Huku Wamerekani wakisherehekea siku ya uhuru (Julai 4), familia ya Obama wao walikuwa na kitu kingine cha kusherehekea, nacho ni Malia Obama kutimiza umri wa miaka 16 (Sweet 16).
Binti wa kwanza, ambaye hivi karibuni alionekana akichukua mafunzo ya televisheni mjini California, alikuwa na miaka 10 wakati baba yake alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Miaka sita imepita, nchi hiyo imemshuhudia akikuwa, mrefu, mpenda mitindo, binti anayepevuka, akiwapa wazazi wake sababu nyingi za kujivunia naye.
|
Mama akiwakumbatia wanawe walipokuwa kwenye ziara ya siku sita nchini China Machi, 2014 |
|
Barack Obama akitembezana na malkia wake katika viunga vya White House Januari, 2014 |
|
Rais Barack Obama akiwa na mwanawe Malia Obama wakishuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, Julai 2013. |
|
Ndugu wa pekee Malia (kushoto) na Sasha Obama wakiwa kwenye Ukuta wa Berlin, Ujerumani Juni 2013. |
|
Rais Barack Obama akiwa na binti yake Malia Obama ambaye ametimiza miaka 16, siku ya Jualai 4, ambayo pia ni siku ya sherehe za uhuru wa Marekani. |