Msanii wa Hip Hop,Joseph Haule aka Professor Jay jana alikitembelea chama cha Haki Miliki Tanzania ‘COSOTA’ na kuwauliza kwanini Radio na TV za Tanzania haziwalipi wasanii pindi wanapoziga nyimbo za wasanii kwenye vituo vyao.
Akizungumza na Bongo 5,Professor Jay alisema kuwa baada ya kupeleka shauri hilo, wahusika ambao ni COSOTA wamesema wapo kwenye vikao kulijadili.
“COSOTA sio watu wa mwisho , wameniambia kuna vikao vingine vinaendelea ,tuweke subira lakini hili suala linajadiliwa kila siku. Lakini tuseme kweli haya mambo yanatakiwa yaanze ingawa kumekuwa na changamoto , hata wasanii wenyewe wanafanya muziki kama muziki ilimradi wanajifurahisha lakini kama watakuwa serious vyombo vya habari ‘Radio na Tv’ zinawalipa watu maana yake hata wasanii wenyewe watakuwa serious kufanya muziki kuwa perfect na itachuja upi mchele zipi pumba, naamini hivyo vyombo haviwezi kukubali kumlipa mtu ambaye yupo shaghalabaghala ambao hawafanyi muziki unaoeleweka,” alisema Professor.
Wednesday, July 2, 2014
Professor Jay aongea na COSOTA kuhusu utaratibu wa redio na TV kuwalipa wasanii kwa kucheza kazi zao
Labels:
Entertainment