Mtunzi wa muziki na msanii wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Tanzania Lil Seven ambaye hivi sasa anafanya vyema na kichupa chake kilichobatizwa jina 'Misosi Mitamu' ameelezea kuwa anajiandaa kufanya kolabo zaidi na wasanii nchini.
Lil Seven ameiambia eNewz kuwa hivi sasa ana imani na prodyuza wake anayeitwa Sulesh katika kazi zake zinazofuata kwani Sulesh ameweza kujijengea jina haswa baada ya kumtoa dogo Aslay na wimbo wake unaoitwa 'Naenda kusema kwa Mama'.
Lil Seven anayefanya kazi chini ya studio ya Eyoo Music ya jijini Dar es Salaam ameelezea kuwa baada ya kutoa kibao chake cha kwanza alichokibatiza jina 'Isome' aliomshirikisha msanii Dully Sykes, mipango yake ya sasa ni kufanya remix ya wimbo wake 'Misosi Mitamu' na mkali Ally Kiba.
Tuesday, July 1, 2014
Mtunzi wa muziki na msanii wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Tanzania Lil Seven asaka kolabo
Labels:
Entertainment