye Shule ya upili wa juu ya Valley (Valley High School) iliyopo kwenye mji Clinton, Michigan Juni 8. 
Baba Eminem na mwanaye Hailie Jade Scott Mathers (kulia) ambaye amepewa tuzo ya heshima shuleni kutokana na kufanya vizuri kwenye masomo yake.
Hailie hakuwahi kupata alama za chini kwa kipindi cha miaka minne aliyokuwa akisoma hapo. 

Binti huyo alipewa tuzo ya heshima ya Academic Excellence Award, ya Idara ya Saikolojia ambapo tuzo hiyo hupewa mwanafunzi aliyeweza kudumisha GPA ya 3.9. 

Mipango ya binti huyo ni kutaka kusoma masomo ya saikolojia au ujasiriamali kwenye Chuo Kikuu cha Michigan (Michigan State University). 

Mtoto huyo hakuacha kuwashukuru wazazi wake kwa mafanikio yake, alisema“Mama na baba yangu wamekuwa wakisukuma kuwa mtu niliye leo, na wamenipa msaada wa kufanikisha nilichonacho leo hii”. 

Wasanii wa Tanzania tungependa kusikia watoto wenu wakifanya vizuri shuleni, huenda wewe hujawahi kupata elimu, ila kipaji kikasuadia kutoka mtegoni basi ni vyema ukasomesha wanao kama unao.