Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Saturday, July 5, 2014

Pigo kwa Brazil, Neymar ‘nje’ Kome la Dunia 2014

Mshambuliaji wa Brazil Neymar ameondolewa kwenye Kombe la Dunia baada ya kuvunjika mfupa mgongoni kwenye mechi ya robo fainali ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Colombia. 

Neymar, 22, alikuwa akitokwa machozi wakati akibebwa kutolewa nje na kupelekwa hospitali mjini Fortaleza.  Kocha Luiz Filipe Scolari alisema: “Neymar alikuwa akiwindwa, hii imekuwa ikitokea kwenye mechi tatu.” 

Daktari wa timu Rodrigo Lasmar aliiambia Tv ya Michezo ya Brazil, “Kwa bahati mbaya, hatoweza kucheza, anasikitika sana”.
“Ni jambo la kawaida kwa maana ya kwamba hakuhitajiki upasuaji, ila anahitaji kupumzika ili apone”. 

Lasmar aliongeza kwa kudai kwamba anahitaji majuma kadhaa ili aweze kupona. 
Neymar alipona majeraha ya paja na goti na kuweza kucheza mechi ya ushindi dhidi ya Chile na Colombia.